Akizindua soko kuu jipya la Karikoo leo, Februari 8, 2026, Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wasimamizi wa soko hilo kuhakikisha suala la usafi linazingatiwa ipasavyo, ikiwemo miundombinu ya majitaka.
Amesema kuwa miundombinu ya soko hilo ikisimamiwa vyema itachangia kuwepo kwa mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wananchi wanaotumia soko hilo.
Itakumbukwa kuwa mara kadhaa baadhi ya wadau wamekuwa wakilalamikia kero ya majitaka katika mitaa mbalimbali ya Karikoo, wakidai kuwa suala hilo ni changamoto inayohitaji suluhu, kutokana na kusababisha kadhia ya harufu na kuhatarisha usalama wa afya za wananchi.
Angejikita zaidi kwenye chanzo cha kuungua kwa soko
kwanini liliungua na tume yake mbovu ilifikia wapi?
wafanye nini hali hiyo isijurudie tena?
Ajabu bi chura yeye anaongelea majitaka na mitaro!