Rais Samia, Watanzania kuruhusiwa kufanya kazi Kenya tuepushe na mtego huo

Rais Samia, Watanzania kuruhusiwa kufanya kazi Kenya tuepushe na mtego huo

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Kuna maamuzi ambayo kihistoria unajua tu huo ni mtego mbaya sana! Hatuhitaji ruhusa kama hiyo ambayo ni nadharia tu! Kenya Mkikuyu hawezi kuajiliwa na Mluo. Mluo naye hawezi kuajiliwa na Mkikuyu. Ni hivyo hivyo kwa makabila mengine. Maana yake, hakuna ajira kwa M-TZ, labda kama ni kuzoa uchafu.

Wakenya wanahofia TZ kiasi kwamba hawataki hata apewe ajira za ofisi za UN ambazo siyo za Serikali yao. Mama Tibaijuka anaelewa alivyokuwa anapigwa vita na Wakenya. Wako tayari nafasi ichukuliwe na mtu wa nje ya EAC kuliko Mtanzania.

Mtego huu uliwahi letwa hapa kwenye suala la ardhi eti waruhusiwe kumiliki ardhi TZ na Watanzania waruhusiwe kumiliki ardhi Kenya. Ilishindikana maana TZ tulijua hakuna uwezekanao wa m-TZ kumiliki ardhi Kenya.

Rais epuka mtego huo usio na faida kwa Tanzania.
 
Kuna maamuzi ambayo kihistoria unajua tu huo ni mtego mbaya sana! Hatuhitaji ruhusa kama hiyo ambayo ni nadharia tu! Kenya Mkikuyu hawezi kuajiliwa na Mluo. Mluo naye hawezi kuajiliwa na Mkikuyu. Ni hivyo hivyo kwa makabila mengine. Maana yake, hakuna ajira kwa M-TZ, labda kama ni kuzoa uchafu. Wakenya wanahofia TZ kiasi kwamba hawataki hata apewe ajira za ofisi za UN ambazo siyo za serikali yao. Mama Tibaijuka anaelwa alivyokuwa anapigwa vita na Wakenya. Wako tayari nafasi ichukuliwe na mtu wa nje ya EAC kuliko m-TZ.

Mtego huu uliwahi letwa hapa kwenye suala la ardhi eti waruhusiwe kumiliki ardhi TZ na wa-TZ waruhusiwe kumiliki ardhi Kenya. Ilishindikana maana TZ tulijua hakuna uwezekanao wa m-TZ kumiliki ardhi Kenya. Rais epuka mtego huo usio na faida kwa TZ.

asili ile ile ya kudanganywa na chips mayai na pipi....
 
asili ile ile ya kudanganywa na chips mayai na pipi....
Mama Samia anahitaji kusaidiwa, kuna namna flani anataka kuthibitisha kuwa anaweza bila kujali jinsia yake.... Yaani ni ile mnanichukulia poa kwa sababu ni mwanamke ngoja niwaonyeshe ! Tabu ni kwamba kwenye hizo harakati zake wajanja wanapenyezea agenda zao zinaenda
i hope kuna wa kumsaidia hata kama itakuwa ni nyuma ya pazia. Mabeyo ? I hope so.
 
Kuwekeza Kenya nishuguli pevu saaana kuliko kuwekeza Tanzania. Wakenya wanawinda ardhi . kumbukeni hata enzi za hayati, raisi wa Kenya aliwahisema watanzania ruksa kuoa Kenya . Mungu atupiganie
Wakati wenyewe ardhi yote bado inamilikiwa na akina Lord Delamere na familia za kisiasa za akina Kenyata na oligarchs wengineo.

Cheza na watu wote lakini usicheze na Mkenya. Nilifanya kosa la kumtumia mmoja kama referee wangu kwenye kazi moja nzuri ajabu. Weeeh! Nilikosa ile kazi na nilipofuatilia memba mmoja wa hiring committee akaniambia kuwa kulikuwa na recommendation letter moja ilikuwa mbaya mno; na akamtaja jina yule Mkenya. Nilishangaa kwa sababu jamaa alikuwa mshikaji sana na tulikuwa tumefanya kazi pamoja sehemu mbalimbali duniani japo yeye alikuwa senior kidogo. Wana roho mbaya ajabu!
 
Akubali yote but kwenye ardhi hapana.Ardhi iendelee kumilikiwa na masikini.Leo maisha yakinishinda dar Nakwenda popote kulima na kujisajili mwanakijiji ID yangu tu maisha yanaendelea
 
Back
Top Bottom