Mimi sioni mtego wowote hapo, Kama umeruhusiwa kwenda kufanya kazi kenya bila working permit bado vigezo vitazingatiwa lazima utakuwa na utambulisho wako wa wewe ni Nani? Na sijaona sehemu wakisema ukanunue ardhi huko na wao pia siamini Kama wataruhusiwa kuja kununua ardhi huku, hayo ni mambo ya mahusiano ya kibiashara zaidi Ili kuchangamsha akili zetu na kuondoa uvivu wa watanzania na tunaogopa wasije Ili tuzidi kulala, wewe ukiwa na hela yako kenya ni sehemu ya kwenda kujifunza practical ya utengenezaji wa vitu au kuongeza thamani malighafi tulizonazo sasa hizo working permit huoni zitakukwamisha? Angalia wenye mitaji wanavyo copy bidhaa kenya na kuzitengeneza hapa na sasa hivi tunawaita mamilionea, Sabuni za miche na unga, maziwa, viungo na jinsi ya kupaki, hebu twendeni kenya tukachue ujuzi tumepata hiyo nafasi, hata wao wakija watakuja na hela Kama ni nyumba watalipa kodi kwani watakuja kukaa huku bure? Na vigezo na mashariti vitazingatiwa huwezi kuambiwa ruhusa kufanya kazi wewe ukakimbilia kununua kiwanja.