Rais Samia, Watanzania kuruhusiwa kufanya kazi Kenya tuepushe na mtego huo

Rais Samia, Watanzania kuruhusiwa kufanya kazi Kenya tuepushe na mtego huo

Kuna maamuzi ambayo kihistoria unajua tu huo ni mtego mbaya sana! Hatuhitaji ruhusa kama hiyo ambayo ni nadharia tu! Kenya Mkikuyu hawezi kuajiliwa na Mluo. Mluo naye hawezi kuajiliwa na Mkikuyu. Ni hivyo hivyo kwa makabila mengine. Maana yake, hakuna ajira kwa M-TZ, labda kama ni kuzoa uchafu.

Wakenya wanahofia TZ kiasi kwamba hawataki hata apewe ajira za ofisi za UN ambazo siyo za Serikali yao. Mama Tibaijuka anaelewa alivyokuwa anapigwa vita na Wakenya. Wako tayari nafasi ichukuliwe na mtu wa nje ya EAC kuliko Mtanzania.

Mtego huu uliwahi letwa hapa kwenye suala la ardhi eti waruhusiwe kumiliki ardhi TZ na Watanzania waruhusiwe kumiliki ardhi Kenya. Ilishindikana maana TZ tulijua hakuna uwezekanao wa m-TZ kumiliki ardhi Kenya.

Rais epuka mtego huo usio na faida kwa Tanzania.

Itakuwa laana kama tutauza baraka ya mzaliwa wa kwanza kwa bakuli ya dengu kama Essau.
Mama usiruhusu hilo litokee
 
Upo sahihi na hapo ndipo tunatakiwa kuwa makini. Ukweli ni kwamba hakuna nchi inayotaka kupitwa kimaendeleo na nchi ingine. Ila wahenga walisema "Mchawi mpe mwanao akulelee "

USA na China zinaupinzani Mkali sana kiuchumi lakini USA ndio nchi yenye uwekezaji mkubwa China especially kwenye upande wa viwanda.
Leo hii ukimwambia USA avifunge viwanda vyake china hatokuelewa, pia China ukimwambia aviondoe viwanda vya USA vilivyoko nchini mwake hatokuelewa sababu hapo kuna win win situation, yani kila mmoja anaangalia ni nini anakipata na sio ni nini mwenzake anakipata.

Kuna Shida gani kama ushirikiano wetu na Kenya itaonekana Kenya ndio mfaidika mkubwa japo sisi hatupotezi chochote na pia tunapata faida ya kutosha japo sio ya kufuru kama atakayoipata mshirika mwenzetu?
Tatizo la Kenya siyo kutafuta balance ya biashara, ni kutafuta kutatua matatizo yake ya ndani aliyoyatengeneza. Tukizubaa anahamishia matatizo kwetu na hatutakuwa na sehemu ya kuyapeleka. Kila wakati anatuvutia ili apewe nafasi ya nafasi za kazi na umiliki wa ardhi.
 
Wakenya wanavizia ardhi tu Tz, Mama anahitaji kuwa makini sana
Ni kwel kabisaa..ardhi yao yote ipo kwa wazungu na chache wamegawana kenyata na kina raila..yaan akikosea tu kuruhusu kenyans...heee..na wabongo tulivyo wepesi kuuza ardhi..kesho tuu kila kitu nje.
 
That is Kenyan style, not TZ style! Sisi tunaangalia zaidi ya familia, bhana! Kenya ni familia. Ndo maana kila siku ni mashindano ya wezi tu.
Endelea kufunga macho ukidhani kwenyu ndio hakuna wezi, huku wajanja wenyu wakiwakamua vizuri 'chini ya maji'... Hawakosi watu ka hao! Wewe endelea kungoja vya kupewa bure!
 
Naiona tz inakuja kua kama south. Yaani wazawa watakavyozidiwa na wageni mwishowe hasira ziwashike waanze kuwatimua. Aki wakenya wako far away inapokuja suala la skill.
 
Naiona tz inakuja kua kama south. Yaani wazawa watakavyozidiwa na wageni mwishowe hasira ziwashike waanze kuwatimua. Aki wakenya wako far away inapokuja suala la skill.
Tusiombe ifike huko, Afrika ni yetu sote. Tusitoane nguo bure, kule mabeberu yanatucheka. SA ilishajitia doa tayari kwa wenzao Waafrika.
 
Endelea kufunga macho ukidhani kwenyu ndio hakuna wezi, huku wajanja wenyu wakiwakamua vizuri 'chini ya maji'... Hawakosi watu ka hao! Wewe endelea kungoja vya kupewa bure!
Get whatever you want from the other neighbours. Achana na TZ. Kwani unakosa nini Somalia? Ethiopia?, etc.
Nchi gani hiyo watu wanaishi kama wakimbizi kila siku? Ardhi yote imechukuliwa na kuwaancha wengine ni squatters.
 
Ushakuwa msemaji wa Mh. Suluhu? Hata hakujui, so hata sijui tunabishana nini na wewe. Wacha tubaki kuwa wakimbizi, hayo hayakuhusu,ila ujue KE tutabaki kuwa majirani zenyu mpaka kiama!
 
Kuna maamuzi ambayo kihistoria unajua tu huo ni mtego mbaya sana! Hatuhitaji ruhusa kama hiyo ambayo ni nadharia tu! Kenya Mkikuyu hawezi kuajiliwa na Mluo. Mluo naye hawezi kuajiliwa na Mkikuyu. Ni hivyo hivyo kwa makabila mengine. Maana yake, hakuna ajira kwa M-TZ, labda kama ni kuzoa uchafu.

Wakenya wanahofia TZ kiasi kwamba hawataki hata apewe ajira za ofisi za UN ambazo siyo za Serikali yao. Mama Tibaijuka anaelewa alivyokuwa anapigwa vita na Wakenya. Wako tayari nafasi ichukuliwe na mtu wa nje ya EAC kuliko Mtanzania.

Mtego huu uliwahi letwa hapa kwenye suala la ardhi eti waruhusiwe kumiliki ardhi TZ na Watanzania waruhusiwe kumiliki ardhi Kenya. Ilishindikana maana TZ tulijua hakuna uwezekanao wa m-TZ kumiliki ardhi Kenya.

Rais epuka mtego huo usio na faida kwa Tanzania.
Unaweza kuwa ni mtego kwa mawazo yako.
Ajira si lazima ziwe zile za maofisini,WaTanzania kwa umoja wao wanaweza kutumia vikundi vyao vya uzalishaji mali na kuuza bidhaa zao katika masoko ya Kenya.
mfano :
1.Kuanzisha soko kubwa la kuuza madini yanayopatikana EAC. (wachimbaji wadogo wadogo)
2.Kuanzisha masoko ya bidhaa za utalii,kilimo na ufugaji. (Ajira kwa wadau wa kilimo, ufugaji na utalii)
3.Kuanzisha Makampuni ya Majenzi na Usimamizi yatakayo kuwa yanafanya kazi ndani ya Kenya na Tanzania na hasa kuijenga Upya South Sudan.(Ajira kwa vijana wetu waliopo na watakao hitimu)
4.Kuimalisha sekta za Uvuvi na Usalama wa Mipakani (Ajira kwa vijana wetu wa Ulinzi)
5.Kuimalisha ulinzi wa mazingira kwa matumizi ya nishati endelevu (Ajira za moja kwa moja kwa Makampuni yetu kuwekeza Kenya kama ambavyo yamefanikiwa kuwekeza Tanzania)--Ongezeko la pato la Taifa.
 
Kwa uzoefu wake katika siasa na diplomasia ya hizi nchi, nahisi haya usemayo Mama anayajua vizuri sana tu. Katika biashara na mambo mengine, kukaa na adui yako au mnafiki ni kitu cha kawaida. Nadhani Mama anajua ni maslahi yapi anayoyapa kipaumbele kwa waTz na yapi hayapi kipaumbele (mf. nadhani sisi tunachotaka ni biashara zaidi na kuuza bidhaa zetu kwao, kuongeza utalii n.k, lakini sidhani kama tunahitaji ajira zao, wao wanataka kuingia na kuuza bidhaa na pia kumiliki ardh, hapa hawataruhusiwa) na huenda tukayaona haya mbeleni. Sisi wananchi wa Tz nasi tuwe makini na tuwe tayari kwa ushindani.
Ktk haya unayoyasema, mtu aliekuwa anaaminika pasi na shaka ni mwendazake, kwa mama nadhani anategemea sana washauri ambao wengi si waaminifu, uzoefu umeonyesha.
 
Ktk haya unayoyasema, mtu aliekuwa anaaminika pasi na shaka ni mwendazake, kwa mama nadhani anategemea sana washauri ambao wengi si waaminifu, uzoefu umeonyesha.
Tuzidi kumuombea Mama na washauri wake pia na tuwajengee wananchi nyoyo za kuhoji na kuchambua masuala ya nchi yao na uwazi uwepo ili pale tunapoibiwa tuone na tupaze sauti. Nadhani Mwendazake alifanikiwa kuonyesha kuwa yeye ni mgumu na jeuri ila sioni kama ina maana alikuwa ni bora katika haya pasi na shaka. Tumpe Mama muda tuone tutafika wapi.
 
Jitahidi uwezo wako wa kuona mbali! Tunaozungumza haya tumeishi Kenya na tunaijua Kenya!! Unyang'au Kenya ni sifa ya kujivunia wakati undugu Tanzania ni sifa ya kujivunia! Kwa mentality ya undugu ya Tanzania huwezi kutoboa Kenya! Tumetofautiana sana!! Hakuna fursa za kumfaa mtanzania wa kawaida Kenya! Kwa mfano graduate wa Tanzania hawezi kupambania maisha Kenya kwa kuanza na zero!! Lakini mkenya anaweza kuanza na zero hapa Tz na akafanikiwa! Hatujisifu watanzania kuwa hivyo lakini ndivyo ilivyo!
Mji upgrade sasa Ili muweze kupanda juu ndo hivyo viongozi wenu washakubali mjichanganye mkizubaa na kutamani kubaki chini wenyewe watakuja kuwekeza na huo ujanja wao wanaendelea kuwa juu.
 
Kenya haiongozwi na kauli za Rais kama ilivyo Tz. Mama SSH ukijiroga na kunasa mtegoni, Watanganyika tutaidai Tanganyika yetu kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom