Akizungumza leo jijini Dodoma wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Rais Samia ameeleza kuwa bila kuwepo kwa amani na utulivu, mafanikio yote yaliyofikiwa katika sekta za uzalishaji hayataweza kuwa na maana yoyote kwa taifa.
Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuwa macho dhidi ya viashiria au watu wanaolenga kugawa au kuchochea mfarakano miongoni mwa wananchi na kuhatarisha amani ya nchi.
“Niwasihi Watanzania wenzangu tuendelee kuilinda amani ya nchi yetu na tuwe macho dhidi ya yeyote anayetaka kutugawa, kutuchochea na kututumia kuhatarisha amani na utulivu tulionao. Tusimpe nafasi mtu wa aina hiyo,” -Amesema Rais Samia