Rais Samia: Watanzania tuwe macho dhidi anayetaka kutugawa, kutuchochea na kututumia kuhatarisha amani na utulivu tulionao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani, usalama na utulivu wa nchi, akieleza kuwa ndio msingi mkuu wa maendeleo na mafanikio yote yanayopatikana katika sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi.

Akizungumza leo jijini Dodoma wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Rais Samia ameeleza kuwa bila kuwepo kwa amani na utulivu, mafanikio yote yaliyofikiwa katika sekta za uzalishaji hayataweza kuwa na maana yoyote kwa taifa.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuwa macho dhidi ya viashiria au watu wanaolenga kugawa au kuchochea mfarakano miongoni mwa wananchi na kuhatarisha amani ya nchi.

“Niwasihi Watanzania wenzangu tuendelee kuilinda amani ya nchi yetu na tuwe macho dhidi ya yeyote anayetaka kutugawa, kutuchochea na kututumia kuhatarisha amani na utulivu tulionao. Tusimpe nafasi mtu wa aina hiyo,” -Amesema Rais Samia
Watawala wanapenda sana kuhubiri amani kwa sababu inawafanya wajae madarakani kwa raha mustarehe. Ukiwaomba na wenyewe wakupatie haki wewe mwananchi ili uilinde hiyo amani; wanakuona ni gaidi, mchochezi, mkosoaji, mhaini, nk.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani, usalama na utulivu wa nchi, akieleza kuwa ndio msingi mkuu wa maendeleo na mafanikio yote yanayopatikana katika sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi.

Akizungumza leo jijini Dodoma wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Rais Samia ameeleza kuwa bila kuwepo kwa amani na utulivu, mafanikio yote yaliyofikiwa katika sekta za uzalishaji hayataweza kuwa na maana yoyote kwa taifa.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuwa macho dhidi ya viashiria au watu wanaolenga kugawa au kuchochea mfarakano miongoni mwa wananchi na kuhatarisha amani ya nchi.

“Niwasihi Watanzania wenzangu tuendelee kuilinda amani ya nchi yetu na tuwe macho dhidi ya yeyote anayetaka kutugawa, kutuchochea na kututumia kuhatarisha amani na utulivu tulionao. Tusimpe nafasi mtu wa aina hiyo,” -Amesema Rais Samia
Watekaji,wauaji,wapora chaguzi,chawa,wazalendo feki ndiyo wanatufikisha kote huko,tujiulize tunaongea tunayodhamiria ,tunayo amini ama tunaongea mazuri huku tuki maanisha tofauti,huwa dhamiri inaenda mbali ya maneno hadi kufikia imani sii za kiitikadi ila za kidini na uhalisia aliodhamiria Muumba wa dunia na vilivyomo.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani, usalama na utulivu wa nchi, akieleza kuwa ndio msingi mkuu wa maendeleo na mafanikio yote yanayopatikana katika sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi.

Akizungumza leo jijini Dodoma wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Rais Samia ameeleza kuwa bila kuwepo kwa amani na utulivu, mafanikio yote yaliyofikiwa katika sekta za uzalishaji hayataweza kuwa na maana yoyote kwa taifa.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuwa macho dhidi ya viashiria au watu wanaolenga kugawa au kuchochea mfarakano miongoni mwa wananchi na kuhatarisha amani ya nchi.

“Niwasihi Watanzania wenzangu tuendelee kuilinda amani ya nchi yetu na tuwe macho dhidi ya yeyote anayetaka kutugawa, kutuchochea na kututumia kuhatarisha amani na utulivu tulionao. Tusimpe nafasi mtu wa aina hiyo,” -Amesema Rais Samia
Anaonesha tayari anayo ajenda yake kuhusu tume aliyoiteua jana.
 
Back
Top Bottom