Rais Samia: Watanzania tuwe macho dhidi anayetaka kutugawa, kutuchochea na kututumia kuhatarisha amani na utulivu tulionao

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079

Your browser is not able to display this video.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani, usalama na utulivu wa nchi, akieleza kuwa ndio msingi mkuu wa maendeleo na mafanikio yote yanayopatikana katika sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi.

Akizungumza leo jijini Dodoma wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Rais Samia ameeleza kuwa bila kuwepo kwa amani na utulivu, mafanikio yote yaliyofikiwa katika sekta za uzalishaji hayataweza kuwa na maana yoyote kwa taifa.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuwa macho dhidi ya viashiria au watu wanaolenga kugawa au kuchochea mfarakano miongoni mwa wananchi na kuhatarisha amani ya nchi.

“Niwasihi Watanzania wenzangu tuendelee kuilinda amani ya nchi yetu na tuwe macho dhidi ya yeyote anayetaka kutugawa, kutuchochea na kututumia kuhatarisha amani na utulivu tulionao. Tusimpe nafasi mtu wa aina hiyo,” -Amesema Rais Samia
 
STFU we muuaji.

Kila unapofungua domo lako unatema pumba tu.

Kulazimisha kuwa Rais na kuidanganya dunia eti umechaguliwa kwa 98% ya kura, unadhani hilo linawafanya watu washikamane?

Mburula wa Kizimkazi.

🖕
 
Chura kiziwi at work. Hamna mtu kalipeleka taifa pabaya kama limshangazi.

Your browser is not able to display this video.
 
Mambo yote ya hovyohovyo na mabaya kwa Tanganyika ameyatengeneza huyohuyo Samia kwa kiburi chake,kutosikiliza hoja za wengine,kutokuwa mtulivu,kupokea ushauri mbovu/mbaya,kutaka kuonesha umwamba na kukosa akili njema ya maono kwa nchi na mustakabali wa baadaye.Asimtupie mtu yeyote lawama.Hizo ni zake na atazijutia milele.
 
Duuuu Wacha niwe macho na uvccm
 
Inamana watu wa malawi hadi leo hii hawajafahamu matumizi ya BEWKRAD?

Kama wenyewe wa malawi wameshindwa kwa kuhofia kufanywa kama yule mtanga, basi wafanyie kazi BEWKRAD.

NEMTIH wamo wa kutosha sana watawasaidia sana, kivyovyote jiteteeni watu wa malawi hata ikibidi changianeni muwalipe hao NEMTIH.

Mnawapa SEMAN ya vyawa wote wamalizwe ili HANDRED akose nguvu.

#Hallelujah!!!
 
“Niwasihi Watanzania wenzangu tuendelee kuilinda amani ya nchi yetu na tuwe macho dhidi ya yeyote anayetaka kutugawa, kutuchochea na kututumia kuhatarisha amani na utulivu tulionao. Tusimpe nafasi mtu wa aina hiyo,” -Amesema Rais Samia
Familia za waliotekwa na kuuawa zinaiona hiyo amani?
 
Ujumbe muhimu kwa watanzania wapenda amani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…