Rais Samia: Watanzania Wananiita Mama na hapa Kenya Odinga mnamwita baba, hivyo tunamuunga mkono kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Africa

Rais Samia: Watanzania Wananiita Mama na hapa Kenya Odinga mnamwita baba, hivyo tunamuunga mkono kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Africa

Sisi tuna Rais hatuna mama.

Mama kila mtu anaye wakwake.

Machawa tu ndio wanamtafutia angle ya kumpiga wakaona the soft spot ni kumuita mama na yeye akajaa.
 
Rais Samia amesema Tanzania inamuunga mkono Raila Odinga kama Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU

Rais Samia amesema Watanzania wanasema " baba anatosha"

Soma Pia: Rais Samia kwenda Kenya kushiriki katika Hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Raila Odinga

Source Citizen TV
Hakuzungumzia chochote juu ya "African Union" na uongozi wake?

Kaenda Nairobi kwa gharama kubwa kwenda kusema mipasho ya "Mama na Baba" wa Tanzania na Kenya?

Kuna viongozi hapa Afrika akili zimelala, lakini huyu wetu atakuwa katika ligi yake mwenyewe.
 
Ina maana kubwa Sana kwenye siasa. Kumbuka Mama anakubalika Sana na kuheshimika ukanda huu wa Afrika mashariki , hiii imekuwa kama fursa kwa rais Rutto kurudisha nchini Hali nzuri ya hewani baada ya kadhia za GEN- Z. UWEPO wa Ruto kumuunga mkono Baba na Mama wa afrika mwenye jina la usuluishi( SULUHU) Kutaondoa mess na kuunganisha watoto waliokuwa na itikadi tofauti
 
Wakenya watanufaika na fursa za Africa ni wabinafsi sn watabebana wenyewe, sisi tuna Spika wa mabunge duniani hajawahi hata kumuombea mtanzania kazi ya ulinzi getini
 
Hakuzungumzia chochote juu ya "African Union" na uongozi wake?

Kaenda Nairobi kwa gharama kubwa kwenda kusema mipasho ya "Mama na Baba" wa Tanzania na Kenya?

Kuna viongozi hapa Afrika akili zimelala, lakini huyu wetu atakuwa katika ligi yake mwenyewe.
Ndiyo anachoweza kusafiri pekee, akirudi ataanza kuteua kesho
 
Raila nae ni ccm tu
Nasikitika kusema, lakini nafikiri huyo bwana ni zaidi ya CCM kwa ubovu wake. Akipata nafasi hiyo ya uenyekiti wa Komisheni, ni kwa sababu ya washindani wake kuwa dhaifu zaidi au vi-nchi vyao kutokuwa na uzito wa ushawishi mkubwa kuwaunga mkono wagombea wao.

Ni sawa na huyo 'Spika' wa Mabunge tuliye naye hapa kwetu alivyo weza kunyakuwa nafasi hiyo.
 
Alikuwa anakwenda sana Chato enzi za Shujaa Magufuli 😄😄🌹
Walisoma pamoja na kukaa chumba kimoja bwenini Magufuli na Odinga wakisoma chuo kikuu cha Dar es salaam .Ulitakaje urafiki wao ufe kisa mmoja mkenya mwingine mtanzania au kwa kuwa wako vyama tofauti?

Urafiki wao umedumu toka wakiwa wanasoma
 
Back
Top Bottom