Rais Samia: Watu 13 wamefariki kwenye jengo lililoporomoka Kariakoo. Serikali kugharamia matibabu ya majeruhi na kuhakikisha waliofariki wanasitiriwa

Je, hakuna hatua za kisheria na kinidhamu? Ni kina nani waliohusika na usimamizi na uthibitishaji wa kazi iliyokuwa ikiendelea?
Kwanza fahamu vitu viwili:
1. Mmiliki wa jengo utakuta ana ubia na ccm (au ni chawa kindaki ndaki kama Lucas Mwashambwa).
2. Mkandarasi utakuta ni miongoni mwa wale walionunua ndege na kuijaza mafuta kwa ajili ya kampeni za SSH.

Kifupi upepo utatulia. Tutasahahu na kusonga mbele!
 
Kifo ni kifo tu uhai wa watu wengine kwake sio kipaumbele.

Alisafiri tukio likiwa limeshatokea kuhutubia taifa akiwa ugenini ni aibu kwa Tanzania na Africa kwa ujumla.
 
Hivi ndivyo uwezo wa chadema wa kufikiri ulipofikia.
Acha mbowe aendelee tu kujichotea mabilioni ya ruzuku

Mimi sina kadi ya chama chote cha siasa , tatizo ni uwezo mdogo wa kujibu hoja na kukimbilia kusema siasa.
Ila tuambiane ukweli , hivi kweli wewe nyumbani kwako kumetokea msiba unaweza kusafiri kweli? Unafikiri ndugu zako watakuelewaje hata kama msiba umeshatokea kwamba hata ukisafiri huwezi kuzuia huo msiba , ila kwa kweli ukisafiri utaeleweka vibaya tu.
Acheni kuingiza siasa kwenye masuala ya utu na ubinadamu.
Rais ameonyesha ni mtu asiye na ubinadamu na asiye jali
 
Haya matangazo angerudi ayafanyie nyumbani kuonyesha kujali maisha ya watu wake.
 
Sijajua mola ana mpango Gani na ccm ili tuishi kwa amani ya kweli
 
Maigizo tupu
 
13×-------- =
Idadi hawawezi itoa iliyo sahihi
Wanajua watu mtapagawa

Ova
 
Yule aliyesema "Labda mambo yawe yameharibika sana" nafikiri atusaidie. Maana kama ni mambo kuharibika, yameharibika sana!
 
Hivi tuna raisi kweli nchi hii? Nchi ina msiba wewe raisi unaondoka nchini kwenda kutalii huko huku unaacha msiba nyumbani. Utakuwa baba wa ajabu sana unaacha msiba nyumbani kwako unaenda sherehe kwa jirani.
Viongozi wetu wa kiafrika huwa wanaona wananchi wake kama nyani vile.hawajali kabisa.


Ingekuwa nchi zinazojielewa raisi angeahirisha safari kabisa. Ila sasa huku kwetu kusadidika wananchi watajiokoa na kujipigania wenyewe.

Najua kuna chawa watakuja hapa kumtetea mama yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…