Rais Samia: Waziri wa Nishati aliondoa Tozo kwenye mafuta kimakosa kwa sababu Tozo ilipitishwa na bunge, Nimeirejesha!

Rais Samia: Waziri wa Nishati aliondoa Tozo kwenye mafuta kimakosa kwa sababu Tozo ilipitishwa na bunge, Nimeirejesha!

Tunaopata tabu ni Sisi UVCCM,maana ilipoondolewa tulisifia na asahivi imerejeshwa hatuna budi kusifia hivyo hivyo.
 
Wanawaza wao wapate ata kama mwananchi ataumia ilo wao haliwahusu. Unasema gharama za kusafirisha vitu toka china zimepanda maradufu , muda huo huo unaongeza urasimu pale bandarini.
 
Mama anasema Waziri wa fedha aliondoa Tsh 100 kwenye bei ya mafuta lakini akairudisha kwasababu moja ilikuwa imeshapitishwa kwenye bajeti na pili isingeleta unafuu wowote kwa walaji katika kipindi hiki cha mfumuko.

Swali langu kwanini Waziri aliamua kuondoa hiyo tsh 100 wakati Bunge lilikuwa limeshapitisha? Je alitaka kumchonganisha Rais na Bunge? Alilidharau Bunge? Alipitiwa? Ana mamlaka hayo kwa mujibu wa sheria? Au ndio yale mambo ya watu watatu kukaa na kuamua kukopa au kubadilisha matumizi ya mkopo kwa niaba ya Taifa?
 
Mie simshangai Mwigulu, nashangaa Wabunge na Wanasiasa hasa wa Upinzani pamoja na vyombo vya habari vilivyopiga kimya uvunjifu huu wa sheria

Spika msomi kuliko wote waliowahi kutokea Ndugu Tulia nae alitulia…mchambuzi wa kujitegemea wa Uchumi na Bajeti Ndugu Zitto nae kimya…mwanasheria Nguli Antipas Lissu nae Kimya. JF nako tukapiga kimya!

Hadi kina Fatma Karume na Maria Sarungi nao kimya

Tuliandika humu kuwa tutalipia gharama ya kumzodoa Ndugai, na ndio hii watu wanakosea hadi wanagundua wenyewe wanajirekebisha sie tupo kimyaaa tu kwa kuwa tunaogopa mashambulizi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu toka Njombe kwa mikwala

Zogo la Katiba mpya limeanzishwa upya ili kuficha mengi sana maana sote tuko busy kwny hili, nawakumbusha. Escrow ilipigwa wakati tupo busy na Heka heka za Rasimu ya Warioba

Tume ingeundwa kuchunguza hili maana sio kawaida kwa ukimya huu
 
Mama anasema Waziri wa fedha aliondoa tsh 100 kwenye bei ya mafuta lakini akairudisha kwasababu moja ilikuwa imeshapitishwa kwenye bajeti na pili isingeleta unafuu wowote kwa walaji katika kipindi hiki cha mfumuko...
Lengo lilikuwa hawasaidie nyie matahila,mnunue mafuta kwa Bei ya chini, au kakosea?
 
Uchumi vyanzo vya mapato ni sawa na mishipa ya damu kwenye mwili wako na wanyama, ukikata ghafla damu itatoka weeeee hadi kuhitaji kuongezewa. budget process inaishia kwa bunge kupitisha mafungu ya matumizi na mapato na hadi kutungia sheria.

Tulishangaa tuliposikia moja ya vyanzo vya mapato imenyofolewa kienyeji bila kurudi kwenye approving authority. Budget ni sheria ukipunguza budget au kuongeza budget ya nchi bila utaratibu ni kuvunja sheria na katiba. Hapo chachaa kazi kwenu.
 
Mama anasema Waziri wa fedha aliondoa tsh 100 kwenye bei ya mafuta lakini akairudisha kwasababu moja ilikuwa imeshapitishwa kwenye bajeti na pili isingeleta unafuu wowote kwa walaji katika kipindi hiki cha mfumuko...
Mwigulu ana matatizo kichwani mwake, asamehewe tu.
 
Haikuondolewa na Mwigulu hacheni propaganda iliondolewa na January


 
Mie simshangai Mwigulu…nashangaa Wabunge na Wanasiasa hasa wa Upinzani pamoja na vyombo vya habari vilivyopiga kimya uvunjifu huu wa sheria

Spika msomi kuliko wote waliowahi kutokea Ndugu Tulia nae alitulia….
Sheria ngapi zimevunjwa au ni hiyo tu ndiyo umeona?
 
Hivi ni nini kinaendelea duaniani?Rais anasema kontena la fut 40 kusafirishwa kwa sasa ni dola 8000.wakati ilikuwa ni dola 1500.
Nisaudieni kwa data za bandari za karibu
 
Back
Top Bottom