Mie simshangai Mwigulu…nashangaa Wabunge na Wanasiasa hasa wa Upinzani pamoja na vyombo vya habari vilivyopiga kimya uvunjifu huu wa sheria
Spika msomi kuliko wote waliowahi kutokea Ndugu Tulia nae alitulia…mchambuzi wa kujitegemea wa Uchumi na Bajeti Ndugu Zitto nae kimya…mwanasheria Nguli Antipas Lissu nae Kimya…Jf nako tukapiga kimya!
Hadi kina Fatma Karume na Maria Sarungi nao kimya
Tuliandika humu kuwa tutalipia gharama ya kumzodoa Ndugai…na ndio hii… watu wanakosea hadi wanagundua wenyewe wanajirekebisha sie tupo kimyaaa tu kwa kuwa tunaogopa mashambulizi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu toka Njombe kwa mikwala
Zogo la Katiba mpya limeanzishwa upya ili kuficha mengi sana maana sote tuko busy kwny hili… nawakumbusha …Escrow ilipigwa wakati tupo busy na Heka heka za Rasimu ya Warioba
Tume ingeundwa kuchunguza hili maana sio kawaida kwa ukimya huu