Rais Samia: Wenye akili za kawaida ndiyo wananikosoa kusafiri nje

ndo ukope kila siku???
 
SGR pekee ni Trilion zaidi ya 12, sasa si utakamua watu hadi watoke damu.
lakini ulishaanza na umekamilika kwa asilimia kubwa sana kama sioa silimia 90... maana mpaka wanafanya testing. hata ndugai alikuwa anajua hali halisi ya miradi kuwa haiitaji kukopa kopa kila siku
 
Sasa unataka serikali ifanyaje na hizo rasilimali? Si watu binafsi ndio mnatakiwa kuwekeza kuvuna hizo rasilimali nchi ipate mapato? Ni watanzania wangapi wanaoweza kuwekeza kwenye uchimbaji madini wa kisasa? Ni wangapi wanaweza kujenga mahoteli ya kisasa kwa ajili ya watalii? Ni wangapi wanaweza kwenda kujenga mabwawa makubwa na kuendesha kilimo cha kisasa? Hakuna, sasa serikali haiwezi kufanya hayo ni wananchi wanafanya serikali ikakusanya kodi, fedha yetu pia inaimarika..ndivyo nchi zilizoendelea zimepitia njia hiyo

Sasa kama sisi ni choka mbaya serikali inabidi kutafuta wawekezaji na washirika wengine tu hakuna jinsi
 
hii nchi ni kubwa, bila misaada (bakuli) na kuita wawekezaji waje aisee hatutoboi huo ndiyo ukweli, tunatumia zaidi ya tunachozalisha.
Matumizi mengi ni ya ovyo kabisa, tunatafuta kimasikini na tunatumia kitajiri.
 
Wizi tu wa rasilimali.

Toka nchi inapata uhuru hakuna uwekezaji uliobadili maisha ya mtanzania.

Kwa bahati mbaya sana tunakosa usimamizi mzuri na kuruhusu watu wa nje wanufaike zaidi.

Na bahati mbaya tunaye Rais ambaye haamini katika kuwawezesha wananchi wake kumiliki na kunufaika na Rasilimali zao.

Bali katika kuwawezesha wageni waje wamiliki Rasilimali zetu na kuwatumikisha wananchi kwa ujira kiduchu.
 
SGR pekee ni Trilion zaidi ya 12, sasa si utakamua watu hadi watoke damu.
fedha za SGR zimekuwa zikikusanywa toka awamu ya kikwete.

Hiyo Railway Development Levy inayolipwa pale bandarini ndio kazi yake hiyo.

Hivyo sioni sababu ya mradi huu kuchelewa maana fedha zipo.

Unless ilifanyika realocation of funds jambo ambalo sisi maraia hatulifahamu.
 
Tangia uhuru hakuna uwekezaji uliobadili maisha ya watanzania? 🤣

Jamani tunawasiliana kwa intaneti na simu za mkononi sasa hivi, huu sio uwekezaji? Makampuni kama Vodacom, Tigo, Airtel si ya wawekezaji haya?
Kuna benk kubwa kama CRDB ambayo ilikuwa imekufa, leo hii ndio benki kubwa Tz baada ya wawekezaji kuichukua,
Tuna makampuni ya saraji, mabati, vyakula, vinywaji n.k vinavyolipa kodi kubwa serikalini na kutoa ajira, hizi sio faida za uwekezaji?
 
Mkuu private wamewekeza miaka mingi tu kwenye rasilimali. Na ni bora umetolea mfano kwenye madini. Hebu tueleze nchi tunapata kiasi gani kutoka kwenye madini?

Tatizo sio private kuja kuwekeza, tatizo ni viongozi tulionao na mikataba wanayoingia. Nchi za iarabuni wametajirika sababu ya mafuta tu kwa sababu walikua na viongozi makini. Huku kwetu miaka zaidi ya 50 sasa kwenye madini Hakuna tunachoambulia zaidi ya kuchimbiwa kisima Cha maji
 
Anakwepa ukweli huyu.
Sehemu zote zenye rasilimali zinaendeshwa na private, lakini hadi leo hakuna tulichoambulia
 
Kuna kodi na mirabaha serikali inachukua kutoka kwa makampuni ya madini, au unafikiri wanachimba bure?

Private sector ya Tanzania bado haina mitaji, ni dhaifu, hata ujenzi wa daraja au jengo tu la kawaida wanaletwa wachina sababu makampuni ya ndani hayana mitaji na wataalamu
 
Sijaelewa unataka kusema nini sasa. Au ndio unajibu kuwa wewe ni bunadamu.

Kwa maana chochote utakachofanya lazima watokee makundi ya wandamu wapinge.....?!?!?
 
Anakwepa ukweli huyu.
Sehemu zote zenye rasilimali zinaendeshwa na private, lakini hadi leo hakuna tulichoambulia
Kama wapi? Utalii hatupati kodi na fedha za kigeni? Madini hatupati kodi na mirabaha, kuwa wanachimba bure? Uvuvi hatupati mapato? Japo ni madogo sababu hakuna uwekezaji..
 
Hizo hela anapewa au anakopa?? Na tunarudisha nini anapokopa kwa kiwango hiko?? Tunashangilia tu tukija kustukaa mlima sio wetu mbuga sio zetu bandari sio yetu.

Ila kwa kuwa upeo wa kufikiri watz ni chini ya magoti wacha tuendelee kupiga shangwee ccm hoyeeee.
 
Sijaelewa unataka kusema nini sasa. Au ndio unajibu kuwa wewe ni bunadamu.

Kwa maana chochote utakachofanya lazima watokee makundi ya wandamu wapinge.....?!?!?
Huna Akili acha kutupotezea muda sawa?
 
Unashangaa nini wakati 98% ya wanaomuunga mkono ni 'Morons' tupu?
 
Vitu vimepanda Sana bei na bei haina thamani, enzi za magu pesa ilikuwa na thamani japo haikupatikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…