Weka takwimu hapa. Kwa miaka sita aliyokaa madarakani JPM alikopa trilioni ngapi; na kuliacha deni la taifa likiwa trilioni ngapi? Na mama kwa hii miaka michache tu aliyokaa madarakani amekopa trilioni ngapi; na kulipaisha deni la taifa mpaka trilioni ngapi? Ukizipata hizo takwimu utarudi ufute comment yako kama wewe ni mkweli na mwenye dhamira safi isiyotawaliwa na chuki binafsi.
Iko hivi: Kwa nchi zetu hizi huwezi kuziendesha bila kukopa maana uchumi wetu ni legelege sana. Suala ni kwamba unakopa ili ufanyie nini? Kama hukuona hizo trilioni chache alizokopa JPM zilitumika kufanyia nini basi tena....
➡️➡️➡️ Pamoja na kukopa kwake jambo kubwa ambalo alilifanya JPM ni zile jitihada zake za kujaribu kubadili fikra za watu polepole na kuona kuwa wana raslimali za kutosha kujiletea maendeleo kama wakizitumia vizuri. Wengi mnataka mabadiliko ya fikra - Kuwa na umma wenye falsafa ya ukombozi na kujitambua. Oooh miafrika mijinga haijitambui ndiyo maana bara tajiri sana lakini myenyewe ni masikini ya kutupwa. Mnafikiri kwamba kubadilisha fikra za watu, mitazamo na falsafa zao ni jambo rahisi kama kupiga kope kumbe ni kazi ngumu na yenye kuhitaji hata vizazi kadhaa. Na kweli Watanzania walikuwa wameanza kuona mwanga - wa kifikra na kimtazamo tu.
Angalau kwa hilo tu anastahili kupewa maua yake na wachache waliojaribu kumwelewa!
Pole kwa kukosa ajira za ualimu wakati wa JPM. Mama anaajiri walimu 14K mwaka huu. Nakuombea uwe mmoja utakayebahatika kupata kati ya waombaji 250K walioomba.
➡️➡️➡️
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni