Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Wizara ya Afya yetu bajeti ni donor funded kwa asilimia ngapi?

Tuanze kuumiza vichwa.
 


Rais wa Marekani Donald Trump leo amesaini executive order ya kuindoa US kwenye uanachama wa Shirika La Afya Duniani (WHO).

Trump aliwahi kutoa shutuma nyingi dhidi ya WHO wakati wa kipindi cha Covid na aliashiria kujitoa.

US inachangia karibia asilimia 18 ya bajeti ya WHO.

Soma zaidi hapa: Donald Trump signs order to withdraw US from World Health Organization
 
Chat GPT
 
Tayari pameshaanza kuchangamka..wale tuliozea dezo huu ndio mwisho
Hapo ni balaa tupu bado anaitaka greenland anasema kwa kuinunua hata kuivamia, bado anasema anaweza chukua ile canal kule america kusini ambayo anadai amerika iliwapatia bure wakati imechimbwa kwenye eneo lao wenyewe sasa huo ubure sijui unatoka wapi.
Ban ya tiktok kaisimamisha jana so tiktok imerejea US.
NATO nao hawaelewi elewi nini kinaweza tokea. Wasiyemtaka kaja.
Sema kilichonifurahisha, trump yeye hajali masuala ya inclusive kazini na meta imefuta rasmi sera zake za ujumuishi sijui wa gender diversity so mashoga na waliobadili jinsia watajibebea wenyewe
 
Sasa Tundu lissu akichukua nchi atakutana na wakati mgumu sana.

Naona pia ARV zitaanza kuuzwa sasa maana WHO wamepungukiwa mchango wa marekani.
ARV siku zote zinauzwa. Wanachokifanya Serikali ya Marekani kupitia PEPFAR, ni kununua haya madawa kutoka kwenye kampuni kubwa za Madawa halafu wanatugaia kama Msaada as part of their "soft policy" bure. Offcourse baadae lazima upanue.
Au mchango wa marekani wa hizo dola hauna athari?
Athari ni ndogo sana. Almost none. Msaada wa ARV's kutoka marekani ni Direct Funding na hazipitii WHO. Nimehakikishiwa PEPFAR itakuwepo, anagalabu kwa sasa.
Tutakufa kama kuku sasa
Kuku wanakufaje?🤣
 
Inabidi tujitambue, tuache matumizi mabovu kama;
-Goli la mama
-Ununuzi wa magari holela ya viongozi
-Ununuzi wa MABASI YA CCM☹️
-N.K

Kinyume na hivyo tujiandae kuzika/kuzkwa.
Wale wa kuzimu mtabakia kuzimu wale wanaoishi paradiso wataendelea kuishi paradiso
 
Wangemuambia tu China aongeze mchango Jamani 🤭
Kipindi cha COVID19 aliwahi kuonya kuwa ata freez US$400 China akajitutumua kuwa kama US ita freez hela yake basi WHO wasiwe na wasiwasi, wao China wata inject US$ 50😅, halafu WHO wakafurahi.

Viongozi wapigaji WHO hawaoni umuhimu wa mchango wa US sababu wanafanya water tight financial monitoring ya funds zao zisije zikatumika visivyo, every dollar itahtajika maelezo ya namna gani imetumika.

Kila activity lazima iwe justfied, na kila vendor atakayelipwa kwa hela yake ni lazima awe screeed vya kutsha na kufanyiwa background checks ili isije huyo vendor akawa anatafuta hizo pesa ili kuzipeleka kuendesha makundi ambayo ni maadui wa Marekani, au kukawa na conflict of interest na mengineyo.

Lakini hela ya China huwa hata haina ulinzi wa hivyo. Kwanza hutoa kwa ajili ya mambo yanayoihusu, pili hata anapochangia kwenye mambo mengine huwa haulizi mmetumiaje, wala hataki ushahidi wa matumizi. Anachozingatia China ni hata mkipeana mgao, basi maafisa wake wasiwe sehemu ya huo mpango wa kugawiana, maana atawanyonga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…