Ukiniuliza mimi kwenye vita kamili isiyo ya kujificha kati ya Rwanda na DRC nani anashinda nasema ni DRC endapo hakuna external influence baina ya pande zote mbili.
Congo ukitaka kuipima kwa kuangalia eneo lake la Mashariki utapotea, itazame nchi nzima hadi kule Magharibi. Mashariki ni kama imepotezewa na ina waasi wengi wanaojificha na kusumbua kila walijisikia. Wakipigwa wanavaa kiraia wanalima, wakipata support wanaanza mapigano. Ukija kwenye vita ya nchi na nchi hapo hujifichi, madaraja tunajua yalipo, kambi zilipo, airbase ilipo, HQ, defensive lines na mambo mengine.
Congo sio wazembe kuliko nchi nyingi za Kiafrika, tatizo lao wana rasilimali nyingi na bahati mbaya ya kunyonya na mataifa ya nje, ila nchi nyingi za Afrika hazina unafuu kijeshi kuwazidi. Hakuna nchi ina makundi ya waasi hadi 10 kama Congo ilivyo, logistics za kuipiga Congo kuanzia mpakani kwa Rwanda mpaka katikati ya nchi kule ni gharama kwa Rwanda. Rwanda kuipiga Congo sio rahisi hata kidogo