KERO Rais tuma timu ichunguze Hifadhi ya Wanyamapori Uyumbu (Tabora), Mwekezaji 'amewaweka mfukoni’ watendaji, Wananchi hawanufaiki

KERO Rais tuma timu ichunguze Hifadhi ya Wanyamapori Uyumbu (Tabora), Mwekezaji 'amewaweka mfukoni’ watendaji, Wananchi hawanufaiki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
WhatsApp Image 2026-07-16 at 16.36.04.jpeg
Ndani sintofahamu na mivutano ya kiutendaji imekuwa mingi katika Hifadhi ya Wanyamapori Uyumbu ambayo inasimamiwa na Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya Uyumbu (WMA) Wilayani Urambo, Tabora.

Kwa ufupi kuna matumizi mabaya ya madaraka na uingiliaji wa majukumu ya taasisi hiyo unaofanywa na viongozi wa serikalini ngazi ya wilaya na mkoa.

Chanzo kikubwa cha yote yanayoendelea ni malalamiko yetu Wananchi kuhusu mwekezaji anayeendesha Kampuni iliyopewa tenda hiyo na ambaye anakingiwa kifua na viongozi kadhaa wa kisiasa kwa sababu ambazo wanazijua wao.
WhatsApp Image 2026-07-16 at 16.36.04 (2).jpeg
Mwanzo wa Mgogoro na Kupinduliwa kwa Taratibu
Awali, usimamizi ulikuwa chini ya bodi ya wananchi ambao wengi wao hawakuwa na utaalamu wa kutosha, ndipo Wizara ya Maliasili na Utalii ilielekeza kuwepo kwa timu ya wataalamu ili kusaidia jumuiya.

Ulivyoanza mchakato wa kuanzisha mifumo ya kielektroniki na kudai stahiki za wananchi zilikwama kutokana na mwekezaji huyo kutofuata kanuni na kutochangia maendeleo ya jamii kama mkataba unavyoelekeza.

Mkataba wa kwanza wa mwekezaji wa Mwaka 2009–2019 ulitaka alipe Dola 5,000 (takribani Sh milioni 13) kila mwaka kwa ajili ya maendeleo ya jamii, lakini hajawahi kulipa, na kusababisha upotevu wa zaidi ya milioni 130.

Katika mkataba mpya wa Mwaka 2020–2035, taarifa zilizopo kutoka kwa watu wa karibu na viongozi wetu ni kuwa kuna michezo ilichezwa na kuingizwa kiasi cha milioni tano tu kwenye mkataba badala ya Sh milioni 13, kinyume na kanuni.

Uingiliaji wa Viongozi wa Kisiasa na Kufukuzwa Kazi
Kila mara watendaji au wataalamu wa Wizara ya Utalii wanapojaribu kufanya mapitio ya mkataba au kukagua ukiukwaji wa mwekezaji, viongozi wa wilaya, na ngazi ya mkoa wanaingilia kati kumlinda mwekezaji huyo.

Mfano wa matukio yenye utata ya hivi karibuni:
Oktoba 2025:
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliwasimamisha kazi watendaji bila sababu za msingi baada ya mwekezaji kulalamika wizarani. Tume ya uchunguzi ya ofisi hiyo ilibaini watendaji hawakuwa na kosa, wakarejeshwa kazini.

Kuzuia Mafunzo (Mwezi wa 5/6): Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilielekeza bodi mpya ya wananchi ipelekwe mafunzo katika Uhifadhi wa Jamii wa Makame (Manyara). DC alipiga simu kuzuia safari hiyo bila sababu za msingi, na watendaji walipoenda (kwa idhini ya Mkurugenzi wa Halmashauri), DC alivunja bodi yote tarehe 25 Mei.

Biashara ya Mkaa na Ujangili Ndani ya Hifadhi
Kuna uharibifu wa mazingira ndani ya hifadhi hiyo ya Uyumbu, mfano mwanzoni mwa mwezi huu Julai, 2026, Watendaji walikamata mtandao wa watu wanaovuna mkaa na kukata miti kiholela ndani ya hifadhi.

Watuhumiwa walifikishwa kituo cha polisi, lakini kuna watu wakaanza kuwaambia wale walioukamata mkaa huo kuwa "Mmekamata mkaa wa kigogo, hamtabaki salama."

Inavyoonekana watuhumiwa hao wataachiwa huru kwani watendaji walioanzisha kesi hiyo waliondolewa katika nafasi zao.
Screenshot 2026-07-16 173815.jpg
Screenshot 2026-07-16 173839.jpg
Dondoo kadhaa kuhusu mwekezaji
Kuna kiongozi wa Wilaya amekuwa akiishinikiza Jumuiya imlipe mwekezaji kiasi cha shilingi 12,000,000 (Milioni 12) kwa madai ya kufanya matengenezo ya Barabara za kitalu cha uwindishaji, ambapo kimsingi ni jukumu la Mwekezaji kutengeneza Barabara za kitalu chake.

Mwekezaji amekuwa akifanya uwindishaji wa Wanyama wengi tofauti na kibali chake cha kuwinda, hali ambayo pia imewahi kuthibitishwa na maafisa wa wizara, walipofanya thatmini ya utendaji kazi wa WMA, mwezi wa kumi na mbili 2024.

Kuna matukio ya uvunaji wa Magogo hifadhi, ambapo mara kwa mara yamekuwa, yakihusisha kuwa ni mizigo ya Kigogo ambaye niliandika hapo juu mikaa yake imekamatwa.
 
Back
Top Bottom