DOKEZO Rais tuokoe Wananchi wako wa Dodoma Jiji juu ya dhuluma hii ya Mkurugenzi Jiji. Mkuu wa wilaya kashindwa

DOKEZO Rais tuokoe Wananchi wako wa Dodoma Jiji juu ya dhuluma hii ya Mkurugenzi Jiji. Mkuu wa wilaya kashindwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kichwa cha habari cha jitosheleza.

Wananchi wa Makole D center halmashaur ya jiji walihamishwa kupisha mradi wa stendi ndogo na kituo cha biashara ndogo ndogo za ujasiliamali.

Mwanzo walitakiwa kufidiwa kwa malipo ya hela ila halmashauri wakasema fungu lililotengwa lilichukuliwa tena na serikali iliyopita hivyo hawakuwa na fedha ya kulipa fidia. Hivyo wakasema watawapa viwanja sehemu yenye gharama ili wao ndio waviuze kwa thamani kubwa. Eneo hilo plot no

157 Medeli East-Dodoma​

Ila cha kushangaza viwanja walivyopewa na gharama zote za hati wameshalipia kumbe ni mali ya  MSD na vimeshalipiwa mpaka 2025..kwa wale wasiopajua eneo ni lile lenye ukumbi wa JK, B.O.T, HAZINA.
CCM, Chama Cha Madhulumati. Mmesha dhulumiwa
 
Katika mambo yanayoshangaza ni hili la wananchi kukabidhi ardhi waliyopewa na mungu kwa mamlaka walizozipa mamlaka wenyewe kisha kulia lia ..... Hivi kati ya mamlaka za Serikali na binadamu kwa maana ya wananchi walioikalia hiyo ardhi hata kabla ya uhuru ni nani mwenye haki ya kumhamisha mwingine?
Nadhani Katiba mpya itakapoandikwa hili suala la ardhi liangaliwe upya. Wananchi ndio wenye mamlaka ya kuiagawia Serikali ardhi ili ipange miji....sio kinyume chake!. 😲
 
Angalau mwanga unaanza kuonekana kwa mbaaali hongera jerry slaa..
 
Toka wasainishwe check huu unaenda mwez wa pili kimya...zaidi ya miaka kibao manyanyaso yanaendelea...hii nchi ngumu sana...
 
Back
Top Bottom