Rais tupia Jicho malalamiko ya askari wako hayana afya kwa Nchi

Rais tupia Jicho malalamiko ya askari wako hayana afya kwa Nchi

Niliandika asubuhi japo ujumbe haukuwa moja kwa moja kwako,,lakini uzalendo wangu umenituma kurudia tena kuandika,,,Mimi ni mwananchi ambae shughuli zangu hunifungamanisha sana na askari wa majeshi mbali mbali nafikiri toka kipindi cha Magufuli.

Binafsi sipendezwi na maneno ambayo yana malalamiko kuona yanatoka kwa askari ambae tunamtegemea akulinde wewe binafsi mh.rais ambae ni kiongozi wetu mkuu.

Askari hasa walioko wizara ya Mambo ya Ndani hasa polisi na Magereza nimewasikia mara nyingi wakilalamika kunyimwa posho zao za Maji na Umeme nadhani wewe Rais utakuwa unazielewa vema kuliko mimi,,,,wanadai labda kuna watu Wizara wanazuia posho hizo kwani wamezidai ziingizwe katika mishahara yao muda mrefu sana,,,,wanaenda mbali wanadai wewe utakuwa unalielewa vema swala hilo ila kwa sababu pengine hutambui mxhango wao ndo maana unakaa kimya.

Mh. Rais nchi yetu si maskini kiasi hicho kushindwa kuwahudumia askari wako!!!

Wakati mwingine nakutana na askari wa Jwtz nao wana malalamiko kwamba posho yao ya chakula haiboreshwi hivyo kuwapa ugumu kuendana na hali ya maisha ya sasa,,,wanasema mkuu wao amekuwa mtu wa kuwadhibiti badala ya kushughulikia maslahi yao.

Askari wanadai waliongezwa posho yao kipindi cha uchaguzi 2015 ambapo Lowasa alitingisha Nchi hivyo serikali ya ccm ikatoa kama rushwa ili kukilinda chama.

Mh.,mimi kama raia ambae nakutakia mafanikio nisingependa uyaache malalamiko ya askari yanaelea angani maana kinachoweza kutokea unakijua mama angu.

Kumbuka askari si mwalimu au nesi kusema akigoma utamuacha mpaka atakapo jisikia arudi kazini,,nadhani unawajua hawa wadudu walivyo wakorofi mama .

Lakini bado nafikiri askari wetu nao wamesahau kiapo chao cha Uvumilivu maana wameapa hivyo!!! Wengine wanasema hawajaongezwa mshahara toka 2015 mimi nilidhani ni kwa kada nyingine kumbe nao wamo!!!?

Mh.,Nakutakia kila la kheri katika utawala wako ,,,Usiruhusu askari wako wakuchukie,,,ni bora uchukiwe na makada wa chama ila siyo akari wako Mh. Rais hilo ni kundi la kwanza kujipendekeza kwalo.
Ushirika na Shetani haudumu
Pelekeni haya Malalamiko Lumumba CCM
 
Hivi polis wana lipi la ziada? Mbona walimu, mahakimu manesi na wafanyakazi wa kada mbalimbali hawana hizo posho? Au mnawapa posho wawaweke madarakani.yaani mnakujahapa kulalamikia hongo
 
Hivi polis wana lipi la ziada? Mbona walimu, mahakimu manesi na wafanyakazi wa kada mbalimbali hawana hizo posho? Au mnawapa posho wawaweke madarakani.yaani mnakujahapa kulalamikia hongo
Anzisha mada mpya kuwatetea uliowataja!! Kuwa na adabu acha kuyafaninisha majeshi na mambo mengine ni kada zisizofungamana kabisa
 
Hivi polis wana lipi la ziada? Mbona walimu, mahakimu manesi na wafanyakazi wa kada mbalimbali hawana hizo posho? Au mnawapa posho wawaweke madarakani.yaani mnakujahapa kulalamikia hongo
Unalala ndani wenzako wanakesha nje ndio wanakufanya utambe na keyboard Leo
 
Anzisha mada mpya kuwatetea uliowataja!! Kuwa na adabu acha kuyafaninisha majeshi na mambo mengine ni kada zisizofungamana kabisa
Polisi na nesi nani anatakiwa kupewa posho jamani? Hapa nawe unatakiwa uwe na adabu. Kila siku hawa watu wanalalamikiwa kubambika kesi rushwa na hata mauwaji, leo wanalalamia posho kweli uchwala kweli?
 
Polisi na nesi nani anatakiwa kupewa posho jamani? Hapa nawe unatakiwa uwe na adabu. Kila siku hawa watu wanalalamikiwa kubambika kesi rushwa na hata mauwaji, leo w
Wanajeshi sina wasiwasi nao. Issue iko kwa Polisi. Kumbuka hata manesi wanakesha kusafisha vidonda, kuwatawaza wagonjwa nk.
Nurse akigoma utajitibu na mitishamba vipi askari akigoma inakuwaje!?
 
Polisi na nesi nani anatakiwa kupewa posho jamani? Hapa nawe unatakiwa uwe na adabu. Kila siku hawa watu wanalalamikiwa kubambika kesi rushwa na hata mauwaji, leo wanalalamia posho kweli uchwala kweli?
Rushanju toine magezi!! Ujinga wa polisi wachache usikufanye ulichukie jeshi la polisi zima,,,Unesi na Upolisi ni kada mbili zisizofungamana kabisa na unyeti wao unatofautiana pia
 
Rushanju toine magezi!! Ujinga wa polisi wachache usikufanye ulichukie jeshi la polisi zima,,,Unesi na Upolisi ni kada mbili zisizofungamana kabisa na unyeti wao unatofautiana pia
Walalamike pale watakapo kosa mshahara. Hizo posho zinaleta ukakasi kwa wafanyakazi wa kada tofauti. Kila.mfanyakazi ana umuhimu wake kazini kwake. Unaona tuendelee kuwaongeza posho kwa kuwa wana AK47?
 
Pigania haki unazozikosa kisheria kama ambavyo askari wanapigania haki zao ambazo wanastahiki kisheria,,,,kama hazipo haki hizo utadai zanini na kwa sheria ipi!???
 
Watumishi wa umma wamekaa miaka 6 bila kuwajali.Ccm ya leo ni zimwi.
 
Nyie police na waalimu sio watu kuonewa huruma hata kidogo nashauri serikali ishushe hata mishahara yenu
JamiiForums-289452902.jpg
 
Vyovyot utakavyofikiria juzi kati niliandika kuhusu Walimu napo natakuwa mwl siyo!!?
Huyo aloandika siyo askari,amejivika uaskari tu kuchochea jambo.
Fanya utafiti huu.
Kabla ya 2015 haya malalamiko yalikuwa hai na kweli.
Baada yahapo waliheshimiwa sana kwa nyongeza kibao.
 
Polisi na nesi nani anatakiwa kupewa posho jamani? Hapa nawe unatakiwa uwe na adabu. Kila siku hawa watu wanalalamikiwa kubambika kesi rushwa na hata mauwaji, leo wanalalamia posho kweli uchwala kweli?
Magaidi yakitinga na LMG hospitali nesi atafanya kazi?
 
Hivi polis wana lipi la ziada? Mbona walimu, mahakimu manesi na wafanyakazi wa kada mbalimbali hawana hizo posho? Au mnawapa posho wawaweke madarakani.yaani mnakujahapa kulalamikia hongo
Hao uliowataja wote wenye hizo profeshino wanapatikana majeshini.
Lakini kwao huwapati askari.
 
Back
Top Bottom