Rais Uhuru Kenyatta: Nchi jirani zinahitaji siasa ambazo ushindani si uadui na vita

Tukubari tumetia aibu. Hakukuwa na uchaguzi
 
Asante saaaaaaana
 
Ushoga umetapakaa Afrika mashariki tangu zamani. Huyu bwana ana lake na TZ kuna kundi la wabunge majeruhi kutoka chama fulani wanataka ukimbizi awachukue wanadai wanapigiwa simu za vitisho pengine ni watoto ndio wanaopiga simu
 
Kenya kiukweli wako mbali sana ktk demokrasia na kiuchumi. It is an engine of east africa economy. Uhuru Kenyata hakumungunya maneno amemrushia dogo jiwe kuwa upinzani sio uadui wala vita. Sas hivi nchi imegawanyika. Alitukuta wamoja chini ya JK leo anataka atuwache tumepalanyika kwa siasa za visasi. Eti niombee. Tangu lini shetani akaombewa na Malaika!!
 
Kenyatta kaonesha jinsi alivyo mwepesi kujirudi na kuzungumza na mahasimu wake kisiasa kwa maslahi mapana ya nchi na wananchi wake, hapa kwetu hilo halifanyiki, ni kiburi tu cha ushamba wa madaraka.
 
huu utopora man kamwambia kua bongo kuna vita🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Kusema kweli tukianza kuchambua mapungufu ya siasa za Kenya wengi hapa mtaishia kushangaa tu. Pamoja na mapungufu ya siasa za Tanzania, bado huwezi kulinganisha na ya Kenya.

Ni watoto wadogo tu ndio hawajui ubabe, unyanyasaji na mauaji yaliyofanyika na yanayofanyika kwa wanasiasa wa Kenya kwa miongo mingi sasa. Nani hajui kilichowakuta Thom Mboya, Robert Auko, Mutula Kilonzo, Pro. George Saitoti na wengine wengi? Au mmesahau kilichomtokea mkuu wa kitengo cha IT cha Tume ya Uchaguzi ya Kenya miaka michache tu iliyopita? Mnataka tuweke hapa orodha ya Wakenya walioko uhamisoni kwa sababu za kisiasa? Kuna mtoto hapa hajui yaliyotokea Kenya baada ya uchaguzi Mkuu mwaka 2017?

Kusema kweli kuilinganisha Kenya na Tanzania kisiasa ni sawa na kulinganisha usiku na mchana. Kwa Afrika Mashariki bado hakuna nchi inaifikia Tanzania kwa siasa za kistaarabu na zinazoheshimu haji za binadamu. Hiyo sio kusema sisi hatuna changamoto. Zipo lakini ni chache na za kawaida kulinganisha na wengine.
 
Kwani hao watoto wa viongozi wetu wanaosoma kwenye shule za kimataifa na kutembea na maVX ya umma, ww na familia yako pia huwa mnapanda hizo VX?
Kwahiyo unataka wote muwe viongozi ili muwe na mavx?
 
Kenyatta kaonesha jinsi alivyo mwepesi kujirudi na kuzungumza na mahasimu wake kisiasa kwa maslahi mapana ya nchi na wananchi wake, hapa kwetu hilo halifanyiki, ni kiburi tu cha ushamba wa madaraka.
Hujui chochote kule Kenya bora ukae kimya uendelee kumfuatilia tu Amsterdam
 
Lakini kenyata hakutengeneza kura feki na kuonekana wazi wazi?.
Au na yeye alipiga wapinzani wake risasi na kuwapoteza?
Ndio maana tunawaita watoto wadogo!

Ungefuatilia siasa za Kenya hata kwa wiki tu ungemshangaa sana Kenyata anapata wapi kibali cha kuwasema nchi za wenzie
 
Ndio ujinga mmekuwa mkilishwa miaka yote. Nenda Kenya kaone hayo matunda ya uchumi na democrasia.
Wakenya wenyewe wakiona hiki ukichoandika hapa watakushangaa sana
 
Uhuru Kenyatta naye kageuka mwalimu wa siasa za vyama vingi eti siasa za vyama vingi sio uadui ICC alipelekwa kwa sababu gani? Vita zile walitwangana na kuuuana kule Kenya Baada ya uchaguzi na akina Raila Odinga zilikuwa za Nini adi Kikwete akaitwa kwenda kuwasuluhisha

Ama kweli nyani haoni kundule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…