KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Mkuu Philemon Mikael, kwa hiyo tumlinganishe Mwalimu Nyerere na Mzee Kenyatta kwa mabaya yaliyofanyika kwenye enzi zao?Those are the matters of the past ambayo hata sisi tunazo past zetu zilizotokea awamu ya kwanza ambazo hata rais nyerere alikiri alikosea ...mfano Operesheni Vijiji watu wengi walikufa kwa kuliwa na wanyama , kulala nje na njaa kutokana na kuhamishwa kwa nguvu kutoka kwenye maeneo yao ya asili na kuhamishiwa kwenye vijiji vya ujamaa ..... hata sasa ukiongelea mauwaji na utekaji ndio yameshamiri ...
Kuna kumbukumbu zozote ulizonazo kuhusu Mwalimu kuhimiza yeye moja kwa moja kuwadhuru raia zake, kama huko kuwapeleka maporini kuliwa na simba; au hayo ni matokeo mabaya ya watendaji kuhusu utekelezaji wa yaliyokuwa yameamriwa na vikao?
Unaweza kweli ukalinganisha unyama wa Kenyatta aliokuwa akiwafanyia waliokuwa wakipinga mambo yake kama akina JM Kariuki na ubinaadam aliokuwa nao Mwalimu?
Sijasema hapa kwamba hapakufanyika makosa chini ya utawala wa Mwalimu, lakini kuwalinganisha Kenyatta na Mwalimu ni kupotosha maksudi kabisa.
Huyu Kenyatta wa sasa, hata yeye sio msafi kivile. Anajaribu sana sasa hivi kujisafisha, lakini mabaya aliyofanya katika ngwe yake ya kwanza na katika chaguzi zake zote mbili na hata kabla ya hapo, makosa yaliyompeleka ICC yote hayo hayaonyeshi usafi wowote.
Kenya wameua watu wengi, maelfu kwa kila chaguzi wanazofanya. Hawana chochote cha kujivunia zidi ya nchi nyingine.
Naomba nisieleweke kuwa nawatetea hawa waliopo madarakani sasa wanaotupeleka kwenye mambo ya kusikitisha sana ndani ya taifa letu.