Rais Uhuru Kenyatta: Wakenya hawapaswi kujilinganisha na mataifa yanayoficha taarifa za COVID-19

Rais Uhuru Kenyatta: Wakenya hawapaswi kujilinganisha na mataifa yanayoficha taarifa za COVID-19

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
Rais Uhuru Kenyatta amesema Wakenya hawatakiwi kujilinganisha na mataifa yasiyo uhuru wa habari na ambayo yamekuwa hayatangazi taarifa za CoronaVirus

Amesema wananchi wanatakiwa kufurahia kuwa Serikali haifichi kitu chochote na imekuwa ikiwaambia wananchi ukweli kuhusu hali ya mlipuko huo

Kauli yake inakuja kufuatia baadhi ya Wakenya mitandaoni kusema nchi hiyo inapaswa kulegeza masharti ya kudhibiti maambukizi kama Tanzania

Ameeleza kuwa, Kenya ni nchi ya kidemokrasia na vyombo vya habari vipo huru hivyo haiwezi kuficha taarifa. Nchi hiyo imerekodi visa 17,975 na vifo 285 huku wagonjwa 7,833 wakipona hadi sasa

===

- President Uhuru said Kenyans should be proud that the government was not sweeping anything under the carpet but was telling its citizens the truth about the pandemic

- Uhuru said Kenyans should not compare themselves to countries which had limited media freedom and had kept COVID-19 information under wraps

- This came after some Kenyans opined on social media that Uhuru should ease measures like Tanzania

- The John Magufuli-led nation last updated its COVID-19 statistics on April 29 and journalists have faced harassments and arrests for reporting on coronavirus

President Uhuru Kenyatta has asked Kenyans not to compare themselves with countries which are keeping COVID-19 information under wraps.

Uhuru said Kenya was a democratic country and media freedom was paramount and thus could not hide any pertinent information about the pandemic which has infected 17,975 patients in the country as of Monday, July 27.

Source: Uhuru says Kenya cannot hide COVID-19 information like other countries
 
Safi sana rais, endelea kutupea takwimu zote hamna haja kuogopa au kujichokea, isemwe kama ilivyo, mwanzo mwanzoni tulikua na uwoga ila kwa sasa watu wamekua na ujasiri wa kupambana maana hamna kinachofichwa, tunaambiwa kama ilivyo bila kumumunya.

Hili suala la Corona hunikumbusha ilivyokua mara yangu ya kwanza kupima UKIMWI, yaani kabla kupata ujasiri wa kwenda kupima nilihangaika sana kwa uwoga, siku nyingi niliishi kwa kujiaminisha sina UKIMWI, ni gonjwa la mabeberu na haliniathiri, lipo kwa ajili ya wengine, mimi mzima, mimi kidume, nikawa najiaminisha pumba ila kila nikikohoa kidogo tu baasi naamini ndio hapo limenikuta, ila hatimaye nilipiga moyo konde na kupima na tangu kipindi hicho baada ya kupima sijawahi kusita kupima tena na tena, ukweli uliniweka huru John 8:32

Bila kuujua ukweli, mtateseka sana kimawazo maana kila kifo cha mtu yeyote mnajikuta mkishuku na kueneza uvumi na tetesi kwmba kafa kwa Corona.

YOU CAN'T HANDLE THE TRUTH

 
Inaonekana ameshindwa kupambana na Corona nchini kwake badala yake anataka kujilinganisha na nchi zingine, Hakuna nchi inayopambana kwa kujilinganisha na nchi zingine, kila nchi inatumia njia yake inayoona inafaa ili kuwakinga watu wake.

Kwanza tujiulize, kwanini wakenya wanajilinganisha na nchi zingine ambazo kwao wanahisi wamafanya vizuri? Jibu ni Leanna, huwezi kuwazuia watoto wako wasiende kucheza na watoto wa majirani, wakiona vitu vizuri kwa majirani lazima watakuambia na kuomba uwanunulie hivyo vitu, kama unao uwezo utawanunulia ili wasijisikie unyonge, ila Kama huna uwezo utajaribu kuwapa matumaini ya maneno matupu ili wajione nao ni bora kuliko hao majirani wao.

Ukweli ni kwamba Uhuru Kenyatta amepoteza ushawishi kwa wakenya walio wengi, Magufuli amepandisha sana kiwango cha kipimo cha uongozi wa marais hapa Africa, wananchi wengi wanaona marais wao hawafanyi lolote ukilinganisha na Magufuli, njia pekee iliyobaki kwa Uhuru Kenyatta ni kutumia maneno na hoja dhahifu kuwapa moyo wakenya wasijisikie unyonge.

Dunia inaona na wakenya pia wanaona, ikifikia hadi wakenya wanajilinganisha na Tanzania na kumtaka Uhuru Kenyatta kuiga Tanzania, ni kwasababu wamefanya utafiti wa kutosha na kujiridhisha kwamba Tanzania inafanya vizuri, sidhani kama wakenya hawana akili kiasi cha kuvutiwa na jambo ambalo ni baya, kwamba wakenya wote hawana akili ila yeye Uhuru pekee ndio mwenye akili, hiyo ni dalili ya kutapatapa bila kuwa na mipango madhubuti ya kudhibiti Corona.
 
Inaonekana ameshindwa kupambana na Corona nchini kwake badala yake anataka kujilinganisha na nchi zingine, Hakuna nchi inayopambana kwa kujilinganisha na nchi zingine, kila nchi inatumia njia yake inayoona inafaa ili kuwakinga watu wake.
Nimeshangaa sana mkuu,bado naendelea kushangaa hapa.

Kumbe huyu jamaa inawezekana ni kweli anachoma mmea[emoji848][emoji848]
 
Safi sana rais, endelea kutupea takwimu zote hamna haja kuogopa au kujichokea, isemwe kama ilivyo, mwanzo mwanzoni tulikua na uwoga ila kwa sasa watu wamekua na ujasiri wa kupambana maana hamna kinachofichwa, tunaambiwa kama ilivyo bila kumumunya.
Na mnatakiwa mpimwe mpaka mtie akili, mkija kuelewa nini kinaendelea mmeachwa uchi.
 
Na mnatakiwa mpimwe mpaka mtie akili,mkija kuelewa nini kinaendelea mmeachwa uchi.

Najaribu kuwaza hapa, serikali yetu ingefanya mnachokifanya huko yaani hakungekalika, Wakenya huwa tuna muamko tofauti sana, ila naona Wabongo wameanza kuamka amka, kwa namna walivyojitokeza kumlaki Tundu Lissu licha ya mikwara mliyokua mumewatolea inadhihirisha kiaina wana kamuamko fulani.
 
Nimeshangaa sana mkuu,bado naendelea kushangaa hapa.

Kumbe huyu jamaa inawezekana ni kweli anachoma mmea[emoji848][emoji848]
Uhuru amekwama katika uongozi wake, hili janga la Corona ndio limethibitisha udhahifu wake zaidi, wakenya wanachohitaji ni ufumbuzi wa tatizo la maambukizi, mbona Ugandan na Rwanda wanefanikiwa na wanapima na kutangaza kama wanavyifanya Kenya, iweje Kanya maambukizi yanaingezeka kwa kasi lakini Uganda hayaongezeki?

Uhuru na Wakenya kwa ujumla walipaswa kujiuliza na kujilinganisha na Uganda na Rwanda ambazo nazo pia zinapima na kutangaza matokeo, kama kutangaza na kupima ndio sababu ya kusababisha idadi ya maambukizi kuwa kubwa, kwanini Uganda idadi ni ndogo?.

Uhuru Kenyatta is the most useless president in this region, yeye anapaswa kutoa majibu Kwanini maambukizi yanaongezeka kwa kasi nchini kwake, wananchi kuanza kujilinganisha na nchi zingine ni baada ya kuona mambo nchini mwao sio mazuri, anapaswa kuyafanya yawe mazuri badala ya kuwakataza wananchi kujilinganisha na huko wanakohisi mambo ni mazuri.

Binadamu wanajua kipi ni kizuri na kipi ni kibawa, kamwe hawatoacha kuvutiwa na jambo Zuri. Ukisoma comments za wakenya chini ya video za Hotuba ya Uhuru katika YouTube, bado wakenya wengi wanaamini kwamba Magufuli yupo sahihi na kumuomba Uhuru aige mbinu za Magufuli.
 
Najaribu kuwaza hapa, serikali yetu ingefanya mnachokifanya huko yaani hakungekalika, Wakenya huwa tuna muamko tofauti sana, ila naona Wabongo wameanza kuamka amka, kwa namna walivyojitokeza kumlaki Tundu Lissu licha ya mikwara mliyokua mumewatolea inadhihirisha kiaina wana kamuamko fulani.
Kwani mnasemaje kuhusu hali ngumu ya maisha na ufisadi wa serikali yenu,ay hapo mnakosa nguvu[emoji16][emoji16].

Watanzania hawajawahi kukosa mwamko, ila hawana mihemko ya kipumbavu. Hiyo ndio tofauti yenu na sisi. Mnahemuka kwenye mambo ya kipuuzi mnaacha ya msingi.
 
Kwani mnasemaje kuhusu hali ngumu ya maisha na ufisadi wa serikali yenu,ay hapo mnakosa nguvu[emoji16][emoji16].

Watanzania hawajawahi kukosa mwamko,ila hawana mihemko ya kipumbavu.hiyo ndio tofauti yenu na sisi.mnahemuka kwenye mambo ya kipuuzi mnaacha ya msingi.

Kwa hiyo video ya jana wameanza kuamka, walikua wanafahamika kwa uwoga sana yaani "keyboard warriors", nimeshangaa sana kuona wamejitokeza kihivyo licha ya mikwara, halafu nimesoma sehemu kwamba huyo huyo Tundu Lissu atahudhuria sherehe ya kutoa heshima kwa jeneza la Mkapa na maelfu ya Watanzania wako tayari kumiminika huko, aisei hayo matukio yenu yananikumbusha mbali sana wakati Wakenya walikua wanaanza kuamka, zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Naona wana Lumumba mtakua na kazi ngumu sana, sijui hata kwanini mpo huku kwenye jukwaa la Wakenya, mngeenda kupambana kwenye majukwaa yenu ya siasa mjaribu kupooza moto wa Lissu.
 
Kenyatta anapaswa kudili na corona kwa njia anazojua yeye mwenyewe. Aache kulalamika. Wananchi wake wanamacho, wanaakili, wanaona na wanasikia kila kitu kilichopo Tanzania. Huku tz hakuna corona hata chembe, huo ndio ukweli na wakenya msijaribu kutuletea corona yenu hapa.
 
Hongera sana mzee kenyatta, mficha maradhi kifoo humuuumbuaa,😂 waswahili wanaendelea kuzika wabunge, mawaziri hata na maraisi wastaaafu!! huku wakijidanganyaaa no koronaaaaa!😂

Endelea pia kuwabana kabisa kuleee mipakanii na nyanya zaooo hukoo!!
 
hongera sana mzee kenyatta, mficha maradhi kifoo humuuumbuaa,[emoji23] waswahili wanaendelea kuzika wabunge , mawaziri hata na maraisi wastaaafu! huku wakijidanganyaaa no koronaaaaa![emoji23]
endelea pia kuwabana kabisa kuleee mipakanii na nyanya zaooo hukoo!!
Yeye Uhuru Kenyatta asiyeficha maradhi anafanya nini kudhibiti kuenea na vifo vya Corona? Anapaswa kuwaambia wananchi wake mbinu muafaka atakazo tumia ili kuwaponya wakenya, au yeye kwake muhimu ni kujilingabisha na Tanzania, Kama watanzania wanakufa basi kwake iwe ndio sababu ya kuridhika kwamba hata wakenya wakiendelea kufa wasiwe na hofu kwasababu hata watanzania pia wanakufa? [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kiukweli hayo mapambano ya covid huko kenya ni MAIGIZO yaan mchana mambo kama kawaida eti ila lockdown ni jion tu 😆😆😆😆 alafu barakoa zenyee ss utazani jani la migomba ...izo barako mnazo vaa isitoshe rais UK mwenyewe anapiga misere ktk mikusanyiko ya watu hana barakoa 😆😆😆😆😆😆😆😆😆
 
Nyie mumetengenezwa kwa mwili wa chuma ndio maana hamuwezi kupata corona. Munaweza kupata kutu tu.
 
Hongera sana mzee kenyatta, mficha maradhi kifoo humuuumbuaa,😂 waswahili wanaendelea kuzika wabunge , mawaziri hata na maraisi wastaaafu! Huku wakijidanganyaaa no koronaaaaa!!!😂 Endelea pia kuwabana kabisa kuleee mipakanii na nyanya zaooo hukoo!

Hatari sana kwa kweli.
 
Nyie mumetengenezwa kwa mwili wa chuma ndio maana hamuwezi kupata corona. Munaweza kupata kutu tu.
Mbona sisi tulikua tunamsema sana Kikwete kutokana na uongozi wake fhahifu?, kwanini msikubali kwamba Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa marais dhahifu sana katika historia ya Kenya?. Kumsifia ili kutuonyesha kwamba Kanya mambo ni shwari sio suluhisho ya matatizo yenu, Corona itaendelea kuwapukutisha kama wadudu.
 
Kwa hiyo video ya jana wameanza kuamka, walikua wanafahamika kwa uwoga sana yaani "keyboard warriors", nimeshangaa sana kuona wamejitokeza kihivyo licha ya mikwara, halafu nimesoma sehemu kwamba huyo huyo Tundu Lissu atahudhuria sherehe ya kutoa heshima kwa jeneza la Mkapa na maelfu ya Watanzania wako tayari kumiminika huko, aisei hayo matukio yenu yananikumbusha mbali sana wakati Wakenya walikua wanaanza kuamka, zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Naona wana Lumumba mtakua na kazi ngumu sana, sijui hata kwanini mpo huku kwenye jukwaa la Wakenya, mngeenda kupambana kwenye majukwaa yenu ya siasa mjaribu kupooza moto wa Lissu.

My brother, haya mapokezi ya Lisu unaweza kuyalinganisha na mafuriko ya 2015? Kama ni kuamka waTZ waliamka kipindi kile sio leo, na mikwara haijaanza leo ilikuwepo siku nyingi tu. In short yalikuwa ya kawaida sana, yani hata foleni hayakuleta, enzi zile za Lowasa haikuwa hivi.

Kama mchangiaji mmoja alivyosema, wTZ hatukurupuki tu na kuanza kuandamana, tuna ustaarabu wetu na tuna njia zetu za kufikia tunalotaka, mfano mrahisi tu, wajumbe wa CCM ambao wamepiga kura za kuchagua wagombea ubunge na udiwani wanawakilisha waTZ wengi sana, na umeona mwenyewe walichofanya, haikuhitajika maandamano bali ilikuwa ni sanduku la kura limeamua.

Sitataka kuongelea kuhusu kufeli kwa Demokrasia ya Kenya, bali kwa leo naona niseme tu, kwenye hili suala la Korona, majirani sijui hata kama mnajua mnachofanya, kinachouma zaidi kuna mikopo inabidi mlipe.. lakini haidhuru, nyie ni mido inkamu kantri so mnaweza kukopa zaidi.
 
Kasema kweli. Tanzania sio kwamba hakuna Coronavirus,bali hakuna taarifa zinazohusu Coronavirus. Hawapimi wala hawatoi taarifa. Ignorance is bliss.

Sometimes not knowing all the facts about Coronavirus is better. Maana Panic inaua kuliko Coronavirus yenyewe.
 
Back
Top Bottom