MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 8,974
- 12,662
Kwenye hili la Corona, Magufuli ndio ameplay smart. Wote matakuja kwenye same conclusion. We have to live with Corona, hizi partial, semi and full lockdowns will not help.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyie wenye hamuwezi kupata corona endeleeni kujivinjari.Mbona sisi tulikua tunamsema sana Kikwete kutokana na uongozi wake hahifu? Kwanini msikubali kwamba Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa marais dhahifu sana katika historia ya Kenya? Kumsifia ili kutuonyesha kwamba Kanya mambo ni shwari sio suluhisho ya matatizo yenu, Corona itaendelea kuwapukutisha kama wadudu.
We jamaa hata mara moja uwe unakubali kushindwa ndo uungwana sio kila kitu unashupaa, hauonekani mjanja.Najaribu kuwaza hapa, serikali yetu ingefanya mnachokifanya huko yaani hakungekalika, Wakenya huwa tuna muamko tofauti sana, ila naona Wabongo wameanza kuamka amka, kwa namna walivyojitokeza kumlaki Tundu Lissu licha ya mikwara mliyokua mumewatolea inadhihirisha kiaina wana kamuamko fulani.
Endeleeni kuficha kichwa kwenye mchanga kama mbuni. Wote wanaokufa kuna ripoti ya daktari inayoelezea chanzo cha kifo kwa wahusika so endeleeni kuamini mnachoamini kwetu haina athari.hongera sana mzee kenyatta, mficha maradhi kifoo humuuumbuaa,😂 waswahili wanaendelea kuzika wabunge , mawaziri hata na maraisi wastaaafu!! huku wakijidanganyaaa no koronaaaaa!!!😂 Endelea pia kuwabana kabisa kuleee mipakanii na nyanya zaooo hukoo!!
Uliona wamevaa mibarakoa?Najaribu kuwaza hapa, serikali yetu ingefanya mnachokifanya huko yaani hakungekalika, Wakenya huwa tuna muamko tofauti sana, ila naona Wabongo wameanza kuamka amka, kwa namna walivyojitokeza kumlaki Tundu Lissu licha ya mikwara mliyokua mumewatolea inadhihirisha kiaina wana kamuamko fulani.
Lazima aendelee kupima pima tu. Kwa maana mabeberu mwishoni watahitaji retirements ya hizo fedha. Uhuru anapaswa kujua ya kuwa:-
1. Elimu ya namna ya kujikinga na tiba ndiyo jambo kuu. Wawafundishe wananchi jinsi ya kujikinga na lililo la muhimu zaidi ni jinsi ya kufanya kinga yako iimarike. Tanzania walijitahidi kufanya mambo yanayoimarisha kinga na kubadirisha mitindo ya maisha ambayo ni hatarishi. Ndiyo maana wagonjwa ni wachache sana katika mahospitali (considering cases vs serious cases).
2. Kuondoa hofu kwa wananchi ni jambo la msingi katika vita dhidi ya korona.
3. Kupima kwa mtu ambaye hana dalili hata moja ya ugonjwa au kumkamata na kumpima mtu anayetembea zake barabarani kuelekea kwenye shughuli hakuta punguza korona, wala si njia ya kupambana na ugonjwa bali ni kupotea rasilimali tu.
4. Kama unataka kupima kweli hali ya korona kwa watu, ni kupima ni weekly or semi-month basis. Hiyo ni kwa maana hali (status) ya ugonjwa kwa mtu hubadirika daima. Ukinipima leo sina maambuki, lakini baada ya majuma mawili ukinipima utanikuta na maambukizi. Au leo umenipima nina maambukizi, lakini baada ya juma moja au mawili utanikuta SINA MAAMBUKIZI. Hivyo status yake hubadirika daima. Tofauti na ukimwi ukipimwa unao, basi baada ya miezi mitatu wakikupima tena watakuta unao.
Kwa sisi ambao tumetumia muda mwingi kuusoma na kuufuatilia ugonjwa huu. Kupima kama kenya inavyofanya hakutoi picha halisi ya maambuizi ya ugonjwa.
5. Kuna mambo mawili katika ugonjwa huu. Mosi ni maambuki (cases) na pili ugonjwa au kuumwa sana (sevior cases). Mafanikio katika ugonjwa huu ni kutotishwa na idadi ya maambukizi, bali shughulika kikamilifu na wagonjwa ambao wanaumwa. Hili ni jambo la msingi sana, maana kuna nchi nyingi ambazo cases zinaongezeka, lakini serious cases, yaani wagnjwa hospitalini wanapungua sana. Mfano mmoja wapo ni nchi ya Sweden.
Huo ndiyo ukweli kuhusu huu ugonjwa wa kovidi.
Wananchi wa Kenya ni hofu tu kila wakati na takwimu zinapaishwa kila kukicha hasa pale rais anapotaka kutoa taarifa za ugonjwa kuna nini nyuma ya paziaNyie wenye hamuwezi kupata corona endeleeni kujivinjari
Safi sana rais, endelea kutupea takwimu zote hamna haja kuogopa au kujichokea, isemwe kama ilivyo, mwanzo mwanzoni tulikua na uwoga ila kwa sasa watu wamekua na ujasiri wa kupambana maana hamna kinachofichwa, tunaambiwa kama ilivyo bila kumumunya.
Hili suala la Corona hunikumbusha ilivyokua mara yangu ya kwanza kupima UKIMWI, yaani kabla kupata ujasiri wa kwenda kupima nilihangaika sana kwa uwoga, siku nyingi niliishi kwa kujiaminisha sina UKIMWI, ni gonjwa la mabeberu na haliniathiri, lipo kwa ajili ya wengine, mimi mzima, mimi kidume, nikawa najiaminisha pumba ila kila nikikohoa kidogo tu baasi naamini ndio hapo limenikuta, ila hatimaye nilipiga moyo konde na kupima na tangu kipindi hicho baada ya kupima sijawahi kusita kupima tena na tena, ukweli uliniweka huru......John 8:32
Bila kuujua ukweli, mtateseka sana kimawazo maana kila kifo cha mtu yeyote mnajikuta mkishuku na kueneza uvumi na tetesi kwmba kafa kwa Corona....
YOU CAN'T HANDLE THE TRUTH
Ni aibu sana watu mnaopenda kujiita wataalam na nyie pia mlishaingizwa kwenye hayo mawazo ya kujichokea, mpaka mnatumia nguvu nyingi kujaribu kueleza zero points, tafuta mtu akutafsirie nini maana ya "asymptomatic carriers of COVID-19" ambayo inasababisha watu wajitokeze kupimwa hata kama hawaumwi ili kuwalinda walio na magonjwa mengine kama kisukari.
Hiyo mnayopenda kujipa mfano nayo leo hii wanapukutika kushinda maelezo, uzuri wao hawafichi.
Wakati mwingine kuna mambo hutakiwi kuwaambia wananchi maana yanazidi kuhatarisha maisha yao. Kuna wakati unaweza ukawa umelalia nyoka bila kujua na ukaamka ukaondoka na nyoka asikuguse, lakini mtu anaweza kukuambia umelelia nyoka ukazimia ukafa, na saa ingine hata huyo nyoka pengine hayupo.
Kwahiyi MK254 si vizur kutangaza tangaza kiholela inachangia kuumiza watu pia na sio sifa ama democrasia! [emoji114][emoji114]
Uwe unakuwa makini sana kutumia neno kabla ya kulijua. Siyo kwa kuwa umesikia watu wakiongea, basi na wewe unadandia kulitumia hata pasipo stahili.