Safi sana rais, endelea kutupea takwimu zote hamna haja kuogopa au kujichokea, isemwe kama ilivyo, mwanzo mwanzoni tulikua na uwoga ila kwa sasa watu wamekua na ujasiri wa kupambana maana hamna kinachofichwa, tunaambiwa kama ilivyo bila kumumunya.
Hili suala la Corona hunikumbusha ilivyokua mara yangu ya kwanza kupima UKIMWI, yaani kabla kupata ujasiri wa kwenda kupima nilihangaika sana kwa uwoga, siku nyingi niliishi kwa kujiaminisha sina UKIMWI, ni gonjwa la mabeberu na haliniathiri, lipo kwa ajili ya wengine, mimi mzima, mimi kidume, nikawa najiaminisha pumba ila kila nikikohoa kidogo tu baasi naamini ndio hapo limenikuta, ila hatimaye nilipiga moyo konde na kupima na tangu kipindi hicho baada ya kupima sijawahi kusita kupima tena na tena, ukweli uliniweka huru John 8:32
Bila kuujua ukweli, mtateseka sana kimawazo maana kila kifo cha mtu yeyote mnajikuta mkishuku na kueneza uvumi na tetesi kwmba kafa kwa Corona.
YOU CAN'T HANDLE THE TRUTH