Rais Uhuru Kenyatta, William Ruto wafuata nyayo za Rais John Magufuli

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216
WAKATI Rais John Magufuli akionesha mfano kwa kubana matumizi katika safari za nje, nchini Kenya, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto wamepunguza safari za nje ya nchi kwa asilimia 79 ndani ya miezi tisa.
Kwa Rais Magufuli aliyeingia madarakani kuiongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania kuanzia Novemba 5, mwaka 2015, mpaka sasa hajatoka nje ya ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), licha ya kuripotiwa kuwa na mialiko ya zaidi ya nchi 100.

Ametembelea kikazi Rwanda, Uganda na Kenya ambazo ni sehemu ya nchi za EAC, nyingine zikiwa Tanzania, Burundi na Sudan Kusini.
Kazi nyingine za ndani na nje ya Afrika amekuwa akiwatuma ama Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wakati mwingine viongozi wengine waandamizi serikalini. Mathalani, katika kipindi cha miezi tisa wametumia Sh milioni 36.5 za Kenya kufikia Machi mwaka huu.

Taarifa kutoka kwa Mdhibiti wa Bajeti nchini Kenya zinaonesha kuwa, safari hizo zimeokoa zaidi ya Sh milioni 143.7 za Kenya, kutoka Sh milioni 180.2 zilizotumika katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Uamuzi wa kupunguza safari umeonekana kushika kasi zaidi tangu Rais Kenyatta aanze kuitawala Kenya katika awamu yake ya pili mwishoni mwa mwaka jana. Wakati anaingia madarakani Aprili mwaka 2013, Kenyatta alitumia Sh milioni 75.9 za Kenya kwa safari za nje.

Na tangu hapo, bajeti ya safari ilipaa. Kufikia Machi, 2016, alitumia Sh milioni 167.5 za Kenya kwa safari za nje, ikiwa ni ongezeko kutoka Sh milioni 138.5 zilizotumika katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Aidha, safari za mawaziri, wakuu wa mashirika na taasisi za umma nazo zimeshuka kwa asilimia 33 hadi Sh bilioni 3.07 za Kenya ikilinganishwa na Sh bilioni 4.6 za nchi hiyo zilizotumika mwaka uliopita, jambo linaloashiria kuwa, kazi ya kubana matumizi kwa safari za nje inazaa matunda.
JPM aokoa matrilioni Kwa mujibu wa Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kati ya Nonemba 2015 na Novemba 2016, serikali iliokoa kiasi cha Sh bilioni 902 kutokana na kusitisha safari za nje ya nchi kwa watumishi wa serikali. Ripoti hiyo ilionesha kuwa, Tanzania ilitumia kiasi cha Sh trilioni 1.7 katika safari za nje ya nchi, ikiwa ni sawa na punguzo la trilioni 1.2 ambapo kwa kipindi kama hicho Novemba 2014 hadi Novemba 2015, serikali ilitumia kiasi cha trilioni 2.64 kwa safari za nje ya nchi.

Novemba 6, 2015 ikiwa ni siku moja tangu aapishwe kuishika Ikulu ya Tanzania, Rais Magufuli alisema safari za nje ya nchi zilikuwa zikiigharimu Tanzania fedha nyingi ambazo zingeweza kutumiwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Mbali na kuzuia safari za nje ya nchi, Rais Magufuli pia alifuta semina elekezi kwa viongozi, alipiga marufuku kufanyia mikutano kwenye kumbi za hoteli, kufuta sherehe za uhuru na kadhalika na badala yake, fedha za shughuli hizo zilitumika kwa shughuli nyingine za maendeleo.

Kagame, Museveni Wakati Magufuli na Kenyatta wakionekana kushika hatamu katika kubana matumizi ya fedha za umma kwa safari za nje, marais wengine wa ukanda huo, nao wana mtazamo sawa.
Hata hivyo, Rais Paul Kagame wa Rwanda anaonekana kuwa na safari nyingi za nje kutokana na kuwa pia na majukumu ya kimataifa, kwani kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Kwa Museveni, pia safari zake za nje kwa sasa zinachangiwa pia na nafasi yake ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayohitaji safari za mara kwa mara za kikazi kwa ajili ya jumuiya hiyo yenye zaidi ya wakazi milioni 160.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi hajaonekana kuwa na safari za nje kwa takribani miaka miwili sasa, wakati Salva Kiir wa Sudan Kusini, naye amekuwa na safari chache, ukiondoa nyingi za safari za ndani ya jumuiya zinazolenga kumkutanisha na wadau wengine katika mchakato wa kusaka amani ya kudumu katika taifa hilo changa zaidi duniani.
 
Jiwe kutosafiri kwake kumeinufaisha vipi Nchi ili hali bado umaskini ni wa kutupwa na still Nchi ni omba omba tu
 
Wewe huwezi kuelewa!
Kuna mashirika ya ndege ya nje yamepunguza safari zake na mengine yamefuta kabisa kuja Dar, Maana wateja wao wakubwa walikuwa ni watumishi wa Serikali!
Usiongee vitu ambavyo huvijui kijana mdogo walahi!
That’s all!
 
Kwa hiyo mnaona ujiko sio kuharibu uchumi wa Nchi kwa upumbavu wenu na huyo jiwe wenu eti!??
 
Kwa hyo hii nayo unaona ni sifa?
 
Kwa hiyo mnaona ujiko sio kuharibu uchumi wa Nchi kwa upumbavu wenu na huyo jiwe wenu eti!??
Labda uchumi wa nyumbani kwako lakini wa taifa unasonga mbele SGR mwaka kesho inafungulia Dar to Moro ndege zimeshakuja nne sasa iliwemo dreamliner acha utendaji serikalini umekuwa bora sana!! Ila wewe ambaye ulizoa madili utapata taabu sana awamu hii. Mkuu badilika anza kupiga kazi na uchumi hapo nyumbani kwako utakuwa!!
 
Hizi ndo porojo zenu siku zote nyie wafuasi wa jiwe,boresheni huduma za kijamii kwanza hadi Leo bibiako anakunywa maji ya tope kijijini kwenu
 
Jiwe sio kwamba hapendi kwenda nnje anapenda sana tatizo ni luga hajui kuswahili wala kingereza, unategemea ataenda kuongea nini na wazungu[emoji23][emoji23]
Rais wa china haongei kiingereza na anakwenda kukutana na wanaozungumza kiinigereza. Na akikutana nao yeye hupiga kichina chake tu.

Mfano mwengine Umoja wa mataifa, kuna viongozi wanaongea lugha za kwao tu. kwaio Lugha sio sababu ya mtu asiende nje. Tafuta jengine
 
Badala ya kujisifia huduma bora za kijamii tunajisifia ujinger na upumbervou
 
Iyo pesa ya inayobaniwa matumizi si ndyo inanunua wabunge au???
 
Jiwe sio kwamba hapendi kwenda nnje anapenda sana tatizo ni luga hajui kuswahili wala kingereza, unategemea ataenda kuongea nini na wazungu[emoji23][emoji23]
Yani kwa akili yako Wachina wanapokuja hapa wanajua kiswahili? Embu kuwa mtu Wa kisasa. Vifaa vipo na wakalimani wapo.
 
Kubana matumizi ya serikali ya kenya si kwa kupenda kwao. IMF imeamuru GoK wasitishe matumizi ya pesa kwa miradi mipya na matumizi hovyo lasivyo waondoe Foreign Exchange reserve safety net. Si kwa hiari yao kama vile JPM amefanya mwenyewe
Unaongea vitu vikukwa na vipana for average Joe to understand.
 
Back
Top Bottom