Rais umewasikiliza wanaotaka katiba mpya! Je, sisi tusiotaka katiba mpya utatusikiliza lini? Tuna hoja!

Nyie tayari mulisikilizwa na marehemu ...mara ngapi tena?
 
Basi kama hamtaki, kaeni kimya. Kelele za nini, na wakati hamtaki? Waache wanaotaka, wapige kelele kudai hiyo Katiba Mpya.

Wewe endelea kulamba hilo buyu la asali, lililopo mbele yako.
Akumbuke kuwa, hilo buyu la asali analo lamba sasa siku moja litakwisha. Hapo ndipo akili zake timamu alizokuwa amezipoteza zitarudi.
 
Mama ni wale kama jk wanasema ukitaka kula lazima uliwe. Ukweli hatuna haja ya katiba mpya ila marekebisho ya hapa na pale. Mama anaunda tume kama uyoga kuwapa watu kula tu. Hadi natamani na kuona wivu huu ulaji anatoa mama. Ukweli hakuna tija yoyote ila kutuliza watu kwa kuwahonga.
 
the negative is usually incapable of proof
 
Acha kuwanga mchana...Nyinyi si mlisikilizwa kwa miaka hiyo 50 unayodai?
 
Walisifia nchi jirani wakati wa uchaguzi eti katiba mpya sasa kinachotokea huko siyo katiba mpya bali kitabu kipya
 

Na Rais akijitahidi akafanikisha katiba mpya, atakuwa amevunja rekodi na kukumbuka daima.
 

Africa kusini Rais anashtakiwa sio Kama bongo.
 
Hatuwezi kukaa kimya na Sasa tunaanza rasmi mapambano ya kupinga huo utopolo wenu

Unapinga Nini? Wewe unaumwa sio mzima. Kila mwaka bunge linaandika sheria mpya, mbona hujawahi kupinga? Ila katiba mpya ndio inakukera.
 
wote anawasikiliza usijali
 
Niko tayari kukosolewa na nimejiandaa kwenda kuzuia huu mchakato mahakamani

Unarudi kulekule, unataka kwenda kuzuia mchakato wa katiba mpya mahakamani lakini hujui kuwa mahakama ya kiktiba Tanzania haijawahi kufanya kazi? Maana haijatoa Nani mwenye mamlaka ya kupeleka mashauri pale na pia procedures. Sasa katiba mpya itatupatia mahakama ya katiba ili uwe na uwezo na kupeleka shauri la kikatiba mahakamani hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…