Duh...!. Mkuu
Mganguzi , kwanza nikupongeze kwa bandiko hili na kuheshimu uhuru wa maoni na uhuru wa kijieleza, yaani freedom of expression and freedom of speech.
Dunia ilipoumbwa, hakuna aliyejua dunia ni duara, watu wote kwa kutokujua kwao wakajua umbo la dunia ni umbo bapa.
Galileo Galilee alipogundua telescope na kuliona umbo la dunia kupitia kivuli cha kwenye mwezi, alipotangaza kuwa dunia ni duara, Galileo Galilee aliuwawa kwa kosa la kumkufuru Mungu kwa kitendo chake cha kusema dunia ni duara!.
Ukiwa hujaonja embe dodo ukiambiwa tunda tamu kuliko yote ni pera utaamini mpaka utakapoonja embe dodo ndio utagundua kumbe tunda tamu ni embe dodo.
Ukionja zabibu unagundua ni zabibu, ukionja nanasi unagundua ni nanasi, ukionja tende unagundua ni tende, ukionja asali ndipo utagundua asali ndio funga kazi ya utamu!.
Wewe ni mmoja wa Watanzania wasiojua katiba wala Umuhimu wa katiba mpya, hivyo wameridhika sana na hii katiba pera iliyopo, bila kuonjeshwa katiba embe, katiba nanasi, katiba tende na katiba asali, kamwe hauwezi kujua Umuhimu wa katiba mpya.
Hili la Watanzania kutujua katiba, hata Rais Samia amelisema
Hivyo watu kama akina sisi tuliobahatika kajiuwezo ka kusoma sheria na kuijua katiba, tumejitolea kuwaelimisha wengine Umuhimu wa katiba mpya kwanza kwa kuwaelimisha Watanzania wenzetu elimu ya katiba ili waifahamu katiba.
Angalia bandiko hili elimishi kuhusu kuijua katiba ni la lini na limechangiwa na watu wangapi ili kupata picha ya Watanzania wanavyotaka kuijua katiba
Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio ila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?
Just imagine mtu unajitolea kuelimisha umma kuhusu katiba halafu responses ndio hii!, utaendelea kweli?.
Hivyo watu kama nyinyi mnapojitokeza kusema hamuhitaji katiba mpya, hatuwashangai bali tunawahurumia!.
Laiti ungelijua tungekuwa na katiba bora, Tanzania tungekuwa wapi, ndipo ungeweza kujua tofauti ya utamu wa pera na asali!.
Kama una muda karibu pande hizi
- Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
- Mchakato huu wa Katiba ni umasikini wetu. Tujikubali, tuukubali, tuupigie kura ya ndio
- Je Wajua Kuwa Kura ya "Hapana" Kwa Katiba Mpya! Ni Kura ya "Ndiyo!" Kwa Katiba Hii Iliyopo?
- Bora Katiba tuikubali, tusiichukie CCM kwa sababu CCM itahukumiwa na Karma kwa Uovu wake
- Pascal Mayalla: CHADEMA watengeneze kwanza Katiba mpya ya chama chao kabla ya kukimbilia katiba ya nchi, wawatendee haki wabunge 19
- Mungu asingemchukua yule Mwamba, ilikuwa atuachie katiba mpya Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!.
- Sasa Mama atatuletea katiba mpya ila ni 2025 -2030, ila sisi washauri wa bure tumemshauri Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
P