Rais umewasikiliza wanaotaka katiba mpya! Je, sisi tusiotaka katiba mpya utatusikiliza lini? Tuna hoja!

Katiba mpya ni madai ya CDM vyama vingine wanafuata mkumbo ili siku mtu akitaka kwenda CDM apokelewa sababu katiba iliyopo haina ubaya kama unaosemwa kikubwa vyama pinzani wanaona kupata nafasi zingine ubunge ushakuwa kazi sana kutokana na kuwa na ushawishi mdogo kwa wananchi fikiria kama Mwenyekiti wa CDM amekosa jimbo sasa wanachofanya ni kutanua wigo wa kupata nafasi zingine kama u DC u kuu wa mkoa, ukurugenzi na nafasi ya katibu tawala pia wanataka nafasi ya u waziri kwamba Mh. Asiteue hao watu wapigiwe kura sasa wananchi tutakuwa tunafanya shughuli gani kila siku ni uchaguzi. Madai ya katiba mpya ni tamaa za madaraka za wapinzani wanaona CCM kama wanafaidi kumbe hata wakipigiwa kura kwenye hizo nafasi bado watakosa tu mfano mdogo tu kama udiwani ndani ya kata tu mnashindwa kushawishi wananchi ndio mtaweza wilaya au mkoa mnacheza nyie. Wananchi hawana shida na katiba iliyopo kama marekebisho ni madogo madogo sana tusisemee watu maneno ambayo hawajasema kama mnataka ukuu wa mkoa na wilaya nendeni mkaombe sio kushinikiza Serikali iliyopo madarakani mambo yenu binafsi.
 
Acha upotoshaji, katiba mpya sio ya wanasiasa pekee, wanasiasa au CHADEMA, wanaonekana mbele kwasababu Katiba inaanza na political process. Ila katiba inajumuisha makundi yafuatayo.

1. Wakulima
2. Wafanyakzi
3. Wafanyabiashara
4. Walemavu.
5. Wanafunzi.
6. Wanasiasa.
7. Wazee.
8. Wanawawake
9. Watoto.
10. Wasiojiweza.
11. Wanamichezo.
12. Wasanii.
13. Wanataaluma.

Pia, katiba mpya sio kwaajili ya udc au ubunge Bali inajumuisha mambo mengi. Kama.

1. Muuondo wa muungano.
2. Haki za binadamu.
3. Maadili ya taifa.
4. Uchumi.
5. Ushirikiano wa kimataifa.
6. Kodi na mapato ya taifa.
7. Rasilimali za nchi.
8. Wajibu wa kila Raia.
9. Wajibu wa serikali.
10. Mahakama
11. Bunge.
12. Mamlaka ya nchi.
13. Vyombo vya ulinzi na usalama.
14. Tume ya uchaguzi. Nk.

Kwa hivyo chadema Kama wanasiasa wait Wana haki ya kujadili mambo yanayo wahusu kwenye katiba na wengine wataingilia Kati.
 
Katiba mpya ni madai ya CDM vyama vingine wanafuata mkumbo ili siku mtu akitaka kwenda CDM apokelewa sababu katiba iliyopo haina ubaya kama unaosemwa kikubwa vyama pinzani wanaona kupata nafasi zingine ubunge ushakuwa kazi sana kutokana na kuwa na ushawishi mdogo kwa wananchi fikiria kama Mwenyekiti wa CDM amekosa jimbo sasa wanachofanya ni kutanua wigo wa kupata nafasi zingine kama u DC u kuu wa mkoa, ukurugenzi na nafasi ya katibu tawala pia wanataka nafasi ya u waziri kwamba Mh. Asiteue hao watu wapigiwe kura sasa wananchi tutakuwa tunafanya shughuli gani kila siku ni uchaguzi. Madai ya katiba mpya ni tamaa za madaraka za wapinzani wanaona CCM kama wanafaidi kumbe hata wakipigiwa kura kwenye hizo nafasi bado watakosa tu mfano mdogo tu kama udiwani ndani ya kata tu mnashindwa kushawishi wananchi ndio mtaweza wilaya au mkoa mnacheza nyie. Wananchi hawana shida na katiba iliyopo kama marekebisho ni madogo madogo sana tusisemee watu maneno ambayo hawajasema kama mnataka ukuu wa mkoa na wilaya nendeni mkaombe sio kushinikiza Serikali iliyopo madarakani mambo yenu binafsi.

Acha kujificha kwenye mgongo wa wananchi. Mwaka 1977 Tanzania iliandika katiba mpya, je wananchi waliamdamana kuishinikiza katiba mpya?. Tusiwatumie wananchi Kama mgongo wa kakimbia majukumu.
 
Mama ni wale kama jk wanasema ukitaka kula lazima uliwe. Ukweli hatuna haja ya katiba mpya ila marekebisho ya hapa na pale. Mama anaunda tume kama uyoga kuwapa watu kula tu. Hadi natamani na kuona wivu huu ulaji anatoa mama. Ukweli hakuna tija yoyote ila kutuliza watu kwa kuwahonga.

Unajipinga mwenyewe. Unataka Katiba ifanyiwe marekebisho ila hutaki katiba mpya kisa wanatume watalipwa pesa?. Huo ni wivu tu. Mbona miaka michache iliyopita watu waliunga juhudi na Uchaguzi ulikuwa unafanyika kila siku?. Mbona hukuhoji Hilo?

Mbona katiba iliandikwa mwaka 1977 hamkulalamika? Ikaja kufanyiwa marekebisho makubwa 1984 hamkulalamika? Imefanyika marekebisho mpaka 2005. Sasa kwanini tufanye marekebisho baadla ya kuandika mpya. Mnataka nchi iende kibabe kwa maslahi ya Nani?.
 
Mkuu Mganguzi kwanza nikupongeze kwa kuwa na maoni tofauti na lazima tuheshimu kwa kuwa Kila mtanzania anauhuru wa kutoa maoni yake.

Ila napata mashaka kwamba hata hii katiba ya Sasa Bado hauijui na ndio maana huwezi kuona mapungufu yake, kwa upana wa katiba hii lakini wewe umeona jambo moja tu AMANI. Ni kweli AMANI ni jambo muhimu lakini hii katiba ya Sasa inamengi sana yanayokandamiza hiyo AMANI unayoizungumzia.

Ushauri; Kabla hatujaanza kujibizana kwa hoja tumia muda kwanza kupitia katiba ya Sasa ya nchi halafu Rudi ulete neno.

Alamsik.
 
Asalaam ndugu zangu ..nianze Kumpongeza rais kwa kusikiliza hoja za watu wa kada mbalimbali hasa wa mlengo wa kisiasa wakidai katiba mpya .. wamesikilizwa na ninasikia mchakato karibia utaanza ni jambo jema ... Lakini tupo sisi ambao hatukubaliani na mchakato huo .. hatuhitaji katiba mpya na tuna hoja na sababu za msingi ..nchi yetu imekuwa na amani kwa miaka zaidi ya 50 kwa katiba hii .. nchi yetu imekuwa na uchumi unaokuwa vizuri kwa katiba hii ... Kwa sisi tusiotaka katiba utatusikiliza lini ? Na sisi tuna haki ya kusikilizwa kama ulivyowasikiliza hao wanaotaka katiba mpya !! Mimi na wenzangu wengi TU tusiotaka katiba mpya tutasikilizwa lini ? Hatutaki kabisa katiba mpya !! Tumeona nchi jirani zilizokimbilia katiba mpya kwa minajiri ya ustawi kisiasa na maisha ya watu wetu lakini imekuwa kinyume chake! Kenya vurugu tupu! Afrika kusini vurugu tupu !! Nchi zote zilizothubutu kubadilisha katiba ziliingia kwenye migogoro isiyoisha .. please rais hakuna legacy yoyote utakayoiacha kwa kuleta katiba mpya zaidi ya fujo na vurugu ..asanteni
..

Wanaotaka katiba mpya wamejitokeza hadharani na kuidai, na wanafahamika waziwazi. Je nyie msiotaka katiba mpya kwanini hamjitokezi muipinge hadharani?
 
Asalaam ndugu zangu ..nianze Kumpongeza rais kwa kusikiliza hoja za watu wa kada mbalimbali hasa wa mlengo wa kisiasa wakidai katiba mpya .. wamesikilizwa na ninasikia mchakato karibia utaanza ni jambo jema ... Lakini tupo sisi ambao hatukubaliani na mchakato huo .. hatuhitaji katiba mpya na tuna hoja na sababu za msingi ..nchi yetu imekuwa na amani kwa miaka zaidi ya 50 kwa katiba hii .. nchi yetu imekuwa na uchumi unaokuwa vizuri kwa katiba hii ... Kwa sisi tusiotaka katiba utatusikiliza lini ? Na sisi tuna haki ya kusikilizwa kama ulivyowasikiliza hao wanaotaka katiba mpya !! Mimi na wenzangu wengi TU tusiotaka katiba mpya tutasikilizwa lini ? Hatutaki kabisa katiba mpya !! Tumeona nchi jirani zilizokimbilia katiba mpya kwa minajiri ya ustawi kisiasa na maisha ya watu wetu lakini imekuwa kinyume chake! Kenya vurugu tupu! Afrika kusini vurugu tupu !! Nchi zote zilizothubutu kubadilisha katiba ziliingia kwenye migogoro isiyoisha .. please rais hakuna legacy yoyote utakayoiacha kwa kuleta katiba mpya zaidi ya fujo na vurugu ..asanteni
..
Wengi wape
 
Kula chuma hicho
B11F099C-619F-4CA2-8F4D-164FC6E0268A.jpeg
 
Back
Top Bottom