Katiba mpya ni madai ya CDM vyama vingine wanafuata mkumbo ili siku mtu akitaka kwenda CDM apokelewa sababu katiba iliyopo haina ubaya kama unaosemwa kikubwa vyama pinzani wanaona kupata nafasi zingine ubunge ushakuwa kazi sana kutokana na kuwa na ushawishi mdogo kwa wananchi fikiria kama Mwenyekiti wa CDM amekosa jimbo sasa wanachofanya ni kutanua wigo wa kupata nafasi zingine kama u DC u kuu wa mkoa, ukurugenzi na nafasi ya katibu tawala pia wanataka nafasi ya u waziri kwamba Mh. Asiteue hao watu wapigiwe kura sasa wananchi tutakuwa tunafanya shughuli gani kila siku ni uchaguzi. Madai ya katiba mpya ni tamaa za madaraka za wapinzani wanaona CCM kama wanafaidi kumbe hata wakipigiwa kura kwenye hizo nafasi bado watakosa tu mfano mdogo tu kama udiwani ndani ya kata tu mnashindwa kushawishi wananchi ndio mtaweza wilaya au mkoa mnacheza nyie. Wananchi hawana shida na katiba iliyopo kama marekebisho ni madogo madogo sana tusisemee watu maneno ambayo hawajasema kama mnataka ukuu wa mkoa na wilaya nendeni mkaombe sio kushinikiza Serikali iliyopo madarakani mambo yenu binafsi.