Ninaandika huu ujumbe nikiwa katika hali ya uchungu mkubwa. Nimechoka! Nimevunjwa moyo! Nimeonewa kiasi cha kuhisi mimi si binadamu tena. Kila siku naamka nikiwa na maumivu mapya, nikiwa na mzigo mzito wa uonevu moyoni mwangu. Ninaomba msaada! Ninaomba mwenye kusikia kilio cha mnyonge anisaidie!
Mwaka 2022 nilipata nafasi adimu ambayo ilikuwa mwanga wa matumaini kwangu na kwa familia yangu. Nilijua maisha yangu yatabadilika, nikajua juhudi zangu hatimaye zitalipa. Lakini ndoto hiyo ilizimwa kwa sababu tu sikuwa na pesa ya kutoa rushwa! Nimehangaika kwa miaka miwili sasa, nikilia na kusihi, lakini kila ninapokwenda, nimepuuzwa! Nimefungiwa milango! Nimechukuliwa kama mtu asiye na thamani!
Badala ya msaada, nimetishiwa! Nimeambiwa nitafunguliwa kesi ya uongo, nitaambiwa si Mtanzania eti kwa sababu sikutoa rushwa! Naumia! Naumia sana! Nauliza, hivi kweli haki ni ya matajiri peke yao? Hivi kweli maskini hana nafasi katika nchi hii?
Mheshimiwa Rais, tafadhali, naomba msaada wako! Mimi ni kijana mdogo tu, sina nguvu ya kupigana na mfumo huu wenye uonevu. Nimechoka! Sina pa kukimbilia tena! Naomba unisikie, naomba unione, naomba unisaidie!
Na kwa yeyote anayeguswa na mateso yangu, naomba unisaidie! Kama una njia yoyote ya kunisaidia, tafadhali usikae kimya, nisaidie kwa hali na mali! Nimeumia vya kutosha, nimenyanyaswa vya kutosha, nimeonewa vya kutosha!
Sauti ya mnyonge ni dhaifu, lakini haipaswi kupotea! Tafadhali, yeyote mwenye huruma, mwenye utu, mwenye uwezo wa kunisaidia, ninaomba msaada wenu! Nimebakia peke yangu kwenye giza, naomba mwangaza wenu!
Mheshimiwa Rais, na watu wote wenye utu, tafadhali, naomba msaada wenu! Usiniruhusu niteseke hivi!

Mwaka 2022 nilipata ufadhili wa masomo hivyo ikabidi niende kurasini kuomba passport, nilienda na documents zote kama utambulisho wangu. Nilipofika mapokezi nikasikilizwa vizuri na nikaambiwa niende chumba namba 115 kwa afisa aliyeitwa Renatus Vincent.
Afisa huyu baada ya kumpa documents zangu alinihoji vizuri na akaniambia nimpe namba ya mzazi ili aongee naye kama ni kweli hivyo basi baada ya kumpigia hawakuelewana vizuri sababu ya kelele ikabidi afisa huyo aniambie nilipie na kwenda kupiga picha na kuweka fingerprint hivyo ataongea naye kwa muda wake. Nakumbuka nilipoenda kupiga picha nikapewa tarehe ambayo naikumbuka 24/01/2022 ya kwenda kuchukua passport posta.
Lakini nilipoenda kuchukua passport sikuikuta zaidi niliambiwa kuna document ambayo haipo hivyo nirudi tena Kurasini kwa yule afisa. Hivyo nilipoenda kwa yule afisa akaniambia bado hajaongea na mzazi nimpe muda aongee naye, nakumbuka Ijumaa nilipompigia sababu alinipa namba alisema siwezi kupata passport sababu mzazi kashindwa kujieleza vizuri na ikizingatia anatokea Kigoma.
Hivyo ikabidi niwatoe wazazi mkoani waje hapa Kurasini kuhojiwa vizuri lakini afisa huyo alikataa kabisa kusaidia zaidi ya kusema Mimi siyo Mtanzania hivyo nimpe milioni 1 anisaidie au niombe uraia. Baada ya kuona hanisaidii ikabidi niende kwa kiongozi wake ambaye ni PCO kwa jina la pale anaitwa mama Dora ingawa sasa hayupo.
Kiongozi huyu hakuonesha kunisaidia sababu alikuwa upande wa yule afisa naye alitaka nitoe hiyo pesa. Ikabidi nitafute msaada zaidi sababu hakuna anayenisaidia ikabidi nitafute namba ya kamishina wa passport kwa jina anaitwa Gerald Kihinga, nakumbuka nilipompigia simu kumweleza changamoto yangu alisikitika sana akaniambia niende nipewe passport sababu yeye alikuwa amesafiri yupo Kagera.
Nilipoenda Kurasini yule afisa pamoja na yule PCO wakaniambia watanipa passport ya miaka 5 wakasema niende nikachukue posta. Nakumbuka ilikuwa Jumatatu nilipoenda pasta niliambiwa haipo ikabidi nimpigie tena Kihinga nakumbuka aliniambia njoo huku Kurasini.
Hivyo basi nilipokuwa namngoja Kihinga ndani ya ofisi yake ghafla akatokea PCO, nakumbuka aliniambia kwa hiyo umekuja kunisemea kwa boss wangu? Basi PCO yule akanifukuza nisionane na kamishina akanipeleka ofisini kwake pia akamuita yule afisa wa mwanzo then Mimi wakanitoa nje wakabaki wawili nakumbuka walikaa kama nusu saa then wakanichukua hadi kwa Kihinga na wakati wanaingia wakaniambia nibaki nje kwanza hivyo sijui kilichoendelea ndani ndo nikaitwa ndani baada ya dakika 30 basi Kihinga akabadilika akasema nitoe milioni 1 niombe uraia.
Sasa nikawa sina mtetezi tena ikabidi nitafute mbunge wangu ambaye alikuwa Kitila Mkumbo nikampigia simu nikamueleza hakika nakumbuka alisikitika sana akasema hata yeye mke wake jambo hili liliwahi kumkuta hivyo ndo maisha akasema ngoja awasiliane na uhamiaji.
Nakumbuka alinipigia Ijumaa jioni saa mbili usiku aliniambia Jumatatu niende uhamiaji kwa Kamishina sababu jambo limekaa sawa. Basi Jumatatu na mapema nikadamka hadi kwa Kihinga, lakini bado alisema nitoe milioni 1 ili anipe mtu anisaidie. Ikabidi niende siku nyingine nakumbuka siku hiyo nilienda nimevaa nguo nyekundu hakika nakumbuka siku hiyo msaidizi wa kamishina aliniambia niende nje nikatafute nguo nyingine nivae sababu nguo ile ilikuwa nyekundu kama jezi ya simba na ukizingatia kamishina alikuwa ni Yanga na walikuwa wamefungwa siku iliyopita na Simba, yule msaidizi alisema hatanisikiliza na hiyo nguo bora urudi uje wakati mwingine. Basi ikabidi nimpigie tena Kitila Mkumbo kumwambia kwamba bado wanataka pesa nakumbuka alisema watafutie tu wape kwani siunaenda kusoma nje sasa pesa hiyo itakushinda nini?
Basi hadi leo nikimtafuta hapokei wala hajibu SMS kama mwanzo, ikabidi nianze kumtafuta Waziri wa Mambo ya ndani ambaye alikuwa Masauni, nikafanikiwa kupata namba zake nikampigia pia nikamtumia ujumbe kwa njia ya WhatsApp alinijibu akanipa namba ya kamishina mkuu wa uhamiaji akasema nimtafute. Siku iliyofuata nikamtafuta akasema niende uhamiaji, nakumbuka nilipoenda afisa wakanikataza kuingia wakisema wewe ni nani umepata wapi namba ya mheshimiwa na kwanini umtafute basi tuwambie sisi una shida gani.
Ikabidi niende siku yake, nakumbuka nilienda asubuhi lakini nilionana naye saa kumi jioni. Akaniita akanihoji pia akamuita yule afisa lakini nasikitika yule afisa akaanza kuongea uongo kwamba nipipofika mapokezi watoa huduma walinishuku kwamba Mimi siyo RAIA.
Basi kamishina akasema niende nitafute cheti cha kuzaliwa cha bibi au babu then nimpe yule afisa wa mwanzo. Nilipoenda kutafuta nikakosa nikamfata yule afisa kumwambia nimekosa ila nina barua ya kiapo lakini yule afisa alikataa na akisema kesi haipo kwake hivyo ipo kwa Kamishna mkuu, sasa nikajikuta sina msaada tena nikimpigia kamishina anasema nilikupa mtu na yule mtu nikimfata anasema kesi yako iko juu
Basi ikabidi niandikie barua tena kwa Waziri wa Mambo ya ndani wa sasa lakini tokea mwezi wa kwanza sijajibiwa hivyo nakosa msaada.
Naomba mheshimiwa Rais na viongozi wengine watakaoguswa jambo hili naomba msaada