Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amteua Mohamed Dewji (Mo) kuwa mshauri wake kwenye masuala ya Uwekezaji

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa amemteua Mohamed Dewji kuwa mshauri wake wa Masuala ya uwekezaji.

Mohamed dewji 'MO' atashiriki vikao vyote vinavyohusiana na uwekezaji na atakuwa miongoni mwa washauri wa Rais Ramaphosa kwa kipindi Cha miaka mitatu.

----
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua mfanyabiashara kijana nchini, Mohamed Dewji (Mo) kuwa kwenye jopo lake la watu watano kumshauri kuhusu masuala ya uchumi na uwekezaji.

Dewji, ambaye hivi karibuni Jarida maarufu la Forbes limemtaja kuwa bilionea kijana wa 13 kati ya 18 barani Afrika, ameingia kwenye jopo hilo ambalo lengo ni kupanga mikakati ya namna bora ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Afrika Kusini.

Taarifa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa Mo Dewji, anayemiliki kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL), atakuwa kwenye chombo hicho kwa kipindi cha miaka mitano.

Imesema kuwa uamuzi wa Ramaphosa kumteua Mo Dewji kuwa mshauri wake umetokana na kuvutiwa na jitihada za mfanyabiashara huyo maarufu nchini, kubobea kwenye masuala ua uchumi, huku akiifanya MeTL kuwa miongoni mwa kampuni bora Afrika.

Pia, uteuzi huo umeelezwa kuwa unatokana na Ramaphosa kuthamini na kutambua mchango wa Mo katika uwekezaji ambao umekuwa kichocheo kwa uchumi wa mataifa mbalimbali Afrika.

“Ninayo furaha kubwa kukujulisha kwamba, nimekuteua kwenye Baraza la Ushauri la Rais kuhusu uwekezaji ambalo lina jukumu kubwa kuhakikisha Afrika Kusini inapiga hatua kiuchumi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

“Imani yangu ni kuwa kwa kutumia umahiri na uzoefu wako kwenye masuala ya biashara, utashirikiana vyema na wajumbe wengine katika kutupa mwanga ili kuongeza tija kwenye ukuaji wa uchumi na kuvutia wawekezaji zaidi,” imesema taarifa hiyo.

Afrika Kusini ni miongoni mwa mataifa ya Afrika yenye uchumi imara na unaopiga hatua kwa kasi na mikakati ya Rais Ramaphosa ni kuona sera na jitihada zake zinaongeza tija kwenye ukuaji wa uchumi na uwekezaji mpya.

Baraza hilo la ushauri litakuwa jukwaa la kuchakata mawazo, vikwazo na kuangalia njia bora za kukuza ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi, wadau wa maendeleo na mawakala wa uwekezaji ili Afrika Kusini ipige hatua katika maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia.

Kutokana na uteuzi huo, Mo Dewji atapata fursa ya kuhudhuria vikao mbalimbali vitakavyoandaliwa ndani na nje ya Afrika Kusini vitakavyohusisha wafanyabiashara, viongozi wa Serikali ikiwa ni ukuzaji wa uchumi na kuwavutia wawekezaji.

Mwananchi
Meko alitaka kumuua huyu.
 
Ajabu ni kwamba sisi kwetu tunamuona MO kama mfadhili/mdhamini wa Simba na mfanyabiashara mkubwa...wenzetu wanamtumia kupiga hatua kimaendeleo kama nchi
 
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua mfanyabiashara kijana nchini, Mohamed Dewji (Mo) kuwa kwenye jopo lake la watu watano kumshauri kuhusu masuala ya uchumi na uwekezaji.

Dar es Salaam. Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua mfanyabiashara kijana nchini, Mohamed Dewji (Mo) kuwa kwenye jopo lake la watu watano kumshauri kuhusu masuala ya uchumi na uwekezaji.

Dewji, ambaye hivi karibuni Jarida maarufu la Forbes limemtaja kuwa bilionea kijana wa 13 kati ya 18 barani Afrika, ameingia kwenye jopo hilo ambalo lengo ni kupanga mikakati ya namna bora ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Afrika Kusini.

Taarifa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa Mo Dewji, anayemiliki kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL), atakuwa kwenye chombo hicho kwa kipindi cha miaka mitano.

Imesema kuwa uamuzi wa Ramaphosa kumteua Mo Dewji kuwa mshauri wake umetokana na kuvutiwa na jitihada za mfanyabiashara huyo maarufu nchini, kubobea kwenye masuala ua uchumi, huku akiifanya MeTL kuwa miongoni mwa kampuni bora Afrika.

Pia, uteuzi huo umeelezwa kuwa unatokana na Ramaphosa kuthamini na kutambua mchango wa Mo katika uwekezaji ambao umekuwa kichocheo kwa uchumi wa mataifa mbalimbali Afrika.

“Ninayo furaha kubwa kukujulisha kwamba, nimekuteua kwenye Baraza la Ushauri la Rais kuhusu uwekezaji ambalo lina jukumu kubwa kuhakikisha Afrika Kusini inapiga hatua kiuchumi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

“Imani yangu ni kuwa kwa kutumia umahiri na uzoefu wako kwenye masuala ya biashara, utashirikiana vyema na wajumbe wengine katika kutupa mwanga ili kuongeza tija kwenye ukuaji wa uchumi na kuvutia wawekezaji zaidi,” imesema taarifa hiyo.

Afrika Kusini ni miongoni mwa mataifa ya Afrika yenye uchumi imara na unaopiga hatua kwa kasi na mikakati ya Rais Ramaphosa ni kuona sera na jitihada zake zinaongeza tija kwenye ukuaji wa uchumi na uwekezaji mpya.

Baraza hilo la ushauri litakuwa jukwaa la kuchakata mawazo, vikwazo na kuangalia njia bora za kukuza ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi, wadau wa maendeleo na mawakala wa uwekezaji ili Afrika Kusini ipige hatua katika maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia.

Kutokana na uteuzi huo, Mo Dewji atapata fursa ya kuhudhuria vikao mbalimbali vitakavyoandaliwa ndani na nje ya Afrika Kusini vitakavyohusisha wafanyabiashara, viongozi wa Serikali ikiwa ni ukuzaji wa uchumi na kuwavutia wawekezaji.
🥱🥱kwa Bongo tunakumbuka tu watu wasiojulikana
 
Ujumbe Kwa Kigwangalla,

Dangote & Mo Dewj hawakua ma billionea kwasababu tu ya kuandika "AMEN" na kugonga "LIKE" katika mitandao ya kijamii mchana kutwa. Walifanya kazi kwa juhudi...!!!

Andika barua ya kuomba kazi kwa Mo Dewj ukiambatanisha na CV zako zote, ukatumwe hata kufuata chumvi dukani.

NOTE THAT: Tofauti ya Rais na Mchawi;

Rais: Anachagua matajiri kuwa washauri wake kwenye maswala ya biashara.!!!

Mchawi: Matajiri wataishi kama mashetani.!!!
Hapa Tanzania kikundi fulani cha watu wenye uchu na hila kilimteka na mwishowe tukaletewa ile ccctv ya Sirro na gari lake la Msumbiji
 
Ona lijiwe lilivyoifanya nchi, marais wengine wanawatumia matajiri wetu kuinua uchumi wao, sisi tunafanya nini..mama naamini atatumia mbinu hio lengo na sisi tufaidike na hawa matajiri kwa kuzingatia sheria ambazo si kandamizi kwao.
 
Huku kwetu mwendazake aliishia kumteka ili kupora fedha.
Mwendazake alikua disaster kwa nchi yetu, potential Kama hizi hakuziona.

Kwenda zako mwendazake
Moderator kama mnaruhusu ujinga huu ijulikane basi
 
Mbona lile taahira lenu kule twiter mnaloliamini sana kina muona tapeli na huwa mnashangilia
Nani huyo?
Nilivhomaanisha ni kuwa mo alitekwa na kina Bashite wakachukua mpunga mrefu wakamrudisha.
Kwa hio hutaki?
 
Ukiwa Rais Safi sana, watu wako wa kuoiga nao story unawateuwa basi huku tunadhani ni cheo kapata
 
Wawekezaji wote walikuwa wanaangalia Kama ni wahujumu uchumi. Kwa maana nyingine wenye akili ya kibiashara walikuwa wanabezwa badala yake wanakumbatiwa bodaboda, mama ntilie au mambumbumbu ndo jamaa anayakumbatia.

Hebu angalia nchi zenye akili na mwelekeo mzuri wa uchumi Kama south africa wamemuomba no dewji awe mshauri wa masuala ya uchumi na biashara wa rais wao lakini sisi tuliishi kumteka na kumharas tu.

Sijui jpm angemaliza miaka kumi nchi ingekuwa na Hali gani. Labda wote tungekuwa machinga nchi hii au bodaboda Mana ndo ilikuwa dreams zake ili abaki tajiri peke yake.

We had the fake president.
 
Na mbaya zaidi mwendazake alikuwa ashawatia hii akili mbovu baadhi ya watanzania
 
Umewahi kuishi South Africa?hali ya wenye asili ya nchi ile ikoje??
 
Back
Top Bottom