Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amteua Mohamed Dewji (Mo) kuwa mshauri wake kwenye masuala ya Uwekezaji

Usjali mkuu,now kumepambazuka ingawa Kuna watu wanamhujumu MAMA YETU,Ila hatutakubali!
 
Huyo Mo ni kanjanja tu Hamna lolote,S.A ndio inaongoza kwa Mabilionea Afrika ashindwe kuwachukua hao aje amuchukue huyo Mhindi wenu.
 
Umewahi kuishi South Africa?hali ya wenye asili ya nchi ile ikoje??
Unataka kudanganya hapo SA ukiwa na id tuu yaani huduma nyingi unapata kwa zero deposit mpaka Elimu ukitaka kufungua kampuni mfano ya usafirishaji au mitambo id yako ndio dhamana Nchi gani Africa kuna kitu kama hicho ni baadhi ya watu wamelala hasa waliotoka maporini na kukosa Elimu...
 
Hongera zake Dewji.

Rais Ramaphosa inakuwa kama ana nafasi maalum ya mshauri wa uchumi kutoka Tanzania.

Hii nafasi alikuwa nayo gavana wa zamani wa BOT Dr. Benno Ndulu mpaka anafariki hivi karibuni.

Dr. Benno Ndulu amefariki February 22 2021, Rais Ramaphosa amemteua Dewji kushika nafasi hiyo.
kwahyo Mo atakua akilipwa na huyo Rais?
 
Ujumbe Kwa Kigwangalla,

Dangote & Mo Dewj hawakua ma billionea kwasababu tu ya kuandika "AMEN" na kugonga "LIKE" katika mitandao ya kijamii mchana kutwa. Walifanya kazi kwa juhudi!

Andika barua ya kuomba kazi kwa Mo Dewj ukiambatanisha na CV zako zote, ukatumwe hata kufuata chumvi dukani.

NOTE THAT: Tofauti ya Rais na Mchawi;

Rais: Anachagua matajiri kuwa washauri wake kwenye maswala ya biashara!

Mchawi: Matajiri wataishi kama mashetani!
hii ya wachawi ni kiboko 😂😂
 
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua mfanyabiashara kijana nchini, Mohamed Dewji (Mo) kuwa kwenye jopo lake la watu watano kumshauri kuhusu masuala ya uchumi na uwekezaji.

Tanzania billionaire Mohammed Dewji told kidnapper to shoot him - BBC News

Dewji, ambaye hivi karibuni Jarida maarufu la Forbes limemtaja kuwa bilionea kijana wa 13 kati ya 18 barani Afrika, ameingia kwenye jopo hilo ambalo lengo ni kupanga mikakati ya namna bora ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Afrika Kusini.

Taarifa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa Mo Dewji, anayemiliki kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL), atakuwa kwenye chombo hicho kwa kipindi cha miaka mitano.

Imesema kuwa uamuzi wa Ramaphosa kumteua Mo Dewji kuwa mshauri wake umetokana na kuvutiwa na jitihada za mfanyabiashara huyo maarufu nchini, kubobea kwenye masuala ya uchumi, huku akiifanya MeTL kuwa miongoni mwa kampuni bora Afrika.

Pia, uteuzi huo umeelezwa kuwa unatokana na Ramaphosa kuthamini na kutambua mchango wa Mo katika uwekezaji ambao umekuwa kichocheo kwa uchumi wa mataifa mbalimbali Afrika.

“Ninayo furaha kubwa kukujulisha kwamba, nimekuteua kwenye Baraza la Ushauri la Rais kuhusu uwekezaji ambalo lina jukumu kubwa kuhakikisha Afrika Kusini inapiga hatua kiuchumi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
 
Hongera zake
 
Hongera zake Dewji!
Majambazi toka msumbiji walitaka kumpoteza.
Lala salama Jiwe,tutakukumbuka kwa mabaya pia.
 
SAFI SANA, NA SIO NCHI ZETU MAPROFESA UCHWARA WA THEORY NDIO WASHAURI, WANAACHA KUTOA THEORY ZAO ZA NYUNGU MADARASANI WANAINGIA KWENYE PRACTICALS.
 
Hivi Tz washauri wa Rais huwa ni kina nani?
 
Back
Top Bottom