Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amteua Mohamed Dewji (Mo) kuwa mshauri wake kwenye masuala ya Uwekezaji

Usjali mkuu,now kumepambazuka ingawa Kuna watu wanamhujumu MAMA YETU,Ila hatutakubali!
 
Huyo Mo ni kanjanja tu Hamna lolote,S.A ndio inaongoza kwa Mabilionea Afrika ashindwe kuwachukua hao aje amuchukue huyo Mhindi wenu.
 
Umewahi kuishi South Africa?hali ya wenye asili ya nchi ile ikoje??
Unataka kudanganya hapo SA ukiwa na id tuu yaani huduma nyingi unapata kwa zero deposit mpaka Elimu ukitaka kufungua kampuni mfano ya usafirishaji au mitambo id yako ndio dhamana Nchi gani Africa kuna kitu kama hicho ni baadhi ya watu wamelala hasa waliotoka maporini na kukosa Elimu...
 
kwahyo Mo atakua akilipwa na huyo Rais?
 
Hii mada itaharibika wakija watu wa yanga🀣🀣

Wataiona imekaa kimichezo na kuipendelea simba.
Utuache..
Bado tunaomboleza.
Baada ya siku 21 kupita, tumeongeza sita.
 
hii ya wachawi ni kiboko πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua mfanyabiashara kijana nchini, Mohamed Dewji (Mo) kuwa kwenye jopo lake la watu watano kumshauri kuhusu masuala ya uchumi na uwekezaji.



Dewji, ambaye hivi karibuni Jarida maarufu la Forbes limemtaja kuwa bilionea kijana wa 13 kati ya 18 barani Afrika, ameingia kwenye jopo hilo ambalo lengo ni kupanga mikakati ya namna bora ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Afrika Kusini.

Taarifa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa Mo Dewji, anayemiliki kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL), atakuwa kwenye chombo hicho kwa kipindi cha miaka mitano.

Imesema kuwa uamuzi wa Ramaphosa kumteua Mo Dewji kuwa mshauri wake umetokana na kuvutiwa na jitihada za mfanyabiashara huyo maarufu nchini, kubobea kwenye masuala ya uchumi, huku akiifanya MeTL kuwa miongoni mwa kampuni bora Afrika.


Pia, uteuzi huo umeelezwa kuwa unatokana na Ramaphosa kuthamini na kutambua mchango wa Mo katika uwekezaji ambao umekuwa kichocheo kwa uchumi wa mataifa mbalimbali Afrika.

β€œNinayo furaha kubwa kukujulisha kwamba, nimekuteua kwenye Baraza la Ushauri la Rais kuhusu uwekezaji ambalo lina jukumu kubwa kuhakikisha Afrika Kusini inapiga hatua kiuchumi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
 
Hongera zake
 
Hongera zake Dewji!
Majambazi toka msumbiji walitaka kumpoteza.
Lala salama Jiwe,tutakukumbuka kwa mabaya pia.
 
Hongera sana, wakina kanjibahi sasa meno yote nje πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
SAFI SANA, NA SIO NCHI ZETU MAPROFESA UCHWARA WA THEORY NDIO WASHAURI, WANAACHA KUTOA THEORY ZAO ZA NYUNGU MADARASANI WANAINGIA KWENYE PRACTICALS.
 
Hivi Tz washauri wa Rais huwa ni kina nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…