Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua

Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua

Nadhani taarifa waliyotoa inatosha kabisa. Tena wamefanya uungwana sana maana Magufuli alikuwa rais lakini hawakutoa taarifa yoyote. Privacy wanayotaka ni katika kumuuguza, watu wasiwachokonoe kwa kuwazongazonga. Augue pole.
Sisi wananchi tunataka tukamuone hapo wodini akiwa anapewa matibabu, ubaya uko wapi? Hadi awekewe faragha?
 
Watoto wa Mwinyi wengine tumewakaribisha kutoka Zanzibar, tumesoma nao vizuri, tumekuwa marafiki wakiwa watu wa kawaida sana mpaka tukawa tunatilia shaka kama hawa ni watoto wa rais kweli au tunadanganywa tu, kwa jinsi walivyoishi maisha ya kawaida.

No wazi walilelewa kwa maadiki ya kuthamini utu wa watu kuliko kujiona wao watoto wa rais.

Kwa hivyo huyu Mzee unaweza kumuangalia kama "Mzee Ruksa" Mwinyi ex president, lakini watu wengine huyu ni mzazi wa rafiki tuliyeishi naye vizuri kwa heshima kubwa.

Hivyo tuangalie hilo pia.

Sio kila kitu siasa.
Mpwa wake nilisoma naye shule moja.....

Mzee Ruksa alikuja shuleni enzi hizo akiwa rais.

Usemayo ni kweli
 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua. Anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali.

Abdullah Ali Mwinyi
Msemaji wa Familia
Mola ampe nafuu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ndugu Abdullal Alli Mwinyi Msemaji wa familia ya Rais mstaafu wa awamu ya pili mzee Mwinyi ameiomba jamii kumkumbuka mzee wetu na Rais wetu mstaafu kwa sara,dua na maombi.

Ambapo amepelekwa hospitalini kutokana na maradhi ya kifua na kuendelea kupatiwa matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari wake.

Kwa hiyo watanzania wenzangu tumuombee mzee wetu na Rais wetu mstaafu ambaye ndiye muasisi wa mageuzi ya kisiasa hapa nchini.

Ni wakati wake ndio mfumo wa vyama vingi uliingia nchini na demokrasia kuanza kuchukua nafasi yake na kutoa nafasi ya watu kuzungumza kwa uhuru bila shida. Ni wakati wake ambapo mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi yalifanyika katika kuwaondoa watanzania katika dimbwi la umaskini uliotopea.

Kwa waliosahau au kutoelewa ni kuwa mzee wetu huyu hapo mwakani panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu atatimiza miaka mia moja yaani karne moja.jambo ambalo kiukweli kufikisha umri huo hapa Duniani ni lazima umshukuru Mungu na kusema imekuwa hivyo kwa neema tu ya Mungu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
sengerema kweli wewe punga wa head
 
Huyo naona ana matatizo ya akili yanayomsumbua ambayo yanahitaji matibabu ya haraka sana.maana mtu mwenye akili Timamu hawezi kuandika ujinga aliouandika.
hana tatizo lolote la akili bali anatimiza wajibu wa kiraia wa kuchangia maoni kwa uhuru

mtu amekuwa Rais wa nchi ya watu milioni 60 miaka 10, unamleta kwenye jukwaa huru la kijamii halafu unategemea kupata mawazo milioni 60 yote ya kumsifia ? Kwa vile aliwafurahisha wote milioni 60 kwa kila jambo kwa miaka 10 ??? hapo ni wewe ndio una matatizo ya akili!

....acheni public figures wajadiliwe kwa namna chanya na hasi, kwa sababu walijiingiza wenyewe kwenye public life

.... hakuna kumjadili, kwa hiyo akivuta pia hakuna kujadili legacy yake ???????
 
On the throne of time death is unavoidable.

Complications za uzeeni ni indicators kwamba muda wowote waweza kuvaa mbawa.
 
Wasanii wajiandae kuingia studio
Ya Mungu mengi, tunaweza kushangaa mzee amerudi mtaani, alafu wewe ndo tunapokea habari zako hapa JF kuwa mwana JF mwenzetu I am Groot hatunae tena duniani.

Kuna muda wagonjwa wanapona wazima wanaondoka, au wazee wanaishi watoto wanakufa.

Mungu amponye na kumpa nguvu mzee wetu 🤲
 
Back
Top Bottom