Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua

Ndiyo umri nitakaofikisha mie,🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Kwa nchi kama yetu ukiona unatangaziwa basi jua unaandaliwa kisaikolojia.

Viongozi wanaugua mara nyingi tu, hakuna matangazo yoyote.
 
Hivi huyu jamaa huwa Kanisa lake liko wapi? Maana huwa anaongea mambo mazito

Mbezi Beach upande wa baharini, karibu na njia ya Whitesands...

Kuna mitaa fulani ina apartments nimesahau jina lake, kanisa lipo hapo pembeni...
 
Mnaitangazia dunia wenyewe kuwa anaumwa halafu tena mnataka faragha!

Mara zingine akiumwa mbona huwa hamtangazi?

Si bora msingetupa taarifa mkauguza kimyakimya tu ndiyo faragha,nani angejua.
 
Taarifa za Jasusi Chahali zina kila uwezekano wa kuwa kweli ; kuna mtu anaogopa wosia wa Mzee kutaka azikwe pembeni ya baba yake mkuranga ukitekelewa atakosa madaraka ….
Sasa Atujui nini kinaendelea kama yuko hai au yuko kwenye friji hadi familia ifike muafaka
Huyu ni mali ya Watanzania , kama alia usia akifa arudishwe MKURANGA .. tafadhali msibadili kwa tamaaa ya madaraka ; atawajia usiku

—/———————————————————

Somo: Situation report (SITREP) kuhusu hali ya Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Usuli wa ripoti:

Majuzi, familia ya Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi ilitoa taarifa kwamba kiongozi huyo wa zamani anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari baada ya kupelekwa Hospitali [haikutajwa] kutokana na kuugua maradhi ya kifua.

Kinachoendelea:

Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi alitoa maagizo huko nyuma kuhusiana na mustakabali wake, na nini familia yake inapaswa kutekeleza.

Hata hivyo, maelekezo hayo yamepelekea mvutano kwa sababu endapo yatazingatiwa, yatakuwa na athari kubwa za kisiasa huko Zanzibar.

Mvutano huo umedumu kwa siku kadhaa sasa na inaelezwa kuwa mmoja wa wanafamilia anayeamini kuwa kutekelezwa kwa matakwa ya Mzee Mwinyi kutakuwa na athari kwake kisiasa, amekataa katakata “kumaliza suala hilo” kinyume na matakwa yake.

Kwa lugha nyingine, ili umma ufahamishwe “kisichoelezwa hadi sasa,” ni pale tu matakwa ya mwanafamilia huyo yatakapotekelezwa japo ni kinyume na matakwa ya Mzee Mwinyi mwenyewe.

“Amesema hata kama itachukua mwaka mzima na iwe hivyo lakini kamwe hatokubali…anahofia matakwa ya Mzee yakitekelezwa, maadui zake wa kisiasa watesema si tuliwaambia huyu mtalii kutokana Bara?” kilieleza chanzo kimoja cha kiintelijensia.

Mustakabali:

Wakati hayo yakiendelea, mamlaka za kiserikali upande wa Muungano na Zanzibar zimekuwa zikipitia wakati mgumu kwa sababu haziwezi kutamka lolote bila idhini ya familia.

Hata hivyo, kuna dalili za “ushindi” kwa mwanafamilia anayetaka matakwa yake yatekelezwe japo ni kinyume na matakwa ya Mzee Mwinyi. Katika hilo, kuna dalili kwa mamlaka za kiserikali za Muungano na Zanzibar kuridhia matakwa ya mwanafamilia huyo muda wowote kuanzia sasa.

Na pindi hili likitokea, wananchi watapewa taarifa ambazo hadi wakati ripoti hii inaandikwa zimekuwa restricted [zimezuiliwa].

Hitimisho:

SITREP ijayo itafafanua zaidi kuhusu yaliyomo kwenye SITREP hii pindi taarifa hiyo ya familia itakapokuwa unrestricted.

ANGALIZO: Ripoti hii imeheshimu haki ya faragha ya familia ya Mzee Mwinyi na ndio maana kuna baadhi ya maelezo hayajawekwa wazi. Hata hivyo, ukweli kwamba Mzee Mwinyi sio tu alikuwa kiongozi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali pia ni kipenzi cha Watanzania wengi ambao pia wana haki ya kufahamishwa kuhusu maendeleo ya kiongozi wao na kipenzi chao, umelazimu kuchapishwa kwa SITREP hii.
 
Kama kilichoandikwa hapa ni kweli, binafsi sioni maana ya hayo madai, ni hofu tu isiyo na msingi wowote.

Mzee pia alishawahi kuwa kiongozi wa JMT, ameishi Bara, mahala pa kuzikwa siku zote ni chaguo la marehemu, haiwezekani na haitakiwi yeyote nje ya marehemu abadilishe huo msimamo.

Hata hayo maneno ya kuogopa kuitwa "mtalii toka Bara" ni siasa tu, ambayo kwangu sioni uzito wake ni kama upepo tu, utapita, kwanza sioni anahofia kitu gani wakati mpini wamekamata wao?!
 
Walishaomba faragha ya mgonjwa lakini hulika sio ya mwafrika watanzania kutoheshimu faragha za watu na kupenda umbea majungu chuki na uchimvi yamepelekea kuleta hiyo tungo tata!
 
kuna kababu ka lidinya mpaka mama mzazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…