Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Mwinyi aliwahi kuitisha Baraza la Mawaziri na kulivunja mbele yao

Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Mwinyi aliwahi kuitisha Baraza la Mawaziri na kulivunja mbele yao

Baada ya kulivunja maendeleo yalipatikana?
Ukiwauliza wale walioambiwa wafunge mikanda miezi kumi na nane ya shida watakupa majibu.. ukiwauliza wale waliokuwa wakitembea kwa miguu ubungo mpaka temeke watakujibu... ukiwauliza ambao waliaminishwa luninga ni anasa hawatokaa kimya... ukiwauliza waliokimbizana na gari za ugawaji kisa nusu kilo ya dona la yanga na kibaba cha maharagwe hakika hawatonyamaa... usiishie waliovaa viraka na katambuga za kuwa mtoko... watakueleza kama kulipatikana maendeleo ama laa!!
 
Singida, Dom, Tabora, Shinyanga n.k mbona bado kuna nyumba za tembe/nyasi?
Sawa. Sio kwamba yeye ndio alikuja kumaliza zote kwa mkupuo. Kwingine wapi zilikuwepo? Na hazipo tena,badala kuna nyumba za bati?. Hayo ndio maendeleo
 
Singida, Dom, Tabora, Shinyanga n.k mbona bado kuna nyumba za tembe/nyasi?
Walioahidi kuziondoa tembe na nyumba za nyasi bado ni walewale na ndio haohao wanaoahidi kushuka kwa bei za umeme na saruji....
Mzee Ruksa aliikuta nchi iko uchi.. baada ya kufilisiwa na "vita" pasipo kusahau "manyang'au" yaliyokuwa yamemzunguuka Mwalimu.
#Katiba mpya ndio suluhisho la sera na maendeleo...
 
Bwashee una kumbukumbu nzuri sana.

cc: Pascal Mayalla na mrangi
Mkuu ukiangalia kwa makini, utagundua kwamba mabaya mengi ya kuuwa uchumi aliyoyafanya mtangulizi wake msalaba wote alibebeshwa Mwinyi, na yale mazuri yote aliyoyafanya Mwinyi kuwaletea wananchi wake maendeleo alipewa Mkapa. Ndio maana leo ni kawaida kusikia mtu au kijana aliezaliwa miaka ya 90 anakwambia kwamba Mwinyi ktk utawala wake hajafanya kitu
 
Kazi yake ilikuwa NDOGO SANA YAANI "KILA KITU RUKSA"....
Kama kazi ilikuwa ndogo kwa nini mtangulizi wake alishindwa mpaka tukawa tunatembea matako nje,vifo vingi vya watoto kwa ajili ya utapiamlo,kukimbizana na magari ya maiti(trekta)tukifikiri ni magari ya ugawaji nk?
 
Umesahau moja; Television( Tuliita video) nazo zikaruhusiwa kuingia nchini maana kabla, wengi walikuwa wanazisikia tu kwenye stori za vijiweni.
Sisi walalahoi picha tulikuwa tunaenda kuangalia Drive in Cinema tulikuwa tunaangalia kibubububu huku tukipigwa na baridi na tulikuwa tukiludi home usiku kwa mchakamchaka sisi ndio tuliokuwa tunaishi mjini sijui hao wa vijijini ilikuwaje?
 
Baada ya kulivunja maendeleo yalipatikana kwa kufufua uchumi uliokufa enzi za mtangulizi wake. Bidhaa dukani zilijaa kama vile unga, sukari, mchele, ngano, mafuta ya taa na ya kupikia, sabuni za kuogea na kufulia. Maduka makubwa nayo hayakuwa nyuma watu wakaanza kuingiza TV, Redio na vitu mbali mbali vinavyotumia umeme. Pia magari ya kila aina yakaanza kuingia kwa wingi yakiwemo mabasi ya abiria, barabara zikapanuliwa kutokana na mahitaji ya kipindi kile, moja ya barabara na alama aliyoacha Mwinyi ni hii ya morogoro road ambapo lile daraja la manzese lilijengwa wakati wa utawala wake, shule za serikali ziliongezeka, na za binafsi pia zikajengwa kwa wingi, nguo za mitumba na dukani zikaanza kuingia kwa wingi hata ww leo unavaa kiatu kizuri, jinsi zuri na unaenda kunyoa salon kwa mashine, hizo ni juhudi za Mwinyi ktk kuwaletea maendeleo raia wake. hapo sijataja hospital nyingi za serikali na private zilizojengwa kwa wingi chini ya utawala wake including madawa nk. Hakika Mwinyi ameifanyia mengi ya kiutu nchi hii, na alikuwa na uwezo wa kuthubutu bila kujali nani anasema nini.
Akajiita "Mtukufu Rais".

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo. Tulianza kununua na TV kuona kinachoendelea duniani ikiwemo Ligi ya Uingereza. Nayo hayop ni maendeleo. Tatizo mmekaririshwa na mwendazake kwamba maendeleo ni Flyovers za Ubungo kumbe hata uhuru wa mawazo na uhuru wa kujieleza ni maendeleo. Mwendazake ameliharibu Taifa na kupandkiza roho mbaya kwa wengi sana!
Hata lile Daraja la Manzese(Msufini)kipindi linajengwa na upanuzi wa ile barabara ya Morogoro yalikuwa ni maendeleo makubwa na yamfano kwa kipindi hicho
 
Sisi walalahoi picha tulikuwa tunaenda kuangalia Drive in Cinema tulikuwa tunaangalia kibubububu huku tukipigwa na baridi na tulikuwa tukiludi home usiku kwa mchakamchaka sisi ndio tuliokuwa tunaishi mjini sijui hao wa vijijini ilikuwaje?
Kasesela alikuwa hakosekani hapo Drive in na alikuwa na tofali lake ambalo hakalii mtu mwingine!
 
Baada ya kulivunja maendeleo yalipatikana kwa kufufua uchumi uliokufa enzi za mtangulizi wake. Bidhaa dukani zilijaa kama vile unga, sukari, mchele, ngano, mafuta ya taa na ya kupikia, sabuni za kuogea na kufulia. Maduka makubwa nayo hayakuwa nyuma watu wakaanza kuingiza TV, Redio na vitu mbali mbali vinavyotumia umeme. Pia magari ya kila aina yakaanza kuingia kwa wingi yakiwemo mabasi ya abiria, barabara zikapanuliwa kutokana na mahitaji ya kipindi kile, moja ya barabara na alama aliyoacha Mwinyi ni hii ya morogoro road ambapo lile daraja la manzese lilijengwa wakati wa utawala wake, shule za serikali ziliongezeka, na za binafsi pia zikajengwa kwa wingi, nguo za mitumba na dukani zikaanza kuingia kwa wingi hata ww leo unavaa kiatu kizuri, jinsi zuri na unaenda kunyoa salon kwa mashine, hizo ni juhudi za Mwinyi ktk kuwaletea maendeleo raia wake. hapo sijataja hospital nyingi za serikali na private zilizojengwa kwa wingi chini ya utawala wake including madawa nk. Hakika Mwinyi ameifanyia mengi ya kiutu nchi hii, na alikuwa na uwezo wa kuthubutu bila kujali nani anasema nini.
Dudumizi, ulikuwa na umri gani wakati huo??

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Inawezekanaje boss wa bunge awe na hofu wakati anapigiwa kura na bunge? Nilidhani ambaye anaweza kuwa na hofu ni boss wa Mawaziri kwa kuwa jina lazima litoke kwa boss wa Nchi

By the way kila la kheri Mama kwenye kupewa mikoba ya Chama
Heeeeee!!!,Boss wa chama anaweza kumkataa bosi wa Bunge jina lake likatupiliwa mbali kabla ya kupelekwa Bungeni.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Mama anaweza kufanya hivyo ama asifanye kulingana na mahitaji ya timu anayoitaka ktk uongozi wake na si vinginevyo.
 
Kasesela alikuwa hakosekani hapo Drive in na alikuwa na tofali lake ambalo hakalii mtu mwingine!
Kipindi hicho tulikuwa tunaongopeana tu huyu anaitwa Wan yu miluzi,Bruce mawani,Bruce kijeba, aisee kwa kweli tukikumbuka shida tulizokuwa tunapata kipindi kile halafu anakuja mtoto wa miaka ya90 anamtukana(mdhalau) Mzee Mwinyi unatamani kumchapa kibao
 
Heeeeee!!!,Boss wa chama anaweza kumkataa bosi wa Bunge jina lake likatupiliwa mbali kabla ya kupelekwa Bungeni.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Nilikuwa sijui boss, but shukrani kwa clarifications zako.

Kumbe ndiyo maana Mwl Nyerere alibaki na Uenyekiti wa Chama wakati Mwinyi ndiyo Rais, kumbe Mwenyekiti wa Chama ananguvu kuliko Rais wa Nchi🙌
 
Back
Top Bottom