Alimpachika pale kwa lengo la kumshikia akili, amwambie Mwinyi fanya hivi au fanya vile nk. kumbuka moyo wa mtu msitu kwahiyo Mwinyi ukimuona kwa macho anaonekana ni mpole, lkn anachokiwaza akilini kwake hauwezi kukijua. Baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa CCM na nchi ikiwa chini ya mikono yake hapo ndo alipoanza kuonesha kuwa anaweza kufanya chochote mwenyew bila kushikiwa akili na mtu yoyote. Akaanza kwa kuufufua uchumi uliokufa enzi za mtangulizi wake, akaruhusu vitu viingie na vingine vitoke ili nchi iweze kupata hela za kigeni. Pesa ikawa nyingi mtaan hadi wauza kahawa, wachoma mahindi, wauza machungwa, mamantilie mitaani wakaanza kununua viwanja na kujenga sehem mbali mbali, mji ukapanuka, biashara zikawa nyingi, zahanati, mahospital, na maduka ya kuuza madawa yakawa mengi. I mean neema ikawa kubwa hata mtangulizi akapata tumbo joto la kupoteza heshima na legacy yake. Ndo hapo sasa akaanza kutupa madongo ya lawama kwa Mwinyi ili kujaribu kumfunga paka kengele, lkn Mwinyi alipuuza yale aliyoona hayana manufaa kwa taifa na kufanya yale aliyoona binafsi yana manufaa kwa taifa. Mema aliyofanya Mwinyi ktk nchi hii mengi ndugu nikisema niyataje siwezi kuyamaliza hapa. Kifupi huu mfumo unaoongoza leo pamoja na maendeleo muasisi wake ni Mwinyi
Vijana wa juzi hawajui hili mkuu. Sisi tuliokuepo tunayakumbuka haya. Mzee mtulivu, mwenye subra na hekma.
Tena huyu baba alikuwa bingwa wa demokrasia, hakuogopa kukosolewa. Baba huyu aliruhusu vyama vingi 1992, pamoja na kwamba wananchi walipiga kura ya hapana. Waziri wake wa mambo ya ndani ( Augustine Lyatonga Mrema) aliingia upinzani na akawa anamkosoa haswa, lakini Mzee Mwinyi kept cool and calm.
Halafu hata Kikwete nakumbuka aliwahi kuwa waziri wake wa fedha. Nakumbuka anaingia na ile briefcase yenye budget bungeni anacheeeka, baadae alkuja kuwa Raisi mzuri sana. Alifundwa na Mwinyi. Kikwete alkua baba wa democracy, hakuogopa kukosolewa na alipenda watu wake waishi vizuri.
Mama Samia pia anaenda vizuri. Mama ni hustler, fighter, ana exposure. Mama Samia anaufahamu maisha halisi ya mtanzania, wa chini mpaka wa juu maana kayaishi. Anafahamu tumetoka wapi.
Hakika huu SASA ndo mpango wa Mungu, mama Samia atafanya wonders.
Namwombea ujasiri wa kulivunja bunge. Hii itamsaidia kupata watu sahihi wa kufanya nae KAZI KWA utii na uaminifu. Akifanikiwa kumaliza hii miradi ya hayati JPM (KWA utaratibu lakini), huku akiratibu MIPANGO ya maisha Bora KWA watu wake, atajijengea Legacy kubwa Sana.
Akimaliza awamu yake, Mungu akitupa Mwinyi Jr. Tutakua tumeula.
Nina imani Sana na Mama Samia na Mwinyi II