Rais wa JMT akemea makundi yanayodai ufisadi umerudi. Je, ni makundi gani?

Rais wa JMT akemea makundi yanayodai ufisadi umerudi. Je, ni makundi gani?

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
"Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya serikali, na yanageuka kusema serikali ya awamu ya 6 ufisadi umerudi mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo, mambo hayo yalifanyika huko nyuma, gari bovu linaangushiwa awamu ya 6 sitakubali.

IMG_20211204_132254.jpg
 
Sasa kama wako hovyo mbona anawaacha tu waendelee kufanya mambo ya hovyo?

Maana kama wako hovyo halafu hawako kwenye utumishi, shida iko wapi?

Kama wako hovyo, badala ya kulalamika, awapige chini. Wananchi walalamike na rais naye alalamike? Mantiki ya uongozi inapotelea mbali.
 
"Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya Serikali, ni makundi hayohayo yanageuka kusema Serikali ya Awamu ya Sita ufisadi umerudi, mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo na mambo yale hayakufanyika ndani ya Awamu ya Sita, yalifanyika huko nyuma gari bovu linaangushiwa Awamu ya Sita, sitakubali, sitakubali, niliapa kusimamia haki za Wananchi nitasimama nao nitasimama kutetea haki za Wananchi sitakubali"———Rais Samia akizindua maboresho ya gati (0-7) Bandari ya Dar es salaaam.

My Take
Au hayo makundi ya hovyo yafungulie kesi ya ugaidi 🤣🤣🤣
 
"Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya Serikali, ni makundi hayohayo yanageuka kusema Serikali ya Awamu ya Sita ufisadi umerudi, mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo na mambo yale hayakufanyika ndani ya Awamu ya Sita, yalifanyika huko nyuma gari bovu linaangushiwa Awamu ya Sita, sitakubali, sitakubali, niliapa kusimamia haki za Wananchi nitasimama nao nitasimama kutetea haki za Wananchi sitakubali"———Rais Samia akizindua maboresho ya gati (0-7) Bandari ya Dar es salaaam
🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔😂😂😂😂😂
 
Bibi tozo usituchoshe. Hatutaki drama.

Umetubomolea vibanda wamachinga — Kwanza nina hasira sana na wewe. Kaa kimya na ushungi wako.

Bei za bidhaa ziko juu, gesi juu, mafuta juu, sukari juu.

Umeme wa mgao, maji tabu, umeua miradi ya umeme... Bwawa la Nyerere etc. Tozo kila mahali.

Umetuletea machanjo ya ajabu ajabu. YAANI WEWEEE.... i wish niku....
 
Kwanini asiyashughulikie hayo makundi akiwa kama mkuu wa serikali na mwenyekiti wa chama chake? analalamika kwa nani? alituambia yeye ndie Rais mwenye jinsia ya kike au ameshasahau?

Rais atambue kuacha miradi mikubwa ya mtangulizi wake kabla haijamalizika huku nae anaibuka na miradi yake ya gharama kubwa mpaka $30 bil. ni dalili za ufisadi, hizo pesa watazitoa wapi? watazirudisha vipi? anatakiwa kujibu haya maswali asihangaike na watu wanaotoa maoni yao.

Na hizo haki za wananchi anazoapa kuzisimamia ni zipi? kule magereza wapo waliobambikiwa kesi huku kila siku jamhuri wakishirikiana na jaji wanatoa ushahidi wa aibu ili kuhakikisha washtakiwa wanafungwa bila hatia, haya yanatokea kwenye awamu yake ya sita, asikwepe kitu.

Rais ajue haki za wananchi ni pamoja na wapinzani, nao ni watanzania wanastahili kuishi kwa amani ndani ya nchi yao, asichague wa kuwapa haki na wengine awanyime kwa sababu za kisiasa, ajue dhamana aliyokabidhiwa kuwatumikia watanzania na aisimamie vizuri bila ubaguzi wowote, maneno matupu bila vitendo hayana maana.
 
"Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya Serikali, ni makundi hayohayo yanageuka kusema Serikali ya Awamu ya Sita ufisadi umerudi, mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo na mambo yale hayakufanyika ndani ya Awamu ya Sita, yalifanyika huko nyuma gari bovu linaangushiwa Awamu ya Sita, sitakubali, sitakubali, niliapa kusimamia haki za Wananchi nitasimama nao nitasimama kutetea haki za Wananchi sitakubali"———Rais Samia akizindua maboresho ya gati (0-7) Bandari ya Dar es salaaam
Kama anawajua hao watu wa hovyo na mafisadi, why asiwashughulikie badala yake anahangaika na Mbowe?
Rais analalamika, wananchi wanalalamika! Nchi ngumu sana hii aisee.
 
"Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya serikali, na yanageuka kusema serikali ya awamu ya 6 ufisadi umerudi mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo, mambo hayo yalifanyika huko nyuma, gari bovu linaangushiwa awamu ya 6 sitakubali"@SuluhuSamia Bandarini Leo https://t.co/2LreQmIlmkView attachment 2032536
MAMA JITAMBUE WEWE NI RAISI. KAULI ZA KIKE ZA KUCHAMBANA ACHANA NAZO. HAO UNAOWASEMA NI WANA CCM WENZAKO ITANENI KWENYE VIKAO VYENU VYA CHAMA MUONYANE.

KUMBUKA JPM ALITUKANWA NA KUNDI NDANI YA CCM [KIGOGO] MPAKA ANAKUFA. HIVYO HUWEZI KULAZIMISHA WATU WOTE NDANI YA CHAMA CHENU KUKUPENDA.
 
Inaonekana hayo Makundi yana nguvu kuliko Rais! Kama Mwendazake hakuyagusa,yatampa shida Mama.
 
Back
Top Bottom