Kwanini asiyashughulikie hayo makundi akiwa kama mkuu wa serikali na mwenyekiti wa chama chake? analalamika kwa nani? alituambia yeye ndie Rais mwenye jinsia ya kike au ameshasahau?
Rais atambue kuacha miradi mikubwa ya mtangulizi wake kabla haijamalizika huku nae anaibuka na miradi yake ya gharama kubwa mpaka $30 bil. ni dalili za ufisadi, hizo pesa watazitoa wapi? watazirudisha vipi? anatakiwa kujibu haya maswali asihangaike na watu wanaotoa maoni yao.
Na hizo haki za wananchi anazoapa kuzisimamia ni zipi? kule magereza wapo waliobambikiwa kesi huku kila siku jamhuri wakishirikiana na jaji wanatoa ushahidi wa aibu ili kuhakikisha washtakiwa wanafungwa bila hatia, haya yanatokea kwenye awamu yake ya sita, asikwepe kitu.
Rais ajue haki za wananchi ni pamoja na wapinzani, nao ni watanzania wanastahili kuishi kwa amani ndani ya nchi yao, asichague wa kuwapa haki na wengine awanyime kwa sababu za kisiasa, ajue dhamana aliyokabidhiwa kuwatumikia watanzania na aisimamie vizuri bila ubaguzi wowote, maneno matupu bila vitendo hayana maana.