Rais wa JMT akemea makundi yanayodai ufisadi umerudi. Je, ni makundi gani?

Rais wa JMT akemea makundi yanayodai ufisadi umerudi. Je, ni makundi gani?

Kwanini asiyashughulikie hayo makundi akiwa kama mkuu wa serikali na mwenyekiti wa chama chake? analalamika kwa nani? alituambia yeye ndie Rais mwenye jinsia ya kike au ameshasahau?

Rais atambue kuacha miradi mikubwa ya mtangulizi wake kabla haijamalizika huku nae anaibuka na miradi yake ya gharama kubwa mpaka $30 bil. ni dalili za ufisadi, hizo pesa watazitoa wapi? watazirudisha vipi? anatakiwa kujibu haya maswali asihangaike na watu wanaotoa maoni yao.

Na hizo haki za wananchi anazoapa kuzisimamia ni zipi? kule magereza wapo waliobambikiwa kesi huku kila siku jamhuri wakishirikiana na jaji wanatoa ushahidi wa aibu ili kuhakikisha washtakiwa wanafungwa bila hatia, haya yanatokea kwenye awamu yake ya sita, asikwepe kitu.

Rais ajue haki za wananchi ni pamoja na wapinzani, nao ni watanzania wanastahili kuishi kwa amani ndani ya nchi yao, asichague wa kuwapa haki na wengine awanyime kwa sababu za kisiasa, ajue dhamana aliyokabidhiwa kuwatumikia watanzania na aisimamie vizuri bila ubaguzi wowote, maneno matupu bila vitendo hayana maana.
Kama ameona jinsia ya kike haimsaidii abadilishe.
 
Bibi tozo usituchoshe. Hatutaki drama.

Umetubomolea vibanda wamachinga — Kwanza nina hasira sana na wewe. Kaa kimya na ushungi wako.

Bei za bidhaa ziko juu, gesi juu, mafuta juu, sukari juu.

Umeme wa mgao, maji tabu, umeua miradi wa umeme... Bwawa la Nyerere etc. Tozo kila mahali.

Umetuletea machanjo ya ajabu ajabu. YAANI WEWEEE.... i wish niku....
Kibanda ulichojenga nani alikupa ruhusa ya kukijenga?. Gwaride la kawaida tu, ni mwengo wa mguu sawa.
 
Watakuwa Sukumagang na ChaGadema tu.....Mama Samia Watimue na wakae jela wasikusumbue
 
"Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya serikali, na yanageuka kusema serikali ya awamu ya 6 ufisadi umerudi mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo, mambo hayo yalifanyika huko nyuma, gari bovu linaangushiwa awamu ya 6 sitakubali"@SuluhuSamia Bandarini Leo https://t.co/2LreQmIlmkView attachment 2032536
Anakemea ufisadi au anakemea wanaomtaarifu kwamba ufisadi umerejea? Hapo tuwekane sawa

Ufisadi awamu ya sita umeongezeka mara mia tano zaidi ya awamu zote huku wenye nacho wakineemeka na maskini kuzidi kuisoma namba
 
Hivi kweli unamteua MaRope kama waziri kwanini tusikuhisi vibaya,
 
Mama tumuombee adumu, amalize kipindi hiki na kile cha 2025. Alichokosea kabisa ni kudhani mfumo wa Dkt Magufuli ulikuwa mbaya. Alipaswa atembelee hiyo nyota japo kwa mwaka ili kupata somo. Ila kama kuna watu walimuua Dkt Magufuli na yeye wakamnyetishia kuwa asipotekeleza ya hao mafisadi watamuondoa basi kazi ipo. Ila Mama hana tamaa kabisa, ni mzalendo ila shida mifumo inakinzana. Angekubali kuendelea na mfumo wa Dkt Magufuli yaani mpaka sasa angakuwa hero.
Hili lipo na linawezekana,ila subiri 2024 tukikaribia uchaguzi JPM ataimbwa sana na tutaenda sana ziara chato

Si inajua uchaguzi bila machinga hauendi.
 
MaCHADEMA yatake yasitake mama tunamuongezea muda
 
Kibanda ulichojenga nani alikupa ruhusa ya kukijenga?. Gwaride la kawaida tu, ni mwengo wa mguu sawa.
Kwahiyo nikale wapi?

Anipe ajira basi!

Watu tunapambana kutafuta kuendesha maisha yeye anatuma migambo kutubomolea biashara zetu?
 
Bibi tozo usituchoshe. Hatutaki drama.

Umetubomolea vibanda wamachinga — Kwanza nina hasira sana na wewe. Kaa kimya na ushungi wako.

Bei za bidhaa ziko juu, gesi juu, mafuta juu, sukari juu.

Umeme wa mgao, maji tabu, umeua miradi ya umeme... Bwawa la Nyerere etc. Tozo kila mahali.

Umetuletea machanjo ya ajabu ajabu. YAANI WEWEEE.... i wish niku....
Hayo pia atasema ameyarithi anafikiri Watanzania hawakuwepo kwenye hizo awamu.

Labda anaongelea awamu ya Msoga.
 
Back
Top Bottom