Kuna mtu alisema barabara inayoanzia Ubungo mataa hadi Mwenge inaitwa Sam Nujoma ukazuka ubishi mkali wa kufa mtu, wakamuuliza wewe unayebisha tupe jina la barabara hiyo akasema inaitwa Sir Mwinyi Juma 🀣🀣
Usikute ukaendelea kubishana nae πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mzalendo mwendo ameumaliza!
 
Apumzike kwa Amani
 
Aliyekuwa Rais wa kwanza wa Namibia Sam Nujoma amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95

Sam Nujoma aliongoza mapambano ya kupigania Uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa utawala wa Afrika Kusini mwaka 1990

Baada ya Uhuru alichaguliwa kuwa Rais na kudumu hadi mwaka 2005 ambapo aliamua kustaafu ila alibaki kuongoza Chama cha South West Africa People's Organisation (SWAPO) hadi mwaka 2007
 
Huyu Mwamba alitembelea Tanzania muda mfupi baada ya Namibia kupata uhuru mwaka 1990, ndipo kipande cha barabara ya Port Access kutoka ubungo kuelekea Mikocheni kikapewa jina la Sam Nujoma Road, na kuanzia ubungo hai bandarini kikaitwa Nelson Mandela Rd
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…