TANZIA Rais wa kwanza wa Namibia Sam Nujoma amefariki akiwa na umri wa miaka 95
Kama kawaida kaanza yeye ila mkewe bado yupo daah ila pumziko jema mwamba na barabara yenye jina lako leo iwekwe bendera nyekundu
 
Apumzike kwa Amani.

Nakumbuka tulivyosota naye katika mapori ya kule Itumbi-Chunya, kipindi hicho Namibia ndiyo inajitafuta kupata Uhuru wake.

 
Ila mke wake yupo?? wa nyerere yupo wa mkapa yupo wa magu yupo yule wa zanzibar yupo WANAUME TUNAKOSEA WAPI,,,??
 
Heri yako Sam Nujoma, umevipiga vita mwendo umeumaliza.

Huku kwetu wastaafu wa Rais hawakai, pengine Mzee Mwinyi tu

Msalimie Mwalimu Julius Kambarage Nyerere , tell him how we missed him
 
Kuna njema moja katikati ya Chalinze na Lugoba ... mbishi sn kufa ikibidi Allah fanya maajabu..
 
🫡🫡🫡🫡🫡 kwaheri mpigania UHURU.
 
Sam Nujoma, aliyekuwa rais wa kwanza wa Namibia, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Alikuwa shujaa wa ukombozi ambaye aliongoza Namibia kupata uhuru kutoka kwa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini mwaka 1990, na alihudumu kama rais kwa miaka kumi na tano.

Kifo chake kilitangazwa na Rais wa sasa wa Namibia, Nangolo Mbumba, ambaye alisema Nujoma alifariki dunia usiku wa Jumamosi baada ya kulazwa hospitalini Windhoek. Nujoma alikuwa kiongozi muhimu katika harakati za ukombozi wa Afrika, akijiunga na viongozi kama Nelson Mandela, Robert Mugabe, Kenneth Kaunda, na Samora Machel.

Alitumia takriban miaka 30 uhamishoni akiongoza harakati za uhuru kabla ya kurejea na kuchaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Namibia mwaka 1990. Alianzisha mapambano ya silaha kupinga utawala wa Afrika Kusini baada ya taifa hilo kupuuza azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1966 la kumaliza mamlaka yake juu ya eneo la zamani la Ujerumani la Afrika Kusini Magharibi.

Nujoma alizaliwa katika familia maskini ya kijijini na alishiriki katika siasa akiwa kijana. Alianzisha Chama cha Watu wa Afrika Kusini Magharibi (SWAPO) mwaka 1960 na aliongoza harakati za ukombozi kutoka uhamishoni. Alipata msaada kutoka kwa nchi kama Tanzania, Algeria, Cuba, Urusi, na China. Alikuwa kielelezo muhimu katika historia ya Namibia, akiongoza taifa hilo kupitia mchakato wa uponyaji na upatanisho baada ya vita vya uhuru na sera za ubaguzi wa rangi za Afrika Kusini. Kama mmoja wa waanzilishi wa SWAPO, Nujoma alipigania uhuru wa Namibia kutoka kwa makaburu wa Afrika Kusini iliyokuwa inaendeshwa kwa kufuata siasa za ubaguzi wa rangi.

Katika harakati zake, alipata ushirikiano na msaada kutoka nchi mbalimbali za Afrika, ikiwemo Tanzania, ambayo ilikuwa kitovu cha harakati za ukombozi kusini mwa Afrika. Tanzania ilitoa mafunzo, makazi, na msaada wa kisiasa kwa wapiganaji wa SWAPO. Kifo chake kimeacha pengo kubwa, lakini urithi wake kama baba wa taifa na shujaa wa ukombozi utaendelea kuenziwa na Namibia na Waafrika wote. Alifariki akiwa hospitalini kutokana na matatizo ya kiafya, na taifa la Namibia limetangaza kipindi cha maombolezo kumuenzi.
 
Ila mke wake yupo?? wa nyerere yupo wa mkapa yupo wa magu yupo yule wa zanzibar yupo WANAUME TUNAKOSEA WAPI,,,??
kiongozi haujui hao ndo wanaombea tutangulie? au kikao cha mwisho hukuwepo?
 
Back
Top Bottom