Mzee Ali Hasssan Mwinyi hakuwa na asili ya Zanzibar, si kwa mama wala kwa baba. Kwao ni Mkuranga na alipelekwa Unguja kusoma tu.
Mama Samia Suluhu Hassa ana asili ya kuzaliwa Zanzibar na wazazi wake wote kuzaliwa Zanzibar.
Ma shaa Allah, ukiisoma historia yake utaona kuwa kila sehemu ya kazi aliyopitia aliifanya kwa uadilifu, uaminifu na welesi mkubwa na kuwa anapanda tu vyeo, mpaka akafikia kuwa Makamo wa Rais na ahatimae sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alitia fora na alionesha umahiri mkubwa alipokuwa naibu Spika kwenye bunge la Katiba mpya ambalo lilikuwa kivutio kikubwa cha malumbano kwa wakati ule wa Kikwete. Hapo ndipo mama Samia Suluhu Hassan akapata kujulikana.
Naam, hakuna amabae alikuwepo wakati huo na hakumuona umahiri wake. Wengi wakawa wanajiuliza, nani huyu mwanamke?
Leo hakuna asiyemjuwa Tanzania hii na duniani kuwa ni Rais wakwanza Mwanamke Mzanzibari anaeiongoza Tanzania kwa umahiri mkubwa sana.
R zake nne anaziishi na hatetereki.
Mwenyezi Mungu amzidishie hekima na weledi atuongoze daima, akiwepo kwenye Uris na atapomaliza muda wake aendelee kutuongoza kwa hekima zake, kama afanyavyo Kikwete hivi sasa.
Mama Samia tunakuomba mapema uchaguzi mkuu utakapokwisha na panapo majaaliwa basi uhakikishe katiba inabadilishwa na Zaznzibar inajitawala yenye ili tusiwe kama mazayuni.
Watanganyika hatuna sababu ya kuitawala Zanzibar bali tuna kila sababu ya Zanzibar kurudisha utawala wake ulioondoshwa na wakoloni wa Kijerumani ili wapate kuiba vozuri mali za ardhi ya Zenjbar kihistoria.