Wananchi ni watu wazima....
Katiba ndiyo DIRA ya kila aina ya utata....
Ndiyo maana ukaitwa msahafu...HISIA HAZIWEZI ZIKAWA JUU YA UHALISIA KATIKA MAISHA YAENDELEAYO....
Hatuwezi kuishi ndotoni....JPM is no more...haijalishi tulimpenda vipi....kumpenda kwake ni KUYAISHI yale mazuri aliyotufanyia....na hatutakiwi kumuishi peke yake bali mazuri ya Marais wote waliopita tokea kwa baba wa Taifa hayati JKN.....
Nchi ipo....
Itakuwepo hata baada ya vitukuu vyetu na marais wao .....
#NchiKwanza
#SiempreJMT
Nilichokuwa naongea ni ufafanuzi wa hoja kuelezea juu ya hali ya utulivu hasa wa kisaikolojia na utawala kutokuwepo. Hii haimaanishi kuwa haya hayatokwisha. Yataisha ila ni kawaida ya binadamu. Hata nyumbani wazazi wanapofariki hali ya sintofahamu utokea, na baadae hali uwa sawa.
Kuhusu katiba ndugu yangu, katiba si jambo linaloleta maendeleo. Unaweza ukawa huna katiba bado ukapata maendeleo. Nchi nyingi za mashariki ya kati hazina Katiba lakini zimeendelea. Angalia tu huko Dubai. Waingereza hawana katiba iliyoandikwa lkn wameendelea.
Zamani hata wazee wetu hawakuwa na katiba lakini waliishi kwa kuwa na uongozi imara.
Kikubwa ni kupata viongozi weye nia njema ya kuleta maendeleo katika nchi, walio wazalendo. Kwani hii katiba tulionayo kuna sehemu inazuia maendeleo? Hakuna, shida tuna viongozi waliojaa tamaa na wabinafsi, Hii haijalishi wako chama tawala au wako Upinzani.
Pia demokrasia haitokaa ituletee maendeleo, wazungu wametutega nasi tumeingia bichwa bichwa. Angalia nchi zote zilizoendelea duniani pamoja na hiyo marekani, hazikuendelea kwa mfumo wa demokrasia. Marekani yenyewe wanawake wameanza kuruhusiwa kupiga kura miaka ya 60, wakati uhuru walipata toka karne ya 18.
Sweden ilikuwa nchi ya utawala wa Mfalme ambae alikuwa mkorofi na tunaweza mwita dikiteta, alilazimisha wananchi wake kulipa kodi, mambo mengi aliamua yeye mwenyewe. Lakini leo ukienda Sweden wanamuona ndo Baba wa Taifa lao, wanasema japo alikuwa dikiteta lakini aliwapa maendeleo, hawamsemi vibaya, na alipenda vita.
Dubai, mtawala wake wa kwanza aliota ndoto na kuanza kuijenga, hawana cha balaza la mawaziri. Alipofariki, mrithi wake akasema atatimiza ndoto ya aliepita kwanza, akimaliza anaanza naye anavyotaka dubai iwe. Angalia China, Ujerumani, Urusi na nyingi nyinginezo ulikuwa ni udikiteta ndo umeleta maendeleo.
Mfano tu angalia Zanzibar, Yale majengo ya Michenzani na kwingineko huko shamba, mabomba ya maji wao wanaita mifereji na barabara kwenda shamba, haya yote yalifanyika kipindi cha hayati Karume. Unaambiwa yeye hakuwa msomi ila alikuwa katoka nje, alisafiri akifanya kazi ktk meli, akaona dunia ilivyo. Alipokuwa Rais alikuwa anatamka tu, jenga hiki hivyo hayo majengo yalijengwa hata bila ramani yaani alitamka ujenzi ukaanza hata nae alishiriki katika ujenzi. Alieneza maji vijijini, na kujenga barabara. Haya yote alitamka na ikafanyika.
Nambie na demokrasia yetu, ni Rais gani wa Zanzibar kaweza fanya alofanya Karume.
Huyu Karume Mungu angeendelea muweka Zanzibar ingekuwa mbali, alikuwa kiongozi mwenye maono na maamuzi. Hiki ndo kinatakiwa. Wala hakuwa hawa wanasiasa wanaoilalamikia Bara kuwa inainyonya Zanzibar. Yeye alifanya. Na Zanzibar ilipiga hatua, Zanzibar ilikuwa ya kwanza kuwa na Television ya rangi Africa. Hii yote ni Karume.
Viongozi wa leo wamejawa tu na ubinafsi na tamaa za madaraka na kujitajirisha ila hawana maono na uzalendo. Wanabaki kusingizia mara katiba mara muungano.