Rais wa Nchi anapofariki akiwa madarakani Nchi huwa katika nyakati za hatari zaidi kuliko wakati wowote ule

Rais wa Nchi anapofariki akiwa madarakani Nchi huwa katika nyakati za hatari zaidi kuliko wakati wowote ule

Huoni yeye kutangaza nia ili hali amekataza wengine wasiinue vichwa inaleta mkanganyiko kwamba kawekwa hapo kwa maslahi ya watu fulani?
CCM ina ada na kawaida zake....

Ni utamaduni wa kumuachia nafasi aliyepo madarakani.......

Mh.Rais SSH alikuwa VP na Sasa ni Rais kikatiba....atakuwaje hapo nje ya maslahi ya taifa?!!! 😳😳

Amefanya vyema KUKITULIZA CHAMA DHIDI YA MINYUKANO YA KUWANIA MADARAKA.....

#SiempreJMT
 
Uwenda watu wengi hawajuwi na huwenda wengi tunafikiri baada ya Rais wa Taifa kufa basi wakisha fukia na kupiga mizinga basi kazi imeisha. Na sasa kila mtu anaona kuna fursa basi aanze kupiga tarumbeta zake..
Jibu ni hapana.
Rais yeyote wa taifa anapo fariki Taifa huwekwa ktk hali ya hatari kwa kipindi kisicho julikana. Wakati huwo team ya watu maalumu inayo undwa na maofisa wa idara nyeti za usalama huwingia kazini na kuanza kutafuta tarifa nyeti na nzito ambazo hata yule alie kaimu huwenda hajuwi... Team hii ya makachero maalumu huwa na makachero maalumu kutoka idara nyeti za mataifa rafiki kufuwatilia sababu za kifo za Rais alie kuwa madarakani.
Kipindi chote cha upelelezi team hii ugawanyika ktk makundi yasiojulikana kuhakikisha yeyote alie ktk kikundi kile hatowi wala kuvujisha taarifa za siri kwa mtu au kikundi chochote. Nikipindi cha hatari na dhahima kwa yeyote anaye waingilia makachero hawa.
Nikipindi ambacho kama upo smart utasikia taarifa za vifo vya top government officer silence pasipo sababu zinajulikana ila moja wapo ni natural death. Alilala hakuamka, alikuwa kikao akasema hajisikii vizuri au covid19.

Niwakati wale walikuwa wandani wa Rais alie kufa hupita nyakati ngumu na mara nyingi kifo na uzima ubaki mikononi ya team inafuwatilia kifo cha rais. Sio wakati hata kama umepata nafasi ya juu sana unapaswa kuonyesha una hatamia au unaona kwako ni fursa maana unaweza kuwa mchawi pasipokujuwa mchawi na mwisho ukaingia ktk report ya siri ya usalama wa Taifa.
Labda niseme hapa kidogo ktk Taifa lolote lenye mifumo imara ya ulinzi hasa idara hii ya usalama wa Taifa nivigumu sana Rais wa nchi kuwa huru kama vile unasikia. Idara hii nyeti ya Taifa lolote huwa ni idara inayo angalia zaidi masilahi mapana ya Taifa na mara nyingi kama Rais wa taifa akienda kinyume na taratibu hii idara ubadilika kuwa adui wa siri wa kiongozi.
Labda nitoe mfano kule Israel mtendaji mkuu wa shughuli za taifa ni waziri mkuu. Waziri mkuu wa Taifa la Israel ni mtu mwenye nguvu sana na mpaka majeshi anaweza yapeleka vitani na kwa wenzetu wame advance huwezi fikia nafasi ya uwaziri mkuu kama hujafanya jambo zito lakijasiri kuitegea nchi yako. Una ambiwa kwa mfano waziri mkuu mstaafu Bwana Benjamin Netanyau ni moja ya mawaziri alie fikia level ya ukomandoo na sio tu komandoo tu jamaa na IQ 153 kama sijakosea yani ni moja ya mawaziri ana akili sana na sio hivyo tu ila kaka yake ni among most intelligent and among the special unity ktk kukomboa mateka kule uganda ila alikufa kwa bahati mbaya na mpaka leo taifa lina omboleza juu ya kifo chake.

Niende kwenye kile nataka kuwaambia kule israel alitokea waziri mkuu mmoja anaitwa Isack Rabin waziri mkuu huyu alifanya tukio ambalo kwa taifa la Israel nikuuwawa alifikiri kwa ushawishi aliokuwa nao na nguvu atawaunganisha Israel na Palestinian na kurudisha ardhi ya Palestinian. Jambo hili alofanikiwa ila aliporudi nyumbani Isack Rabin alipigwa Risasi na kufa hapo hapo na kijana alie kuwa ktk team ya wafuwasi wake.
Jambo la ajabu sana ktk tukio hili nikuwa kulikuwa na taarifa za siri sana kwamba kijana alie muuwa waziri mkuu alikuwa ni kijana alie pikwa kwa siri na team ya mossad ili kumu eliminate waziri huyu kwasababu alikuwa aki hatarisha masilahi mapana ya usalama wa Taifa hilo.
Mossad ni moja ya idara za usalama wa taifa la israel inayo ogopwa na mataifa hata makubwa na kama ulikuwa ujuwi idara hii inaheshimika mpaka na idara nyeti kama CIA, M16 ya UK pamoja na KJB nk. Idara hii haijawahi shindwa na data zake mara zote 100%
Mpaka leo kijana huyo yupo mahabusu na haijajulikana nani alie mtuma.

Rais wa Taifa kufa madarakani ni jambo lahatari sana maana huwa ni kama kibali cha kuuwa kwa jina la jamuhuri. Watu hufa watu hupotea kwa jina la jamuhuri niwakati hata wale wapo madarakani yawapasa kuwa makini na midomo yao ama mawazo yao. Niwakati ambao kama umepewa kurithi kiti basi kuongoza mka pale muda unaisha wa alie fariki nankukaa pembeni wenye nchi wamchaguwe wanaye mtaka ama usubiri kuona giza mbele kama giza liliwakumba watu wa zambia.

Sio muda eti kutangaza nia hapana epuka huwo mtego maana utaonekana mchawi. Nakufanya walio ktk upelelezi wa kifo cha Rais alie kufa kukuweka ktk list ya mambo yakuhisi.
Vyama vya upinzani nilazima kuwa makini hasa hiko kipindi maana unaweza jikuta mna hangaika na mtu msie muona why ni aina hii ya kazi ile team wanafanya.
Naandika haya kama elimu kwa watanzania na makada kujuwa hiki kipindi nikibaya sana kuunda makundi au kuanzisha vuguvugu la nani awe Rais nikitisho kwa usalama wa Taifa na Taifa.
NB
Ndugu msomaji huu uzi una nia moja kuwaelimisha watanzania kuepuka piga siasa wakati Rais ana fariki akiwa madarakani uzi huu hausiani na mtu au kikundi cha watu ktk siasa.
End
Kwa hiyo unamshauri samia suluhu hassan apunguze speed ya kuonesh nia ?
 
Punguzeni kuangalia movie sana!

1.Umejuaje hayo?Wewe ni mtu wa ndani?
-Kama siyo umejuaje?Nani kakuhadithia?
-Kama ndiyo,mbona umeandika shallow sana?Mtu wa ndani huwa anaandika facts zilizoshiba na sio blah blah za kuokoteza!

2.Eti usalama wanaunganisha nguvu na nchi jirani kufanya uchunguzi!Really?Yaani taifa lipate msiba wa Rais halafu muanze kualika vyombo vya nje kuja kushirikiana kuchunguza kifo?Ni kanuni ya nchi gani?Tz au nchi zote?

Nways,kwenye huu uzi naona umeandikwa kwa hisia zaidi!
Uchunguzi Magumashi. Watuhumiwa namba moja kama kweli mnatafuta mchawi waanze na PSU ambao wako na Rais siku zote, masaa yote, dakika zote na sekunde zote.
 
Ulipofananisha MOSSAD na utopolo wa UVCCM waliojaa hapo St.Peter's nimekudharau sana.

Usirudie tena kufananisha MOSSAD na UVCCM.
Pole sana. Kwa africa ni #1. Mleta uzi anaonekana yupo well informed na this is just warning kwa wahusika. Ila ni hatari sana tena sana. Kumbe tuna vipindi vigumu sana mbele yetu kama taifa. Ina maana walioshangilia na wanaoendelea kushabikia kifo cha Dkt Magufuli wanaingia 18. Nimeogopa sana hii taasisi ya urais kumbe ni kubwa sana na inatisha.
 
Ila uliangalia kwa jicho la tumbusi ule mlolongo wa vifo kwa baadhi ya watumishi Ikulu kisha kumalizia na namba moja kuna ka uwalakini fulani hivi, kwa jinsi ninavyoifahamu CORONA imetumika kama subject matter kuficha kitu kwa uangalizi alikokuwa nao hayati kuna jambo linafichwa si bure.
Samia anahusika kwenye huo mchongo
 
Sasa kwa mifano yote uliyotoa, mbona umetoa conclusion kwa kuangalia upande mmoja TU?

Kwamba, Magu amefariki na kwahiyo SSH na wenzake wasijisahau kwa kuona ndo wameshatusua?

Mbona umesahau uwezekano wa kwamba, hao wanaoangalia maslahi mapana ya taifa, ndio waliom-eliminate Mheshimiwa Magu kama alivyokuwa eliminated Rabin?

Na kwamba, endapo above scenario ndio the right one, basi hapo hakuna cha upelekezi wa kuangalia kifo wala nini cuz' MISSION ACCOMPLISHED?!

Ndio nikijiuliza Mosad wajichunguze wakati wanajua walichofanya!!!!!!!
 
Asante sana mkuu kwa hii elimu. Hakika nimeshausoma sasa mchezo. Na kwa ulivyoelimisha nadhani 1 na 3 kazi iko kubwa mbele yao. Hakika Kifo cha Dkt Magufuli ni dhihaka kubwa sana kwa idara nyeti, maana eti wapinzani walifanya sherehe? Yaani baadhi ya viongozi wa juu wa serikali walishukuru na kushangilia kifo. Nadhani wengi hatukufahamu madhara yake. Ni muhimu Mungu amlinde Mama Samia. Tulimuombea sana Dkt Magufuli, na tulikuwa na nafasi ya kumuombea zaidi kama tungejulishwa anaumwa. Mungu hakika sijui ilikuwaje kuugua kwa Dkt Magufuli kuwe siri mpaka kifo chake. Kumbe kuna huo utaratibu tena wa vyombo vya ulinzi na usalama, hakika huu uzi ni muhimu sana kwa viongozi wote waandamizi, hasa waliojitokeza na kuonesha kuwa Wateule wa Dkt Magufuli hawafai kumbe wanaingia 18 za watu.
Unajua ndugu yangu wakati mwingine Mungu uruhusu jambo litokee pengine liwe baya au zuri anasababu zake. Mie si nabii wala mtume wala mchungaji.

Lakini mwaka 2019 niliota tupo Ikulu Dar, kuna sherehe kubwa lkn Magufuli hatumuoni, yupo tu Waziri Mkuu Majaliwa tukimuuliza Magufuli yuko wapi yeye hasemi anatuyeyusha.

Nikajiuliza sherehe kubwa ikulu? Tunakula vyakula kibao. Mwaka 2020, 2021 ndoto ilijirudia vile vile ila wakati huu nikaota Tanzania inarais mwanamke. Nikampigia Rafiki yangu mmoja nikamwambia labda uchaguzi wa 2030 Tanzania tutaongozwa na mwanamke. Anyway tukacheka yakaisha.

Mwaka 2021 February ndoto ile ikajirudia vile vile. Ila wakati huu watu walikuwa hawana raha, Usalama wa Taifa walikuwa busy. Nilijiuliza tu hii ndoto inamaana gani? Sikujali. Ndo baada kusikia Magufuli kafariki ndo sasa nikakumbuka ndoto nilio iota kwa miaka mitatu mfululizo.
Mtoa mada msije mkaniingiza kwa wale watu wakuchunguzwa. Tafadhali hii ilikuwa ndoto tu!
 
Niwakati ambao kama umepewa kurithi kiti basi kuongoza mka pale muda unaisha wa alie fariki nankukaa pembeni wenye nchi wamchaguwe wanaye mtaka ama usubiri kuona giza mbele kama giza liliwakumba watu wa zambia.
Hili umeliona leo tu. Wenye nchi wachague wanayemtaka ama asubiri Giza kama la Zambia??

ccm ilishakufa inadumu kwa nguvu ya kamba mbovu. Muda si mrefu itakatika.
 
Ndugu haya mambo ni kweli yanawezekana ila cyo kwa nchi Kama hii

Hyo Mambo Ni kwa highly systematized countries ambazo mifumo yake ni imara na hai ingiliwi na power ya mwananchi namba mara nyingi hata mifumo yao ya Usalama iko independent kwa ajili ya ustawi wa taifa. Sio unafananisha na nchi ambayo kwnz unaingizwa kwny kwa interest ya mtu/watu fulani na unafanya kazi kwa matakwa yao unachekesha tu

Muwe mnaangalia basi na profile ya nchi za kuwa na mifumo hyo sio mnaongea ongea tu
Amenishangaza hapo kwa maslahi ya taifa. Mi siyaoni.
 
Ukosefu wa utulivu si vurugu mtaani au nn, bali unakuwa hasa kwa system nzima na wananchi. Inaweza kuwa kisaikolojia. Mfano, wananchi watakuwa hawajaelewa, direction ipi wataenda. Kuna kuwa na lugha ambazo mfano kukitokea jambo watu wanakimbilia kusema heri fulani angekuwepo? Haya mambo ni kisaikolojia inaitajika muda mpaka hapo watu watazoea na utulivu utaendelea.

Pia kutokuwepo utulivu ktk maswala mazima ya kiutawala. Hii mfano kuna makundi yatatokea yaweza kuwa ya siri au uwazi. Kuna ambao watakuwa bado wanamlengo wa kiongozi alopita, na ambao watakuwa ktk mlengo wa kiongozi aliopo madarakani. Hii haileti utulivu, hata Rais aliopo itakuwa inamsumbua kichwani. Ni mambo yanayohitaji muda. Tazama hata katuni ya kipaya, utajua nachoongelea.

Utulivu usiokuwepo ni wakisakolojia hasa kwa wananchi. Na pia utulivu usiokuwepo ni wakitawala. Rejea sasa Swala la machinga. Inaonesha viongozi wa mikoa kadhaa wanawatimua machinga. Viongozi wengine wanasema hapana Magufuli alikataa wasitimuliwe. Mama hataki toa maamuzi ya wazi kama Magufuli alivyofanya, alimwita SSH wakati huo akiwa makamu na waziri wa Tamisemi akasema Machinga wasibughuziwe, Mkuu wa Mkoa anae ona hataki kufuata maagizo ajiuzuru. Hii ilikuwa kauli ya JPM haikuwa na unafiki.

Mama yeye anasema wapangeni, lakn viongozi hawajali wameendelea kufanya watakavyo. Je hapa mama Rais wetu anaogopa kuchukua hatua? Make machinga hawapangwi bali wanafukuzwa. Hii ndo kutokuwepo kwa utulivu kiutawala, na mengine mengi.
Wananchi ni watu wazima....

Katiba ndiyo DIRA ya kila aina ya utata....

Ndiyo maana ukaitwa msahafu...HISIA HAZIWEZI ZIKAWA JUU YA UHALISIA KATIKA MAISHA YAENDELEAYO....

Hatuwezi kuishi ndotoni....JPM is no more...haijalishi tulimpenda vipi....kumpenda kwake ni KUYAISHI yale mazuri aliyotufanyia....na hatutakiwi kumuishi peke yake bali mazuri ya Marais wote waliopita tokea kwa baba wa Taifa hayati JKN.....

Nchi ipo....
Itakuwepo hata baada ya vitukuu vyetu na marais wao .....

#NchiKwanza
#SiempreJMT
 
Shida vijana wengi humu wanaushabiki tu, hawapendi kukiri ukweli wa mambo. Wakati tunakuwa , tuliambiwa Tanzania ni moja ya nchi inayoheshimika duniani kwa maswala ya upelelezi. Ila ni nchi isiyo na makuu. Ufanya mambo yake kimya kimya.
Sasa siasa hizi za leo ambazo watu wanadhani kudhalilisha au kutukana viongozi wakuu wa nchi na kukashifu Taifa lako na vyombo vya ulinzi ati ndo siasa za kukufanya uonekane wewe ni mjuvi wa mambo.
Kufa kwa kiongozi wa nchi ni sawa na kifo cha mzazi nyumbani, awe mama au baba. Familia utetereka kwa miaka. Hivyo tusikimbilie kusema nchi imesimama vizuri na kuanza kuropoka maneno tusiyojua.
Kitu kimoja kilinishangaza mama utadhani hii awamu ni tofauti na iliyopita, anasema alipoingia alikuta sijui shule kadhaa sasa anajenga kadhaa. Anajiweka kama vile hakuwepo kwenye serikali hilo pita. Anasahau yeye ni mwendelezo wa kumalizia awamu ya serikali iliyopita. Kwani alikuwa makamu wa Rais na ilani ni ileile inayotumika hakuna nyingine.
Mama anaanza kuona utamu wa madaraka, anajitangaza kuwa mgombea kabla ya wakati. Awe makini asipotoshwe. Hawezi achwa agombee tu bila kupimwa kuwa je ndo alikuwa chaguo baada ya Magufuli kama angemaliza muhula wake.
Nchi bado haijatulia, Rais wetu hasijione kafika. Na kuanza kujiona ana haki ya kufanya lolote!


Kwa hiyo ile picha maarufu kule USA inawezekana ilikuwa ni kipimo?
 
Unajua ndugu yangu wakati mwingine Mungu uruhusu jambo litokee pengine liwe baya au zuri anasababu zake. Mie si nabii wala mtume wala mchungaji.

Lakini mwaka 2019 niliota tupo Ikulu Dar, kuna sherehe kubwa lkn Magufuli hatumuoni, yupo tu Waziri Mkuu Majaliwa tukimuuliza Magufuli yuko wapi yeye hasemi anatuyeyusha.

Nikajiuliza sherehe kubwa ikulu? Tunakula vyakula kibao. Mwaka 2020, 2021 ndoto ilijirudia vile vile ila wakati huu nikaota Tanzania inarais mwanamke. Nikampigia Rafiki yangu mmoja nikamwambia labda uchaguzi wa 2030 Tanzania tutaongozwa na mwanamke. Anyway tukacheka yakaisha.

Mwaka 2021 February ndoto ile ikajirudia vile vile. Ila wakati huu watu walikuwa hawana raha, Usalama wa Taifa walikuwa busy. Nilijiuliza tu hii ndoto inamaana gani? Sikujali. Ndo baada kusikia Magufuli kafariki ndo sasa nikakumbuka ndoto nilio iota kwa miaka mitatu mfululizo.
Mtoa mada msije mkaniingiza kwa wale watu wakuchunguzwa. Tafadhali hii ilikuwa ndoto tu!
Aisee Mungu alikutumia. Sasa ninavyoona kumbe tuna safari ndefu kwa sababu ukiangalia 90% ya viongozi wakubwa serikalini kuna kauli wamezitoa za kushangilia/kufurahia kifo cha Dkt Magufuli. Kumbe maskini hawajui kumbe ni kuidharau idara nyeti. Mpaka hapo 2025 haijulikani kabisa. Jambo lingine ilikuwaje Mama akatangaza nia wakati bado hata mwaka haujaisha???? Nani alimshauri???? Kwa sababu ukiangalia ni kama taifa bado lipo linaomboleza, yaani ni tofauti kama rais Dkt Magufuli angeondoka kupitia njia za uchaguzi nadhani Mama tungemzoea haraka na idara nyeti ingekuwa imejiandaa. Ila kwa hili mtu waliyemuandaa for almost a decade then aje afe kizembe tena kwa kufungiwa na taifa lipate taarifa tu ya kifo tena wengine wafanye sherehe dahhh sijui
 
Wananchi ni watu wazima....

Katiba ndiyo DIRA ya kila aina ya utata....

Ndiyo maana ukaitwa msahafu...HISIA HAZIWEZI ZIKAWA JUU YA UHALISIA KATIKA MAISHA YAENDELEAYO....

Hatuwezi kuishi ndotoni....JPM is no more...haijalishi tulimpenda vipi....kumpenda kwake ni KUYAISHI yale mazuri aliyotufanyia....na hatutakiwi kumuishi peke yake bali mazuri ya Marais wote waliopita tokea kwa baba wa Taifa hayati JKN.....

Nchi ipo....
Itakuwepo hata baada ya vitukuu vyetu na marais wao .....

#NchiKwanza
#SiempreJMT
Nilichokuwa naongea ni ufafanuzi wa hoja kuelezea juu ya hali ya utulivu hasa wa kisaikolojia na utawala kutokuwepo. Hii haimaanishi kuwa haya hayatokwisha. Yataisha ila ni kawaida ya binadamu. Hata nyumbani wazazi wanapofariki hali ya sintofahamu utokea, na baadae hali uwa sawa.
Kuhusu katiba ndugu yangu, katiba si jambo linaloleta maendeleo. Unaweza ukawa huna katiba bado ukapata maendeleo. Nchi nyingi za mashariki ya kati hazina Katiba lakini zimeendelea. Angalia tu huko Dubai. Waingereza hawana katiba iliyoandikwa lkn wameendelea.

Zamani hata wazee wetu hawakuwa na katiba lakini waliishi kwa kuwa na uongozi imara.
Kikubwa ni kupata viongozi weye nia njema ya kuleta maendeleo katika nchi, walio wazalendo. Kwani hii katiba tulionayo kuna sehemu inazuia maendeleo? Hakuna, shida tuna viongozi waliojaa tamaa na wabinafsi, Hii haijalishi wako chama tawala au wako Upinzani.
Pia demokrasia haitokaa ituletee maendeleo, wazungu wametutega nasi tumeingia bichwa bichwa. Angalia nchi zote zilizoendelea duniani pamoja na hiyo marekani, hazikuendelea kwa mfumo wa demokrasia. Marekani yenyewe wanawake wameanza kuruhusiwa kupiga kura miaka ya 60, wakati uhuru walipata toka karne ya 18.

Sweden ilikuwa nchi ya utawala wa Mfalme ambae alikuwa mkorofi na tunaweza mwita dikiteta, alilazimisha wananchi wake kulipa kodi, mambo mengi aliamua yeye mwenyewe. Lakini leo ukienda Sweden wanamuona ndo Baba wa Taifa lao, wanasema japo alikuwa dikiteta lakini aliwapa maendeleo, hawamsemi vibaya, na alipenda vita.

Dubai, mtawala wake wa kwanza aliota ndoto na kuanza kuijenga, hawana cha balaza la mawaziri. Alipofariki, mrithi wake akasema atatimiza ndoto ya aliepita kwanza, akimaliza anaanza naye anavyotaka dubai iwe. Angalia China, Ujerumani, Urusi na nyingi nyinginezo ulikuwa ni udikiteta ndo umeleta maendeleo.

Mfano tu angalia Zanzibar, Yale majengo ya Michenzani na kwingineko huko shamba, mabomba ya maji wao wanaita mifereji na barabara kwenda shamba, haya yote yalifanyika kipindi cha hayati Karume. Unaambiwa yeye hakuwa msomi ila alikuwa katoka nje, alisafiri akifanya kazi ktk meli, akaona dunia ilivyo. Alipokuwa Rais alikuwa anatamka tu, jenga hiki hivyo hayo majengo yalijengwa hata bila ramani yaani alitamka ujenzi ukaanza hata nae alishiriki katika ujenzi. Alieneza maji vijijini, na kujenga barabara. Haya yote alitamka na ikafanyika.

Nambie na demokrasia yetu, ni Rais gani wa Zanzibar kaweza fanya alofanya Karume.
Huyu Karume Mungu angeendelea muweka Zanzibar ingekuwa mbali, alikuwa kiongozi mwenye maono na maamuzi. Hiki ndo kinatakiwa. Wala hakuwa hawa wanasiasa wanaoilalamikia Bara kuwa inainyonya Zanzibar. Yeye alifanya. Na Zanzibar ilipiga hatua, Zanzibar ilikuwa ya kwanza kuwa na Television ya rangi Africa. Hii yote ni Karume.
Viongozi wa leo wamejawa tu na ubinafsi na tamaa za madaraka na kujitajirisha ila hawana maono na uzalendo. Wanabaki kusingizia mara katiba mara muungano.
 
Nikuulize swali,
Mfano raisi Magufuli alovogariki, unataka kusema nchi ilikuwa kwenye hatari? Kivipi? Hatari gani? Hebu fafanua?
Huyo aliyeandika huu uzi, anaonekana ni sukuma gang😁

Bado anaweweseka na kuondoka kwa Mwendazake
 
Kipindi baada ya Rais kufariki ni kigumu lakini sio kwa sababu ulizo orodhesha. Sinto fahamu hiyo inaweza kuleta vurugu ndio maana ni muhimu kufata utaratibu na kubadilisha viongozi kama ipasavyo
 
Back
Top Bottom