Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?

Mwaka ujao tutaona kila rangi tusioiona
 

Soma vizuri kilichoandikwa na mtoa hoja, siyo kukurupuka!
 
Mkuu Kinyungu asante kwa kuliona hilo,sio wewe peke yako umeguswa na hili,
Kila mtanzania mwenye kujituma na asiyetegemea vya bure linamgusa.
Naamini rais anafanya makusudi kwani anajua anaowahutubia kuwa hawawezi kumchallenge,
Huwa najiuliza wazee wa dar ni akina nani nchi hii hata wapewe heshima ya kuhutubiwa maamuzi magumu ya kitaifa?
Basi ingesemwa rais anawahutubia wazee wa nchi nzima kupita wazee wa dar hii ingekuwa na mantiki,
Lakini hili la kusema wazee wa Dar halina mantiki yoyote.Kwa nini asiwe anatoa hotuba
kama hizi kwa wanazuoni hata pale pale ikulu ili washauriane kwanza kisha ahutubie taifa
kama afanyavyo kila mwezi,badala ya kujificha kwa wazee wasiojua lolote isipokuwa kupiga makofi?
Nasikitika,kwani wengine tunafanya kazi kwenye makampuni ya kigeni.
Tunazuiliwa kulipwa fedha ya kigeni eti ni heshima kwa fedha ya nchi yetu,
wakati Rais ambaye ndiye mzalendo namba moja anaidharau sarafu yake mwenyewe.

Sasa kila mtu hapa aone madhara waliyotuletea wabunge wa BMK kwa kuondoa
kipengere cha kupunguzwa kwa mamlaka ya rais,na rais kushtakiwa
Huu ni ulevi wa madaraka na wanafanya wakijua kuwa wana kinga,tunataka katiba itikayowawajibisha watawala wa namna hii,Naungana na wanaosema katiba isipite mpaka mambo muhimu yaliyopendekezwa na kufutwa na mafisadi yarejeshwe.Madhara ya kupingwa kwa rasmu ya Warioba katika sakata la ESCROW yamejionyesha wazi,
Shime wananchi tujitokeze kwa wingi kuikataa katiba pendekezwa hadi itakaporudishiwa minofu iliyonyofolewa kwa manufaa ya watawala.
 
Last edited by a moderator:

Inaweza isiwe na athari ya moja kwa moja kwenye uchumi

Lakini ni ishara ya "Dharau" kwenye fedha yetu
 
Binafsi nimeelewa ni kwa nini kila kitu lazima utasikia
''kwa msaada wa watu wa marekani''
Kumbe hela ya marekani ndo hela ya kwetu ni madafu.
Mh.ssenge analijua hili,wenye akaunti zao uswis wanalijua hili.
Kwa nini na sisi tunaofanya kazi makampuni ya kimataifa humu nchini tusiachiwe na sisi tulipwe hela
badala ya kutulazimisha tulipwe madafu?
 
Mkuu hapo ni kama wewe uambiwe "una degree ya chupi" - yani ni tusi na dharau inayoonyesha kwamba kisomo chako hakina thamani! Hivyo ndio kusema kwamba: "Pesa za madafu" maana yake ni pesa zisizo na thamani!

...asipokuelewa na hapo, nawa mikono, kung'uta miguu ushukuru kisha usepe.
 

Raisi hapaswi kamwe kuikejeli sarafu ambayo yeye ndo alipaswa aisimamie ili thamani yake iwe juu,kwa nchi nyingine zenye uwajibikaji hii ni skandali kubwa yenye uwezo wa kumjambisha mpaka atengue kauli.
Kutokuona kasoro pana ya raisi kutoa kauli kama hiyo ni upuuzi mwingine baada ya huo ulioutaja.
Nawasilisha!
 
Kwanza tujue chanzo cha jina hili "fedha ya madafu". Haya ni maneno ya mtaani. Kwa mfano jina "daladala" sasa
hivi ni jina la kawaida kwa mabasi madogo na imehamia mpaka magari makubwa yanayosafirisha abiria wa mjini na vitongoji vyake. Nakumbuka chanzo chake ni miaka ya 80 kulikuwa na vibasi vidogo hiace, town ace na namna yake ambavyo vilikuwa vikichukua abiria kwa kuiba (sio rasmi) kutoka Magomeni mpaka Posta na kwa kutumia njia zisizo rasmi na nauli ilikuwa ni Sh.5/= ambayo ndio ilikuwa ni sawa na Dola moja, na wakati huo UDA nadhani nauli ilikuwa ni Shs. 2/=. kwa hiyo wapiga debe wake walikuwa wakisema daladala badala ya Shs. tanotano kuzuga vyombo vya sheria. Kuna neno "Bodaboda" nalo asili yake ni maeneo ya mipakani ambapo pikipiki zilikuwa zikitumika kuvusha watu toka nchi moja kwenda nyingine kwa njia zisizo rasmi ambazo pia zimepachikwa jina" njia za panya". Yako maneno mengi ya aina hiyo mengine yanadumu na mengine yanapotea hizi ndio tabia za lugha. "Fedha ya madafu" chanzo chake ni fedha yetu (Shilingi) iliitwa hivyo miaka hiyo ambapo ilikuwa inaweza kutumika nchini tu ikimaanisha utaitumia kununua madafu ambayo yanapatikana hapa hapa na huhitaji fedha ya kigeni kuyapata. Watu walikuwa wanataka sana kumiliki fedha za kigeni km $ au Stg. ikawa ni sababu ya kushuka kwa thamani ya fedha yetu na hali ya uchumi ikichangia.

Je rais hawezi kutumia neno bodaboda? au daladala? au njia za panya? au Lumbesa? Ninachoweza kusema ni kwamba Raisi ametumia neno lililoanza kupitwa na wakati kwani kwa sasa unaweza kupata fedha za nje kwa manunuzi halali bila matatizo, na ndio maana mwekezaji aliweza kuwekewa malipo yake kwa fedha za Kitanzania. ALIKUWA SAHIHI KUTUMIA NENO HILO.
 
Mimi sioni kama kuna tatizo lolote kwa rais kuita pesa ya tz pesa ya madafu. Acheni kumtafutia sababu bna huyu rais , mwacheni amalize muda wake vizuri. Ametuongoza salama mpaka kufikia hapa. Huko kuita pesa ya madafu ni utani tu wala sio chochote seriouz. Na hata hvyo pesa yetu ndio inavyoitwa,,, kwani kuna asiyejua??
 
Unadhani Nyerere alikuwa mjinga kumkataa huyu mswahili wa M.so.g.a?Nyinyi mkajifanya kiherehere kumtaka awe rais wenu eti atawaletea maisha bora,Haya mvumilie sasa maana haya matatizo mliyataka wenyewe!
 
Reactions: SMU

Hata sisi tunaita pesa mkwanja,mapene,mpunga,dinyilu,kisu nk hzo ni nicknames za pesa lakini "madafu" ni kejeli kwa pesa yetu kutokana na kutokuwa na thamani.
Inakuaje raisi anafurahishwa na kubariki kejeli hyo badala ya kusikitika?
 
'Hela ya madafu' ni fedha yenye thamani ndogo,na kweli fedha yetu imeshuka sana thamani kwasababu ya sera zake mbovu za kiuchumi na kifedha pamoja na ufisadi mkubwa unaoendelea kwenye fedha za umma.
 

Hajaikashifu,ila sababu ni nadra sana kuitumia ndiyo maana anaiita hela ya MADAFU.Si wajua akienda zake kupumzika anatumia zile pesa za MFADHILI aliyetunyima mshiko wake?
 
Mkuu,
Bora wewe angalau umeeleza maana ya neno madafu.

Thanks
 

Kamanda, hayo majina ya hizo pesa ukiyatafsiri je yanaleta ukakasi hasi? Utamkwa na wakuu wa nchi hizo wakati wa kudadavua masuala nyeti?
 

= uhalisia
 
Hata sisi tunaita pesa mkwanja,mapene,mpunga,dinyilu,kisu nk hzo ni nicknames za pesa lakini "madafu" ni kejeli kwa pesa yetu kutokana na kutokuwa na thamani.
Inakuaje raisi anafurahishwa na kubariki kejeli hyo badala ya kusikitika?
Mkuu,
Kwa nini unaita pesa yetu mkwanja, mapene, mpunga, dinyilu na kisu?. Huoni kama hii ni dharau kwa sababu kuna jina lake kisheria ambalo ni shilingi.

Kama hiyo siyo dharau, kwa nini kuita madafu ndiyo iwe dharau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…