Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?

Fedha ya nchi yako unaidharau halafu ukizingatia yeye ndo President hajui kwamba hiyo aibu ni yake na inaonyesha wazi kwamba kuna jambo halipo sawa kwenye uchumi.
 
Jamani mimi pamoja na mengi yaliyonichukiza kwenye hotuba ya Rais ya hivi karibuni hili la kiongozi wa dola hii ambae kwa siku za zaman hata picha yake ingekuwa kwenye pesa ya kitanzania kuiita pesa yetu inayotusumbua kila siku kuwa ni pesa ya madafu. Imenishangaza sana hasa kwa status yake. Hakupaswa kabisa kutumia lugha hiyo akiwa kama Rais. Hizo lugha ni za mtaani na awaachie walioko mtaani. Yeye alieko Ikulu anatakiwa ku behave kama mtu anaeishi Ikulu na mwenye dhamana na serikali hii ikiwemo pesa na uchumi wa inchi hii. Nimejiuliza mengi sana baada ya kauli hii.
1. Au wao wana madollar nje ndo maana they dont care?!!!
2. Au ndo kusema hawashuguliki tena hata kuhakikisha pesa hii ambayo leo inaitwa ya madafu na kiongozi wa inchi ipande thamani na iwe juu?!!!
3. Ina maana kushuka thamani kwa pesa yetu kwao ni furaha na ndo maana bila kujali wanaishusha zaidi thamani kwa kuiita ya madafu?!!!
IMENIUMA SANA!! Tunahitaji Rais mwenye uchungu na uzalendo wa inchi hii.
 
Rais kwa maneno yako inaonyesha ni jinsi gani usivyopenda nchi na watu wake huna hata chembe ya uzalendo kwa kejeli.

Hiyo ni lugha ya mwizi aliyebobea. Najaribu kulinganisha nidhamu aliyokuwa nayo wakati wa kugombea urais mara ya kwanza na alivyo sasa. Kila mtu anajua kuwa hata urais hakushinda kwa haki bali alidhulumu ndiyo maana hakuna jipya lenye kumpa heshima au sifa ambalo amelifanya. Ameturudisha nyuma miaka kumi. Huyo ni mla rushwa na fisadi nambari wani. Labda akumbukwe kwa hilo na kwa kuua na kutesa wengi katika utawala wake...
 
Uchumi imara unatengenezw na wanasiasa, sasa sarafu dhaifu pia hutengenezwa na wanasiasa.jk kaua sarafu yetu.kmbk kabla hajaIngia Ben aliacha 1100=1us, sasa hv 1800.increased by 70pct. Akili za kimadafu madafu zimetengeneza sarafu madafu,,!!!!
 

Hizo ni lugha za mtaani. Rais wa USA au Prime Minister wa UK hatumii. Unapokuwa kiongozi kuna lugha ya kutumia.
 
Wamezoea mara vijisenti nahisi kwakuwa hazitoki mfukoni mwao ni za msaada zao toka tra wanaweka 10% escrow zikijaa wanagawana.
 
atafutwe mwigulu aje alitolee ufafanuzi kama ni sahihi kuita Tsh ni hela ya madafu.Wanaiba halafu wanatumia lugha za kuwafanya watz kuiona hela yao haina thamani.chenge aliiba akaita vijisent, na huyu kaka mkuu anaita "hela yenu ya madafu" as if yupo kijiweni.hivi hazina wanamlipa in terms of what usd au Tsh?
 

Acha uongo tunaposema hela Ya madafu ni hela ndogo ndogo isiyokuwa na thaman
 
si vyema kuita hela ya madafu kwakuwa rais anapaswa kutumia lugha rasmi popote anapoongea na wananchi wake..si vizuri kuweka utani katika mambo nyeti yanayogusa nchi..
 

Ndugu umeshasikika hii thread yako una paste kila mahali sijui unatafuta umaarufu
 
... Huyo Ni Rais Wa Tanzania Aliyeongea Ukweli Au Kudharau Thamani Ya Fedha Ya Nchi Yake. Hahahahahaaa. Sijapata Ona Rais Kama Huyu. Tanzania Ina Maadabu Mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…