PreGE2025 Rais wa Serikali ya Wanafunzi UDOM, Mohamed Abdallah: Nikihitimu chuo kikuu naenda VETA

PreGE2025 Rais wa Serikali ya Wanafunzi UDOM, Mohamed Abdallah: Nikihitimu chuo kikuu naenda VETA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Halafu wanafikiri VETA utakwenda usomee mf. ufundi magari halafu ukitoka hapo unafungua li gereji lako unaanza kupiga hela. Hawajui kwamba vyuo vingi vya VETA havina walimu wabobevu katika baadhi ya fani na vingi havina karakana za maana. Labda serikali ifanye uwekezaji wa maana.

Wanaofaidi VETA ni wale ambao tayari wana kaujuzi japo kidogo huku mtaani na kule wanakwenda kuwa certified tu na kuwa professionals. Fundi bubu wa magari mtaani ndiyo hasa anafaa kwenda VETA lakini sidhani kama mtu hujui kabisa magari ndiyo uende VETA halafu ukitoka hapo eti uajirike mtaani.

Nina mtoto wa dada kahitimu ufundi magari anasema hakukuwa na practicals za maana na sana sana tu waliishia kuchora injini ya gari na mengine lakini hawakufanya mazoezi ya kutosha. Sasa hivi yupo anahangaika kujifunza udereva.

Ni mikurupuko tu as usual!
Bora wewe umesema.

Watu wanaona Shida ni degree, Wakienda Huko VETA wakamaliza na kuona still hamna kitu sijui wataenda wapi.
 
Mzee wangu 😅unaposema Huyu bwana mdogo sio smart una maana gani! Nijitolee mfano, mimi pia nina degree Ila nina mpango wa kwenda veta since three years back, nimeanza na kimoja kimoja, before ata hii kauli ya P.M

nimefanya kazi ya driving four years, out my professional ya Chuo, now nina qualifications ya kwenda kusoma madaraja makubwa and driving cars and operating machines ni my passion

Sasa sijajua mzee wangu unasemaje kwamba dogo si smart, huenda ana Maono yake lakini pengine anajisemea kwenda kama trend tu kuchase clout, 🤔
Veta umesomea nini?
 
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma, (UDOM) Mohamed Abdallah Mohamed amesema baada kumaliza elimu yake ya chuo kikuu anajiandaa kwenda chuo cha ufundi (VETA) kupata elimu ya ujuzi.

Akichangia mada ya Miaka Minne ya Uongozi wa Rais Samia katika Kipindi cha Mizani cha TBC1, Mohamed amesema kuwa Rais Samia amewagusa vijana katika maeneo mengi ikiwepo ongezeko la ajira kwa vijana na uboreshaji mkubwa wa vyuo vya VETA ambavyo vinawawezesha vijana kuajiriwa na kujiajiri.

Pia, Soma
Atangilie kabisa huko VETA, degree ya nini?
 
Mwanzo nilidhani shilingi ya Tanzania ndiyo pekee imeshuka thamani, kumbe hata elimu inazidi kuporomoka
 
Saizi nchi yetu hakuna tena reasoning, generation hii imepoteza sana mwelekeo, Zamani University students walikuwa wanaongea vitu kwa kujenga hoja, imagine huyu ndiyo Rais wa wanafunzi anaongea huu upuuzi........ inasikitisha sana
 
Kutafuta teuzi….Kuna madogo kibao wamepita Veta ila ni weupe kichwan…Hizi veta kama vilivyo vyuo vikuu vyuo vya kati na hata taasisi za elimu ya juu zimezalisha watu wengi tu wenye uelewa waliojiajir na wengine kupata nafas ya kujiajiriwa na serikali au private sectors lakin wengine wengi tu wa wahitumu hawa wa veta na hivi vyuo ni weupe hawawez kujiajir au hata kufit kwenye soko la ajira…Veta sio solution
 
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma, (UDOM) Mohamed Abdallah Mohamed amesema baada kumaliza elimu yake ya chuo kikuu anajiandaa kwenda chuo cha ufundi (VETA) kupata elimu ya ujuzi.

Akichangia mada ya Miaka Minne ya Uongozi wa Rais Samia katika Kipindi cha Mizani cha TBC1, Mohamed amesema kuwa Rais Samia amewagusa vijana katika maeneo mengi ikiwepo ongezeko la ajira kwa vijana na uboreshaji mkubwa wa vyuo vya VETA ambavyo vinawawezesha vijana kuajiriwa na kujiajiri.

Pia, Soma
Sasa kwa nini anasubiri mpaka apate Shahada ya Ualimu?....si aache chuo ajiunge moja kwa moja VETA ama aanze ujasiliamali wa kushona viatu ambao hauhitaji hata kujua kusoma na kuandika? Taifa linapitia changamoto kubwa sana hasa katika eneo la namna vijana waliopo mashuleni na vyuoni wanavyoweza kufikiri na kuchanganua mambo?
 
Wanaosema udom ni chuo cha kata sijui tuwapinge kwa hoja gani
 
Back
Top Bottom