Unakumbuka hata uliandika nini kabla ??? Tofauti ipo kubwa sana kati ya waandishi wa biblia
Katika Waandishi wanne wa Injili Hakuna hata mmoja aliyekuwa Mwanafunzi wa Yesu (AS).β
Katika (Luka 6:14-16 na Marko 3:17) tunaona yametajwa majina ya wanafunzi kumi na wawili na Yesu (AS). Huku majina Mathayo na Yohana yamo, na majina Marko, Luka na Paulo hayajatwaja.
Hata hivyo, kutokana na nkuu zifuatazo, utagundua kuwa hizo Injili mbili zinatajwa kuwa ni za Mathayo na Yohana kwa kuwaheshimu tu, kwani ziliandikwa na mtu wa tatu. Soma nakala halisi ya mstari wa (Mathayo 9:9):
"Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani aitwaye Mathayo, akamwambia nifuate. Akaondoka akamfuata."
Na katika (Yohana 21:24):
"Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya; nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli?"
Katika aya ya kwanza, mwandishi anasimulia tu kile kilichotokea kati ya Yesu (AS) na Mathayo, huku katika aya ya pili, ni wazi kuwa kiwakilishi βnasiβ kinawakilisha mwandishi.
Hebu kwa sasa tutafakari juu ya kile kilichosemwa na waandishi wawili wa Kikristo kuhusu kuundwa kwa Biblia:
βWakati mwingine, Wanukuzi wanatia kile kisichokuwemo katika maandishi, pia kile wanachokifikiria kitakuwemo. Mnukuzi anaweza kuamini kumbukumbu zinazobadilika, au anaweza kuunda maandiko kwa mujibu wa mtazamo wa madhehebu anayoyafuata.
Kwa kuongezea katika matoleo na manukuzi ya Mapadri wa Kikristo, takriban (Miswada) ya Mandiko Matakatifu elfu nne ya Wagiriki [MSS], ilijulikana kuwa ipo. Kwa hiyo, tofauti za usomaji ni jambo la kuzingatiwa.β
Kwa hiyo Injili ziliundwa, na ambazo kiwaziwazi, ziliakisi mitazamo ya ufahamu wa mahitajio na matumizi ya jamii za waandishi. Kwao wao, vitu vya kimila vilitumika, lakini kulikuwa hakuna kusita katika kukibadilisha kile kisichoendana na lengo la mwandishi.