JPM TUNAKUKUMBUKA;-
Leo ndugu yangu amejeruhiwa vibaya na kundi la vibaka baada ya kukataa kuwapa password za simu yake wafanye miamala,tukimpeleka hospital akiwa katika hali mbaya damu zikichulizika kama maji alikuwa akitamka "JPM niokoe,JPM niokoe" nikaanza kumtafakari upya Mzalendo,Kipenzi cha watu Rais John Pombe Magufuli,nimegundua katika mioyo ya Watanzania ndani kabisa yupo Rais John Pombe Magufuli,Pumzika kwa amani Shujaa.
Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika maisha yake alikuwa ni mzalendo halisi ( true patriot ) na aliyeweka maslahi ya Taifa letu mbele kuliko maisha yake Binafsi . Pia aliyebeba falsafa ya umajinuni wa Afrika ( Pan ___ Africanist ) ambaye aliishi katika maono na matamanio ya kumkomboa mtu mweusi kutoka katika minyororo ya mabeberu na kumpa uhuru wa kiuchumi . Tuendelee kumuombea kwa mwenyezi mungu ili ampe pumziko la amani Shujaa wetu . RIP Dkt John Pombe Joseph Magufuli