TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Mbaya zaidi alishupaa kuyasema hayo akiwa kwenye mimbari ya msikiti na siku tukufu ya Ijumaa. Ama kweli aliyesema tusichanganye dini na siasa hakukosea!
Nadhani viongozi wa dini zote wamejifunza kutoka kwa utawala wa Kishetani wa Jiwe. Kuanzia sasa wasiruhusu Mwanasiasa yeyote kusimama kwenye mimbari na kuongea pumba,hata salamu iwe marufuku.
 
Duh pole aisee kumbe ulikuwa huamini zile taarifa za akina vigogo na wenzake ulijua ni uongo .Nakubali sana raisi wetu alikuwa ni mtu wa maombi sana hata kama angekufa basi hata cku mbili engepata nafuu ya kutusalimia lkn ni uongo wa serkali uliwaaminisha Watanzania kama raisi ni mzima na anafanaya kazi zake Lawama zote ni za wale waliosema uongo.
 
Mungu ni Mungu. Watanzania miaka sita alitupa tujifunze kuwa kuna viongozi vichaa hutawala dunia kaamua apitie kwetu natumaini mmejifunza wote mliokuwa wateule.

Katikati ya pandemic kama hii yeye havai barakoa na nyie hamvai. Gonjwa limefyeka top layer ya ikulu. Bado makamu naye anafanya ziara. Ni muda tupambane sasa na corona. Pumzika Dr Magufuli. Umeacha funzo kwa Watanzania.
 
Kuna mambo ya kuleta uongo lakini kitendo alichofanya katelephone ,ze comedian chalamila ,mwigulu ni utopolo....Huawezi kudanyanya afya ya rais kwa kusema yupo safi anachapa kazi wakati mtu yupo ICU.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…